Viazi Vya Kuoka

Viazi Vya Kuoka

Vipimo  

Viazi -  8-10

kitunguu - 1

pilipili mboga(kijani/jekundu) -  1

pilipili manga - kiasi

chumvi -  kiasi

siagi - 2 vijiko vya chakula                                        

Namna Yakutayarisha 

1. Vioshe viazi vizuri kisha kata kila kiazi vipande vinne na maganda yake kisha vichemshe kidogo tu na chumvi mwaga maji tia kwenye treya ya kuchomea.

2. Kwenye kikaangio kaanga vitunguu na mapilipili mboga kiasi halafu mwagia kwenye treya ya viazi.

3. Changanya na chumvi na pilipili manga kisha tia kwenye oveni kwa moto wa 350°F kwa dakika 15-20 vitoe na tayari kwa kuliwa.

 

Share