Inafaa Kumuadhinia Maiti Anapozikwa?
SWALI:
Wakati wa kuzika maiti watu wengine wanawa adhiniya maiti inafaa.
JIBU
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Haifai Muislamu kuadhiniwa kaburini au nje yake anapoaga dunia. Haikupatikana kabisa dalili ya kufanya hivyo katika mafunzo ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Maelezo zaidi kuhusu anayopaswa kufanyiwa maiti, ingia katika viungo vifuatavyo:
Dalili Za Kheri Katika Mambo Yamfaayo Maiti
Na Allah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


