Ikifika Wakati Wa Magharibi Anaona Dhiki – Asome Du’aa Gani Kuondosha Dhiki?

SWALI:

 

 

 

Asalam aleikum natumai hapo mulipo nyote hamuna neno.mimi nina swali huwanasikiya dhiki sana  wakati wa magharib  ,hata sijui nini kwanini najaribu kumlani shetwani .sasa naomba munisaidiye na dua ipi ambayo nitaisoma iniodoshe hiyo dhiki na wasi wasi.naomba usaidizi wenu

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Tunasikitika kufikwa na hali hiyo, na yakufanya ili kuepukana na hali hiyo ni yafuatayo:

 

  1. Kusoma Qur-aan kwa wingi

  2. Kumdhukuru Allaah Subhaana wa Ta’ala kila mara

  3. Kusikiliza mawaidha

  4. Kudumisha kusoma nyiradi za Asubuhi na jioni kwa mfululizo kwani zinafaika kubwa ya kuondosha kila dhiki, shari na balaa na kumbakisha Muislamu katika usalama, amani na furaha. Hizi zinapatikana katika kitabu kifuatacho ambacho kina kila aina ya Du’aa:

 

 

Hiswnul Muslim

 

Zifuatazo Du’aa hasa :

 

28 Nyiradi Za Asubuhi Na Jioni

 

35 Dua'a Ukiwa Na Hamu Na Huzuni

 

 

 

Sikiliza mawaidha ya Ruqya:

 

Ruqya

 

 

 

Tafadhali bonyeza pia kiungo kifuaacho upate manuafa zaidi:

 

Nina Dhiki Na Nina Woga Sana Nifanyeje?

 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share