Mahindi Ya Nazi

Mahindi Ya Nazi

Vipimo:

Mahindi - 7 Mashuke

Tuwi la nazi zito - 1 Kikombe

Kitunguu - 1

Nyanya - 1

Chumvi - kiasi

Mafuta - 2 vijiko vya supu

Namna Ya Kutayarish na Kupika

  1. Katakata kitunguu na nyanya vipande vidogo vidogo.
  2. Weka mafuta katika sufuria, yakipata moto tia vitunguu, kaanga kidogo tu viwe laini.
  3. Tia nyanya na endelea kukaanga kidogo.
  4. Mimina katika mashine ya kusagia (blender) utie tuwi la nazi na usage.
  5. Rudisha katika sufuria, tia chumvi na mahindi.
  6. Funika upike moto mdogo mdogo huku unageuza mahindi yaive kwa tuwi.

 

 

 

Share