Kababu Za Nyama Za Kukaanga

Kababu Za Nyama Za Kukaanga

Vipimo

Nyama ya kusaga - 1 kilo

Kitunguu saumu(thomu) na tangawizi iliyosagwa - 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 kijiko cha chai

*Bizari ya Kababu (chaplin Kabab masala) - ½ paketi

Kotmiri (coriander leaves) - ½ kikombe

Chumvi - kiasi

Mafuta - kiasi ya kukaangia

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Changanya nyama pamoja na viungo vyote katika bakuli.
  2. Fanya madonge shape ya duara kama picha weka kando.
  3. Kisha kanga kama sambusa mpaka iwe ziabadilike rangi.
  4. Epua zikiwa tayari kwa kuliwa.

Kidokezo:

*Bizari unaweza kutumia zozote upendazo ila hiyo ya ‘Chaplin’ inayouzwa tayari katika paketi inaleta ladha nzuri katika kababu aina hii.

 

 

Share