Umri Gani Mtoto Anahesabiwa Madhambi Yake? Mtoto Anayefariki Umri Wa Chini Ya Kubaleghe Asomewe Du’aa Ya Kuombewa Maghfira?

SWALI:

 

Nilipata kuambiwa kuwa mtoto kama hajafikia baleghe huwa hahisabiwi dhambi je ni kweli? Na kama ni kweli mtoto mdogo akifa anapaswa kuombewa kwa mwenyezi MUNGU dua ya "allahu maghfir lahu wa arhamhu wamaskana fijanna?"


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu umri ambao mtoto anaanza kuhesabiwa dhambi zake. Hakika ni kweli mtoto mwanzo anapozaliwa anakuwa yuko katika Uislamu. Mtoto kama huyo huwa haandikiwi dhambi mpaka wakati atakapo baleghe. Kwa mwanamme, ni kutokwa na manii na ilhali kwa msichana ni kutokwa na damu ya kila mwezi (ada yake).

 

Du’aa ya mtoto mdogo ni tofauti na du’aa anayoombewa mtu mzima aliye baleghe katika kumswalia Swalaah ya jeneza. Miongoni mwa du’aa ni:

 

 

أللَّهُمَّ أَعِذْهُ مِنْ عَذابِ الْقَبْرِ

“Ee Allaah mlinde na adhabu ya kaburi”

 

Alikuwa Al-Hassan رضي الله عنه anamsomea mtoto mdogo Suratul Faatihah kisha anasema :

اللهُـمِّ اجْعَلْـهُ لَنا فَرَطـاً، وَسَلَـفاً وَأَجْـراً

“Ee Allaah mfanye kwetu sisi ni kitangulizi  cha malipo na dhamana na  malipo” (al-Baghawiy).

 

 

 

 

Na katika du’aa nyingine ni kuwaombea wazazi wake wawe ni wenye kupata malipo kwa ajili ya kuaga dunia kwake:

 

اللهُـمِّ اجْعَلْـهُ فَرَطـاً وَذُخْـراً لِوالِـدَيهِ، وَشَفـيعاً مُجَـاباً، اللهُـمِّ ثَـقِّلْ بِهِ مَوازيـنَهُما، وَأَعْـظِمْ بِهِ أُجُـورَهُـما، وَأَلْـحِقْـهُ بِِصَالِـحِ الـمؤْمِنـين، وَاجْعَلْـهُ في كَِفـَالَةِ إِبْـراهـيم، وَقِهِ بِرَحْمَـتِكَ عَذابَ الْجَـحِيمِ , وَأَبْـدِلْهُ داراً خَـيْراً مِنْ دارِه ، وَأَهْلاً خَـيْراً مِنْ أَهْلِـه, اللَّهُمَّ اغْفِرْ لإِسْلافِنَا , وَأَفْراطِنَا , وَمَنْ سَبَقَنَاَ بِالإِيمَان

“Ee Allaah, mjaaliye kuwa nikitangulizi na akiba kwa wazazi wake na nikiombezi chenye  kukubaliwa du’aa yake.  Ee Allaah  kwa ajili yake zifanye nzito mizani za wazazi wake na yafanye mengi malipo yao, na mkutanishe na wema wa Waumini na mjaaliye awekatika dhamana ya Ibraahiym na umuepushe kwa Rehema yako na adhabu ya moto, na mbadlishie nyumba bora kuliko nyumba yake, na jamaa bora kulko jamaa zake.  Ee Allaah   wasamehe waliotangulia na waliopita na waliotutangulia katika Uislamu”

 

 

 

Ukitizama du’aa hizi utaona bado mtoto anaombewa aepushwe na Moto wa Jahannam kwani muamuzi wa Mwisho ni Allaah Aliyetukuka.

 

 

Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

 

Watoto Wanaofariki Umri Mdogo Nini Hatima Yao?

 

Ishara Za Mtoto Wa Kiume Kubaleghe Na Nini Jukumu La Mzazi Kwa Hali Hiyo Ya Mwanae?

 

 

Na Allaah Anajua zaidi.

 

 

Share