Waliomiliki Mikono Yao Ya Kiume Ina Maana Inafaa Kufanya Mapenzi Na Wafanya Kazi Wa Nyumbani?

SWALI:

 

 

ASSALAAMU ALAYKUM WARAHMATULLAHI WABARAKATUH.

 

Sifa njema zote in za Allaah. Namshukuru Allah Subhannah Wataallah kuniongoza kujiunga na uanachama na AL HIDAAYA. Nimekuwa napata makala zenu kupitia kwa wenzangu kwa muda mrefu na nimefaidika sana kielimu katika dini yetu tukufu ya Kiislamu. Allaah Subhannah Wataallah awajaze kila la kheri wahusika wote wanaojitahidi kuelemisha jamii ya kiislam kupitia mtandao huu.

 

Katika Suratul Muuminun Aya ya 5 na 6 inayosema ‘…na ambao tupu zao wanazilinda’ ‘Isipokuwa kwa wake zao au kwa wale (wanawake) iliyowamiliki mikono yao ya kuume. Basi hao ndio wasiolaumiwa. Na anayetaka kinyume cha haya basi hao ndio warukao mipaka (ya Mwenyezi Mungu)’…Je hii ina maana ya kuwa wanaume wanaruhusiwa kufanya mapenzi na hao wanawake ‘iliyomiliki mikono yao ya kuume’??. Nitashukuru kupata ufafanuzi wa aya hizi na mfano wa hao wanaomilikiwa na mikono yao ya kuume.


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu wanaomilkiwa na mikono yetu ya kuume. Hakika ni kuwa Aayah hizi ambazo umezitaja zinatupatia sifa za Waumini wa kihakika.

 

Ama inayomiliki mikono ya kuume ni wale watumwa wa kike walioshikwa na Waislamu katika vita vya Jihaad. Kuna fadhila ya kuwaacha huru wanawake hawa na thawabu ya kufanya hilo ni nyingi mbele ya Allaah Aliyetukuka. Na ikiwa utamuoa basi itakuwa ni kheri kama ilivyo katika Suratun Nisaa', Aayah ya 3. Na hasa Uislamu umeweka mikakati mizuri ya kuweza kuwakomboa watumwa, kulipa fidia au wao wenyewe kujikomboa kwa mapatano baina yenu. Kwa hiyo, hapa Allaah Aliyetukuka Ametoa ruhusa kwa njia mbili ya kuweza kujitosheleza kwa wanawake, kwa kufanya mapenzi na mkeo wa halali na kufanya hilo na watumwa walio chini. Kufanya moja katika ya hayo mawili ni kutolewa lawamani kabisa.

 

Lakini tufahamu kuwa hawa watumishi wa nyumbani sio hao ‘iliyowamiliki mikono yao ya kuume’. Zaidi unaweza kusoma hapa:

 

House Girl Sio Wale Waliomiliki Mikono Yetu Ya Kuume

 

Kampa Dada Yake Kama Zawadi Aishi Naye Kinyumba Nini Hukmu Yake?

 

Na Allaah Anajua Zaidi

 

 

 

Share