Chops/Katlesi Za Muhogo Na Mayai

Chops/Katlesi Za Muhogo Na Mayai 

Vipimo

Muhogo - 1 Lb (pound)

Mayai yalochemshwa6 - 

Pilipili mbichi ilosagwa - 1 kijiko cha supu

Jira/cummin bizari pilau - 1 kijiko cha chai

Vitungu vya kijani (spring onions) - 3 mich

Siagi - 1 oz

Unga wa dengu (gram flour) - 1 ½  kikombe takriba

Ndimu - 1 kamua

Chumvi - kiasi

Mafuta ya kukaangia

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:

  1. Chemsha mhogo kisha upondeponde (mash)
  2. Katakata vitunguu vya kijani (chopped)
  3. Changanya na vitu vyote pamoja isipokuwa mayai.
  4. Fanya maduara na utumbukize yai, funga duara kufunika yai.
  5. Tia maji kidogo katika unga wa dengu, koroga, kisha chovya humo na ukaange chops kama unavyokaanga kachori.
  6. Epua weka katika sahani, kisha kata katikati na tolea kwa sosi yoyote upendayo

Kidokezo:

Ukikosa unga wa dengu, tumia unga mweupa, na tia bizari ya manjano kidogo.

 

 

 

 

Share