Maiti Aliyekwishaswaliwa Anafaa Kuswaliwa Tena?

 

 

Maiti Aliyekwishaswaliwa Anafaa Kuswaliwa Tena?

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Naomba kuuliza maswali mawili kuhusiana na maiti kwa vile nimependezewa sana na uchambuaji wa namna mnavyojibu mas-al na In shaaAllaah ALLAAH  awazidishie ilmu mtufumbue macho na sisi.

2 -Je, maiti ambae ameshaswaliwa kule ambako amezikwa jee inafaa kumswalia tena sehemu nyengine? 

 

 Majibu naomba yawe na ushahidi wa mambo mawili:-

 

 

1. Quraan

2. Hadithi Sahihi

 

 

JIBU:

 

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

 

Kwa ufupi Swali hili linahusiana na Swalaah ya ghaibu. Katika suala hili wanachuoni kutegemea Hadiyth za Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), wamegawanyika makundi matatu:

 

 

1-Inafaa Swalaah ya ghaibu kwa maiti hata kama ameswaliwa: Hii ni rai ya Imaam Ash-Shafi‘iy, Ahmad katika riwaayah yake moja. Dalili yao ni kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), aliwahimiza watu kwenda kumswalia an-Najjaashiy siku aliyoaga dunia, akatoka na Maswahaba zake mpaka kwenye mswala na kupiga takbira nne [Muslim kutoka kwa Abu Hurayrah [Radhwiya Allaahu 'anhu].

 

 

2-Haifai Swalaah ya ghaibu na kuwa Swalaah ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa an-Najjaashiy ni maalum kwake, hivyo isifanywe kwa kila mmoja. Hii ni rai ya Abu Haniyfah na Maalik.

 

 

3-Inafaa kuswaliwa Swalaah ya ghaibu kwa aliyekufa katika ardhi na hakuswaliwa na akiwa ameswaliwa tu sehemu hiyo haitofaa kuswaliwa tena Swalaah hiyo ya ghaibu. Hii ndio rai iliyochaguliwa na Shaykhul Islaam Ibn Taymiyyah na Imaam  Ibn ‘Uthaymiyn. Dalili yao ni kuwa haikuhifadhiwa kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali Swalaah ya ghaibu ila kwa an-Najjaashiy kwa kuwa alikufa katika Ummah mushrik wasiojua wala kutambua Swalaah. Japokuwa kulikuwa na Waislamu waliokuwa wakiishi huko Habasha (Ethiopia) hawakujua kabisa jinsi ya kutekeleza wajibu huo. Hii ya mwisho ndio rai yenye nguvu kufuatwa na Waislamu.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

Share