Du'aa Gani Ya Kumsomea Maiti, Na Je, Inafaa Kumsomea Maiti Suwrat Yaasiyn?

 

Du'aa Gani Ya Kumsomea Maiti, Na Je, Inafaa Kumsomea Maiti Suwrat Yaasiyn?

 

Alhidaaya.com

 

 

Swali La Kwanza:

 

 

Asalam alaikom warahmatu llahi wabarakatu,kwa kuanzia tu tunawashukuruni sana kwa wale wote waanzilishi wa tovuti hii inshallah Mola awazidishie juhudi za kutuelimishe.... ameen  suali ni kama hi shekhe naomba unipe kwa undani zaidi ya kuaa surat yaasi  haimfalii lolote yule anaesomewa?ikiwa kaburini ama nyumbani? naomba ufafanuzi zaidi. natumai nitapata muongozo mzuri ju ya hili inshallah

 

 

Swali La Pili: 

 

Ama Baada Ya Kumshukuru Allah Na Kumtakia Rehma Nabiy Wetu Muhammad (saw) Napenda Kuuliza Swali Hili Ni Dua Gani Inayofaa Kumsomuombea Maiti Au Ni Sura Gani Inayofaa Kusoma Pindi Unapokwenda Makaburini?maana Baadhi Ya Mashekhe Wetu Huwa Wanasema Kusoma Hitma Ni Bidaa Na Wengine Wanasema Haitakiwi Unapokwenda Makaburini Kusoma Suratul  Yaasin Na Wengine Wanapinga Hilo Je Ipi Inayomfikia Maiti? Please Nisaidie .je Hii Ni Kweli Naomba Mnisaidie.

 
Sina Zaidi

 

 

JIBU: 

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Kuhusu kumsomea  maiti Qur-aan hakuna dalili kwamba inapasa kufanya hivyo. Kumsomea khitma ni mambo ya bid'ah na ni amali ambazo hazina thamani mbele ya Allaah wala hazimfai kitu maiti.

 

Soma Maswali na Majibu pamoja na mada katika viungo vifuatavyo uzidi kupata elimu ya mas-ala haya:

 

 Kumsomea Khitmah Maiti, Kumchinjia Na Kumuombea Duaa Kwa Pamoja

 

Mambo Yanayofaa Kumfanyia Mzazi Aliyefariki

 

Kumsomea Qur-aan Maiti Akishazikwa

 

Khitmah Kutokufaa Na Madhara Yake

 

 

Na kuhusu Suwrah Yaasiyn pia hakuna dalili kuwa Suwrah hii inafaa kumsomea maiti. Soma pia Swali na Jibu lifuatalo upate ufafanuzi zaidi:

 

Fadhila Za Surat Yaasiyn Na Al-An-aam

 

Inavyompasa maiti ni kumsomea du'aa ifuatayo iliyothibitika katika Sunnah ambayo anaweza kusomewa katika Swaalah ya Janaazah au wakati wowote:

 

Maiti mwanamume

 

اللهُـمِّ اغْفِـرْ لَهُ وَارْحَمْـه، وَعافِهِ وَاعْفُ عَنْـه، وَأَكْـرِمْ نُزُلَـه، وَوَسِّـعْ مُدْخَـلَه، وَاغْسِلْـهُ بِالْمـاءِ وَالثَّـلْجِ وَالْبَـرَدْ، وَنَقِّـهِ مِنَ الْخطـايا كَما يُنَقََّ الـثَّوْبُ الأَبْيَـضُ مِنَ الدَّنَـسْ، وَأَبْـدِلْهُ داراً خَـيْراً مِنْ دارِه، وَأَهْلاً خَـيْراً مِنْ أَهْلِـه، وَزَوْجَـاً خَـيْراً مِنْ زَوْجِه،  وَأَدْخِـلْهُ الْجَـنَّة، وَأَعِـذْهُ مِنْ عَذابِ القَـبْر وَعَذابِ النّـار

Allaahumma-Ghfir lahu Warhamhu, wa'aafihi wa’afu 'anhu, wakrim nuzulahu, wawassi' mudkhalahu, waghsilhu bil-maai wath-thalji wal-barad, wanaqqihi minal khatwaayaa kamaa yunaqqa-th-thawbul abyadhw minad-danas, waabdilhu daaran khayran min daarihi, wa ahlan khayran min ahlihi, wazawjan khayran min zawjihi, waadkhilhul jannah, waa’idh-hu min ‘adhaabil qabri, wa ‘adhaabin-naar  

 

Maana yake:

 

“Ee Allaah, Msamehe na Umrehemu na Umuafu na Msamehe na Mtukuze kushuka kwake (kaburini) na Upanue kuingia kwake, na Muoshe na maji na kwa theluji na barafu na Mtakase na makosa kama inavyotakaswa nguo nyeupe kutokana na uchafu, na Mbadilishie nyumba bora kuliko nyumba  yake na jamaa bora kuliko jamaa zake, na mke bora kuliko mke wake, na Muingize Peponi na Mkinge na adhabu ya kaburi (na adhabu ya moto)

 

Maiti mwanamke

 

 

اللهُـمِّ اغْفِـرْ لَهُا وَارْحَمْـها، وَعافِهاِ وَاعْفُ عَنْـها، وَأَكْـرِمْ نُزُلَـها، وَوَسِّـعْ مُدْخَـلَها، وَاغْسِلْـهُا بِالْمـاءِ وَالثَّـلْجِ وَالْبَـرَدْ، وَنَقِّـهِا مِنَ الْخطـايا كَما يُنَقََّ الـثَّوْبُ الأَبْيَـضُ مِنَ الدَّنَـسْ، وَأَبْـدِلْهُا داراً خَـيْراً مِنْ دارِها، وَأَهْلاً خَـيْراً مِنْ أَهْلِـها، وَزَوْجَـاً خَـيْراً مِنْ زَوْجِها،  وَأَدْخِـلْهُا الْجَـنَّة، وَأَعِـذْهُا مِنْ عَذابِ القَـبْر وَعَذابِ النّـار

Allaahumma-Ghfir lahaa Warhamhaa, wa'aafihaa wa’fu 'anhaa, wakrim nuzulahaa, wawassi' mudkhalahaa, waghsilhaa bil-maai wath-thalji wal-barad, wanaqqiha minal khatwaayaa kamaa yunaqqa-th-thawbul abyadhw minad-danas, waabdilhaa daaran khayran min daarihaa, wa ahlan khayran min ahlihaa, wazawjan khayran min zawjihaa, waadkhilhal jannah, waa’idh-ha min ‘adhaabil qabri, wa ‘adhaabin-naar

 

Maiti zaidi ya mmoja

 

اللهُـمِّ اغْفِـرْ لَهُم وَارْحَمْـهم، وَعافِهِم وَاعْفُ عَنْـهم، وَأَكْـرِمْ نُزُلَـهم، وَوَسِّـعْ مُدْخَـلَهم، وَاغْسِلْـهُم بِالْمـاءِ وَالثَّـلْجِ وَالْبَـرَدْ، وَنَقِّـهِم مِنَ الْخطـايا كَما يُنَقََّ الـثَّوْبُ الأَبْيَـضُ مِنَ الدَّنَـسْ، وَأَبْـدِلْهُم داراً خَـيْراً مِنْ دارِهم، وَأَهْلاً خَـيْراً مِنْ أَهْلِـهم، وأََزَوْاجَـاً خَـيْراً مِنْ اَزْوَاجِهِم  وَأَدْخِـلْهُم الْجَـنَّة، وَأَعِـذْهُم مِنْ عَذابِ القَـبْر وَعَذابِ النّـار

Allaahumma-Ghfir lahum Warhamhum, wa'aafihim wa’fu 'anhum, wakrim nuzulahum, wawassi' mudkhalahum, waghsilhum bil-maai wath-thalji wal-barad, wanaqqihim minal khatwaayaa kamaa yunaqqa-th-thawbul abyadhw minad-danas, waabdilhum daaran khayran min daarihim, wa ahlan khayran min ahlihim, waazwaajan khayran min azwaajihim, waadkhilhumul-Jannah, waa’idh-hum min ‘adhaabil qabri, wa ‘adhaabin-naar

 

 

Ama kuhusu mwanamke kuzuru makaburi ingawa ni jambo ambalo halikutazwa katika dini yetu, ila inapendekezeka kuejiepusha nalo kutokana na sababu kadha ambazo zina hikma ndani yake ya kujiepusha kuzuru.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share