Keki Ya Machungwa

Vipimo
Siagi iliyolainika ½ Kikombe cha chai
Sukari 1 Kikombe cha chai
Mayai 2
Maganda ya chungwa iliyokwaruzwa 1 Kijiko cha supu
Ariki ya lozi (almond essence) ¼ Kijiko cha chai
Unga 2 Vikombe vya chai
Baking powder 2 Vijiko cha chai
Chumvi ½ Kijiko cha chai
Iliki ya unga ½ Kijiko cha chai
Maziwa ½ Kikombe cha chai
Juisi ya machungwa ¼ Kikombe cha chai
Lozi ziliyokaangwa na kupondwa ¾ Kikombe cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Washa oveni moto wa 350ºF.
2. Paka siagi chombo utakachochomea (ikiwa unatumia loaf pan ndogo, utahitaji 3)
3. Katika bakuli la mashine, saga sukari na siagi hadi ilainike.
4. Kisha tia yai moja moja, halafu ganda la chungwa na ariki ya lozi.
5. Katika bakuli jengine, changanya pamoja unga, baking powder, chumvi na iliki.
6. Kisha changanya kwenye ule mchanganyiko wa siagi, halafu tia maziwa na juisi ya machungwa, na lozi.
7. Vumbika kwenye oveni kwa muda wa dakika 35.
8. Iache ipowe kabisa na itakuwa tayari kuliwa.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha



assalamu alaykum ningeomba
assalamu alaykum ningeomba munifahamishe keki ya brown inshaallah