Bajia Za Kunde

Bajia Za Kunde

Vipimo

Kunde  za kupaaza - 1 ½  Vikombe

Vitungu vya kijani iliyokatwa katwa - ½  Kikombe

Baking soda - ¼  Kijiko cha chai

*Bizari mchanganyiko - 1  Kijiko cha chai

Maziwa - 2 Vijiko vya supu

Chumvi - 1 ¼ Vijiko vya chai

Unga wa ngano - 2 Vijiko vya supu

Mafuta ya kukaangia

* Unaweza kutumia bizari ya pilau (cummin) ukipenda

Namna ya kutayarisha na kupika

  1. Osha na kuroweka kunde kwenye bakuli la maji ya baridi usiku mpaka asubuhi.
  2. Saga kwenye mashine (food processor)  kisha mimina kwenye bakuli.
  3. Ongeza vitungu, baking soda, masala, maziwa, na chumvi.
  4. Koroga vizuri halafu tia unga kisha uchanganye pamoja.
  5. Fanya vidonge kama nchi moja kisha ukipenda bana katikati ya mikono na kidole katikati ya bajia.
  6. Kaanga kwenye mafuta ya moto mpaka ziive.
  7. Andaa bajia kwenye sahani na chatini uipendayo.

 

 

Share