Keki Ya Stroberi Ya Vipande Vya Mraba

 

Keki Ya Stroberi Ya Vipande Vya Mraba

Vipimo:

Unga -  2 Vikombe vya chai

Sukari -  ½ kikombe

Siagi (butter) - 2/3 kikombe 

Kijazio (Filling)

Malai ya jibini (Cream Cheese )  - 1LB

Sukari  -  ¾ kikombe

Mayai - 2

Ndimu -  1 kijiko cha chai

Jamu ya stroberi (Strawberry jam) - 1 kikombe  

Stroberi (fresh) zilizokatwa ndogo ndogo - 1 kikombe                                                         

 Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Gamba (Crust)  - Au tumia ya tayari.

  1. Washa oven moto wa 350°F (180°C)
  2. Paka mafuta treya ya keki saizi ya 13” x9” (33 cm x 23 cm)
  3. Changanya unga na sukari katika bakuli la kiasi.
  4. Katakata siagi na uchanganye hadi ichanganyike iwe ya chengachenga (crumbs)
  5. Itie katika treya na ungandamize vizuri ienee kote katika treya.  
  6. Tia katika oveni ipikike kwa muda wa dakika 15-20 au hadi igeuke rangi ya hudhurungi isiyokoza.
  7. Itoe iache ipowe huku unatengeneza kijazio.  

Kijazio (Filling)     

1.       Changanya malai ya jibini na sukari katika mashine ya keki (Cake mixer) hadi iwe laini. 

2.       Tia mayai na ndimu ukiendelea kuipiga katika mashine. 

3.       Pakaza jamu juu ya gamba (curst) na mwagia stroberi ulizokatakata juu yake.  

4.       Mwagia mchanganyiko wa malai ya jibini (cream cheese mixture) juu ya stroberi. 

5.       Pika (bake) kwa muda wa dakika 25-30 au zaidi hadi itue yote igande.  

6.       Itoe ipoe katika rafu ya kupozea (cooling rack). 

7.       Kata vipande vipande weka katika sahani zikiwa tayari kuliwa.  

 

Share