Sheer Khurma (Pakistani) Tambi Za Maziwa
.jpg)
Vipimo:
Tambi nyembamba
(Za brown tayari zimeshachomwa (roasted))
Samli 3 vijiko vya supu
Maziwa 7 gilasi
Sukari 1 kikombe
Siagi 2 Vijiko vya supu
Njugu za Pistachio
(zilizokatwa ndogo ndogo) ½ Kikombe
Lozi
(Zilizomenywa na kukatwa ndogo ndogo) ½ Kikombe
Zabibu kavu ½ Kikombe
Hiliki ½ kijiko cha chai
Vanilla 2 kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1) Zikatekate tambi na zikaange kidogo tu kwa samli.
2) Tia maziwa gilasi 5 kwanza
3) Tia sukari, pistachio, lozi, zabibu, hiliki na vanilla.
4) Wacha ichemke kidogo tu kisha epua wacha ipowe.
5) Ukumbusho: Hazitaki kupikwa
6) Ikishapowa tia siagi na maziwa gilasi 2 yalio baridi
7) Mimina katika bakuli kisha pambia juu yake lozi nyingine kidogo.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
