Keki Ya Stroberi Na Njugu Za Pistachio

Keki Ya  Stroberi Na Njugu Za Pistachio

 

 

Vipimo

 

Unga mweupe vikombe 2 ½

Siagi kikombe 1 iliyoyayuka

Mayai 6

Sukari kikombe 1

Baking powder vijiko 2 vya chai

Maziwa mazito au mtindi  ½ kikombe

Arki Ya Stroberry 1 kijiko cha chai (Strawberry flavour)

Rangi nyekundu ¼ kijiko cha chai

Njugu za pistachio katakata ½ kikombe

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Washa oven lishike moto wa kiasi cha kupikia keki kama 300 Deg F
  2. Saga sukari na siagi katika mashine ya kupigia keki.
  3. Tia mayai huku unaendelea kuchanganya, tia arki ya stroberi (Stawberry flavour) na rangi,  tia na njugu changanya vizuri.
  4. Changanya unga baking powder kisha mimina kidogo kidogo umimine katika treya ya keki uliyopakaza siagi.

  1. Weka katika oven pika (Bake) kiasi nusu saa mpaka iwive.
  2. Epua ipoe katakata ikiwa tayari.

 

 

 Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)  

 

 

Share