Keki Ya Mchanganyiko Wa Matunda Kavu

Keki Ya Mchanganyiko Wa Matunda Kavu

Vipimo  

Unga - 2 Vikombe 

Mayai - 6 

Siagi - 200g 

Sukari - 1 Kikombe 

Vanilla - ½ Kijiko 

Arki rose ukipenda - 2 matone 

Baking powder - 2 Vijiko vya chai 

Mchanganyiko wa matunda kavu-  ¾ Kikombe 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Washa oveni 350°c.
  2. Saga siagi na sukari kwa mashine mpaka mchanganyiko ulainike.
  3. Ongeza yai moja baada ya moja na huku ukiendelea kusaga mpaka yaishe.
  4. Tia unga uliochanganwa na baking powder.
  5. Endelea kuchanganya mpaka ichanganyike vizuri, halafu arki rose, vanilla na mchnganyiko wa matunda kavu halafu koroga kidogo ilizichanganyike vizuri.
  6. Mimina mchanganyiko katika chombo cha kuchomea.
  7. Vumbika (bake) kwa muda wa dakika 20 mpaka 25.
  8. Ikisha poa kata kata vipande na tayari kuliwa kwa kahawa au chai.
Share