Vikeki Vya Icing Za Rangi

 

 

 

Vipimo

 

 

 

Unga                                              1 ½ Vikombe

 

Baking powder                                1 Kijiko cha chai

 

Chumvi                                           ½ Kijiko cha chai

 

Siagi isiyo na chumvi                        ½ Kikombe

 

Sukari                                              1 Kikombe

 

Mayai                                               3

 

Vanilla                                              1½ Vijiko vya chai

 

Maziwa                                             ¾ Kikombe

 

 

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

 

 

  1. Washa oveni moto wa 350°. Kisha weka karatasi za kupikia keki za vikombe kwenye treya.

  2. Katika bakuli la kiasi, chunga pamoja unga, baking powder na chumvi na iache kando.

  3. Katika bakuli la mashine changanya siagi na sukari hadi ilainike.

  4. Halafu tia yai moja baada la jengine huku unaendelea kuchanganya, kisha tia vanilla.

  5. Kisha tia mchanganyiko wa unga uliyoweka kando nusu yake huku unaendelea kuchanganya, kisha tia maziwa na umalizie na unga uliyobakia.

  6. kisha mimina kwenye treya/karatasi za kuchomea keki za vikombe lakini usijaze mpaka juu.

  7. Weka katika oveni kwa muda wa dakika 20.

  8. Ziache zipoe kisha zipake icing/cream upendayo na zitakuwa tayari kuliwa.

 

Kidokezo

 

Kipimo hichi ni ya vikeki darzeni moja.

 

Share