Kumshawishi Mke Kupunguza Kiasi cha Mahari Atakacho Kudai

SWALI:

 

ASSALAM ALAYKUM, INAFAA KUMSHAWISHI MTU UNAETAKA KUMUOA KIASI CHA MAHARI ATAKACHOKUDAI?

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kumshawishi mke kuhusiana na kiwango cha mahari atakachodai. Hakuna tatizo kuweza kumshawishi mwanamke utakayemuoa kuhusiana na mahari ambayo utampa lakini bila kumdhulumu kabisa kuhusiana na haki yake hiyo. Na katika kumshawishi haifai kwenu nyinyi wawili kukaa faragha na kuzungumza suala hilo.

 

Mahari ni haki ya mke aliyopatiwa na Uislamu ya kuitisha chochote anachotaka kwa kutizama pia uwezo wa mume mtarajiwa. Kwa minajili hiyo, ikiwa mke ameitisha mahari mengi, mume anaweza kumshawishi ili apunguze kwa kiwango ambacho ataweza kumudu bila ya shida yoyote ile.

 

Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

 

Siwezi Kulipa Mahari Niliyotakiwa Nitoe Nifanyeje?

 

Kiwango Gani Cha Mahari Atoe Mume Asiyejiweza?

 

 

Mke Kumsamehe Mume Mahari

 

2. Mahari –

 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi.

 

 

Share