Keki Ya Kastadi Na Kakao

 Keki Ya Kastadi Na Kakao 

 

Vipimo  

Unga -  850 gm 

Siagi - 450 gm 

Sukari - 425 gm 

Mayai - 10  

Unga wa Kastadi (custard powder) - 1 Kijiko cha supu  

Unga wa kakao (cocoa powder ) - 1 kijiko cha  supu 

Baking powder - 1 kijiko cha supu

Vanilla - 1 kijiko cha supu  

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

  1. Saga siagi na sukari katika mashine ya keki dakika 10  hadi ichanganyike, na iwe laini kama malai [creamy]  
  2. Tia mayai, changanya kwa mashine speed ndogo kwa  dakika 5  
  3. Tia unga huku unachanganya kidogo, na tia Baking Powder  
  4. Tia unga wa kastadi, vanilla au arki na changanya tena vizuri.  
  5. Chota mchanganyiko kidogo weka katika kibakuli kidogo kisha changanya na kakao vizuri. Weka kando.  
  6.  Paka siagia na nyunyiza unga kidogo katika treya utakayopikia keki
  7.  Tia nusu ya mchanganyiko wa keki katika treya ya 33cm x 22cm  (13" x 9"), kisha tia mchaganyiko wa kakao na utandaze kote juu. 
  8. Malizia kutia mchanganyiko uliobakia na uoke [bake] katika oveni kwa muda wa takriban dakika 40 hadi keki iwive.  
  9. Epua, iache ipoe kisha katakata vipande kiasi upendavyo, ikiwa tayari. 

Kidokezo: 

Ikitumia kipimo nusu, na treya tumia ndogo yake.

 

 

 

 

Share