Katlesi Za Samaki Wa Tuna Shepu Ya Yai

Katlesi Za Samaki Wa Tuna Shepu Ya Yai

Vipimo

 

Viazi - 5 vikubwa au 7

Samaki wa tuna - 2 vikopo

Pilipili kijani ya kusaga -2   

Bizari mchanganyiko au ya mchuzi – 2 vijiko vya chai

Ndimu – 1 kamua

Kotmiri – katakata kiasi

Chumvi - kiasi

 

 

Mayai – 2

Unga wa toast - kiasi

Mafuta ya kukaangia

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

  1. Menya viazi, chemsha viive kiasi sio laini sana
  2. Epua chuja maji, tia katika bakuli, pondaponda  
  3. Chambua samaki wa tuna kando, kisha mimina katika bakuli.
  4. Tia bizari, pilipili, ndimu, kotimiri.
  5. Changanya vizuri, kisha tengeneza vidonge kiasi unachotaka na kata umbo kama la yai. Panga katika treya.
  6. Weka mafuta katika karai yashike moto kiasi.
  7. Weka unga wa toast katika kibakuli
  8. Piga yai katika kibakuli
  9. Chomva kidonge cha kiazi katika toast kisha katika yai kisha tumbukiza katika karai upike yageuke rangi ya hudhurungi.
  10. Epua chuja mafuta katlesi zikiwa tayari

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kuburudika)

 

 

 

 

 

Share