Keki Ya Jibini Ya Rasiberi (Raspberry)

Keki Ya Jibini Ya Rasiberi (Raspberry)    

Vipimo

Ukoko wa tayari (ready crust) -  1 ½

Rasberi ya kopo -  1 

Sukari -  ¼ Kikombe cha chai

Siagi -  ¼ Kikombe cha chai

FILLING

Malai ya jibini (cream cheese)  -  1½ Pakiti za 450g

Mayai -  4 makubwa

Sukari - 1½ kikombe cha chai

Ndimu -  kiasi

Chumvi -  kiasi 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Washa oveni moto wa 350°F.
  1. Changanya Ukoko wa tayari (ready crust), sukari na siagi mpaka ushikane tandaza kwenye treya ya mviringo maalum ya kufungua pembeni choma kwa muda wa dakika 15-20 hivi. Katika bakuli la mashine, changanya vizuri malai ya jibini na sukari.
  1. Katika bakuli la mashine, changanya vizuri malai ya jibini na sukari kisha tia yai  moja moja na uendele kuchanganya.
  1. Mwisho mimina ndimu na chumvi.
  1. Mchanganyiko ukiwa tiyari mimina juu ya ile crust uliyochoma kasha itie tena kwenye oven kwa muda wa dakika 20-30 Ikishaiva iache ipoe na huku tayarisha sosi yake.
  1. Katika sufuria, tia juisi ya rasiberi utakayoitoa kwenye kopo pamoja na uweke moto mdogo huku unakoroga mpaka iwe nzito kiasi.
  1. Kisha mimina juu ya ile jibini iliyopoa na upange  rasiberi juu yake yake  kwa mpango mzuri.
  1. Iweke kwenye firiji ipate ubaridi kwa muda wa saa moja na kisha itakuwa tayari kwa kuliwa - kata vipande upendavyo.

 

Share