Kunafah (Vitamu Vya Nchi Za Sham)

 

Kunafah  (Vitamu Vya  Nchi Za Sham)

Muda wa kutengeneza - dakika 20

Muda wa kupika - dakika 25

 

Vipimo

Kataif Pastry  (Tambi za Kataif) - ½ Kg = Pakti moja 

Cheese ya Mazorella - ¼ Kg 

Cheese ya Ricotta - ¼ Kg

(Ukipenda tumia Cheese ya Ricota pekee hivyo itakuwa ½ Kg)

Maziwa - ½  glass

Siagi au samli (iliyoyayushwa) - ½ kikombe

 

Shira

Maji - 1 ½  Kikombe

Sukari - 2  Vikombe

Zaafarani (iroweke na maji kidogo)

 

Namna ya kutengeneza

1.*Kata karatasi ya Wax paper size ya bakuli uweke katika bakuli la Pyrex (la kupikia ndani ya  oven) Bakuli lisiwe lenye shimo sana (sio deep)

*sio lazima kuweka karatasi ya Wax ukipenda tu.

2.Kwaruza (Grate) cheese ya Mazorella na ya Ricotta ichanganye pamoja kisha weka katika bakuli.   

 

3.  Tia maziwa yamoto kidogo katika cheese na changanya  vizuri.  Kisha  ingandamize vizuri ikae sawa katika bakuli.

 

4.  Katakata Tambi za Kataif ndogo ndogo  kwa mkono na kuzichambua  kama urefu wa 3 cm na kuziweka zote  katika bakuli .

 

 

5. Pasha moto siagi au samli katika Microwave.  Nyunyiza katika Kataif uliyoichambua katika bakuli itaipa rangi ya dhahabu.

 

 

6. Kisha weka Tambi za Kataif juu ya cheese uliyokwishaweka katika bakuli ya Pyrex na ieneze vizuri kote huku unaigandamiza katika cheese
ili igande humo.

 

7.  Pika ndani ya oven kwa dakika  20- 25   katika moto wa 300- 350  Deg au  mpaka uanze kuona imebadilika rangu kama ya dhahabu kidogo.

8.  Itoe katika oven  iweke nje ipowe.  

9.  Kisha pika shira   kwa kuchemsha  maji na sukari na ipike mpaka shira iwe nzito kidogo sio sana .Weka Zaafarani  uliyoiroweka na maji kidogo.   Unaweza kuongeza rangi ya machungwa ukipenda kuipa rangi zaidi.  

 

10.  Mwagia shira juu ya Kunafa.   Ikate kate vipande   vya mraba (square)   kwenye bakuli.       Na sasa iko tayari kuila.

 

Kidokezo  (tips)

Inapendeza kuila vugu vugu.

 

Share