075-Asbaabun Nuzuwl: Al-Qiyaamah Aayah 16-19: لَا تُحَرِّكْ بِهِ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

075-Al-Qiyaamah:

 

لَا تُحَرِّكْ بِهِ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِ﴿١٦﴾

16. Usiutikisie (huu Wahy) ulimi wako ili kuiharakiza (Qur-aan ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).

 

إِنَّ عَلَيْنَا جَمْعَهُ وَقُرْآنَهُ﴿١٧﴾

17. Hakika ni juu Yetu kuikusanya na kukuwezesha kuisoma kwake.

 

فَإِذَا قَرَأْنَاهُ فَاتَّبِعْ قُرْآنَهُ﴿١٨﴾

18. Basi Tunapoisoma (kupitia Jibriyl), fuata kusomwa kwake.

 

ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا بَيَانَهُ﴿١٩﴾

19. Kisha ni juu Yetu kuibainisha (kwako).

 

 

حَدَّثَنَا قُتَيْبَةُ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، عَنْ مُوسَى بْنِ أَبِي عَائِشَةَ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، فِي قَوْلِهِ: ((لاَ تُحَرِّكْ بِهِ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِ‏)) قَالَ كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((إِذَا نَزَلَ جِبْرِيلُ بِالْوَحْىِ، وَكَانَ مِمَّا يُحَرِّكُ بِهِ لِسَانَهُ وَشَفَتَيْهِ فَيَشْتَدُّ عَلَيْهِ وَكَانَ يُعْرَفُ مِنْهُ، فَأَنْزَلَ اللَّهُ الآيَةَ الَّتِي فِي: ((‏لاَ أُقْسِمُ بِيَوْمِ الْقِيَامَةِ))  ...((‏لاَ تُحَرِّكْ بِهِ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِ * إِنَّ عَلَيْنَا جَمْعَهُ وَقُرْآنَهُ‏))‏ قَالَ عَلَيْنَا أَنْ نَجْمَعَهُ فِي صَدْرِكَ، وَقُرْآنَهُ ‏‏((فَإِذَا قَرَأْنَاهُ فَاتَّبِعْ قُرْآنَهُ‏))‏ فَإِذَا أَنْزَلْنَاهُ فَاسْتَمِعْ ‏((‏ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا بَيَانَهُ‏))‏ عَلَيْنَا أَنْ نُبَيِّنَهُ بِلِسَانِكَ ـ قَالَ ـ فَكَانَ إِذَا أَتَاهُ جِبْرِيلُ أَطْرَقَ، فَإِذَا ذَهَبَ قَرَأَهُ كَمَا وَعَدَهُ اللَّهُ‏.‏

 

Qutaybah bin Sa’iyd ametuhadithia: Ametuhadithia Jariyr, kutoka kwa Muwsaa bin Abiy ‘Aaishah kutoka kwa Sa’iyd bin Jubayr kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) , kuhusu kauli yake Allaah (سبحانه وتعالى):

لَا تُحَرِّكْ بِهِ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِ﴿١٦﴾

 

Usiutikisie (huu Wahy) ulimi wako ili kuiharakiza (Qur-aan ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).

 

Amesema, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  alikuwa pindi anaposhuka Jibriyl na Wahyi, alikuwa akitikisa ulimi wake haraka haraka pamoja na midomo yake (kufanya haraka kusoma) na hali hiyo ilikuwa ngumu kwake, na ilikuwa inafahamika kuwa ni kuteremshwa kwa Wahyi. Basi Allaah Akateremsha katika Suwratul-Qiyaamah inayoanza na:

 

لَا أُقْسِمُ بِيَوْمِ الْقِيَامَةِ﴿١﴾

1. Naapa kwa siku ya Qiyaamah.

 

Akateremsha:

 

لَا تُحَرِّكْ بِهِ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِ﴿١٦﴾

16.Usiutikisie (huu Wahy) ulimi wako ili kuiharakiza (Qur-aan ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).

 

إِنَّ عَلَيْنَا جَمْعَهُ وَقُرْآنَهُ﴿١٧﴾

17. Hakika ni juu Yetu kuikusanya na kukuwezesha kuisoma kwake.

 

Akasema: Ni juu Yetu kuikusanya katika kifua chako na kukusomea hiyo Qur-aan hivyo basi,

 

فَإِذَا قَرَأْنَاهُ فَاتَّبِعْ قُرْآنَهُ﴿١٨﴾

18. Basi Tunapoisoma (kupitia Jibriyl), fuata kusomwa kwake.

 

Basi pindi tutakaposoma wewe fuatiliza kisomo chetu, na usikilize kwa makini, na pindi tutakapoteremsha sikiliza vizuri.

 

ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا بَيَانَهُ﴿١٩﴾

19. Kisha ni juu Yetu kuibainisha (kwako).

 

Ni juu yetu kukubainishia katika ulimi wako. Amesema: Ikawa kila Jibriy akifika hugonga na akiondoka husoma kama vile ambavyo Allaah Amemuahidi.

[Al-Bukhaariy Kitaab Al-Wahyi na pia usimulizi kama huo katika Kitaab Fadhwaail Al-Qur-aan, Baab At-Tartiyl fiy Al-Qiraa-ah]

 

Pia,

 

 حَدَّثَنَا الْحُمَيْدِيُّ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، حَدَّثَنَا مُوسَى بْنُ أَبِي عَائِشَةَ ـ وَكَانَ ثِقَةً ـ عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ ـ رضى الله عنهما ـ قَالَ : كَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم إِذَا نَزَلَ عَلَيْهِ الْوَحْىُ حَرَّكَ بِهِ لِسَانَهُ ـ وَوَصَفَ سُفْيَانُ ـ يُرِيدُ أَنْ يَحْفَظَهُ فَأَنْزَلَ اللَّهُ: ((لاَ تُحَرِّكْ بِهِ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِ‏))‏

 

Al-Humaydiyy ametuhadithia, ametuhadithia Sufyaan na Muwsaa bin Abiy ‘Aiashah, na alikuwa ni mtu thiqqah. Kutoka kwa Sa’iyd bin Jubayr kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema:  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)   alikuwa inaposhuka Wahyi alikuwa akiharakisha ulimi wake. Sufyaan akatoa wasifu kuwa alitaka kuhifadhi Allaah Akateremsha:

 

16. Usiutikisie (huu Wahy) ulimi wako ili kuiharakiza (Qur-aan ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).

[Al-Bukhaariy, Kitaab At-Tafsiyr]

 

Pia katika Al-Bukhaariy (1/32) kuhusu kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

لَا تُحَرِّكْ بِهِ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِ﴿١٦﴾

16. Usiutikisie (huu Wahy) ulimi wako ili kuiharakiza (Qur-aan ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).

 

Muwsaa bin Ismaa’iyl ametuhadithia amesema Abuu ‘Awaanah ametuhadithia, amesema Muwsaa bin Abiy ‘Aaishah amesema kuwa, Sa’iyd bin Jubayr kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) katika kauli yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 لَا تُحَرِّكْ بِهِ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِ﴿١٦﴾

16. Usiutikisie (huu Wahy) ulimi wako ili kuiharakiza (Qur-aan ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).

 

Amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  alikuwa akipata tabu wakati wa kushuka Wahyi haswa taabu ya kuharakisha mdomo wake. Ibn ‘Abbaas amesema: Na mimi pia ninaizungusha kwenu kama alivyokuwa akiifanya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Na Sa’iyd bin Jubayr naye amesema: Na mimi nilikuwa nikiizungusha kama nilivyomuona Ibn ‘Abbaas alivyokuwa akiizungusha. Allaah Akateremsha:

 

لَا تُحَرِّكْ بِهِ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِ﴿١٦﴾

16. Usiutikisie (huu Wahy) ulimi wako ili kuiharakiza (Qur-aan ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).

 

إِنَّ عَلَيْنَا جَمْعَهُ وَقُرْآنَهُ﴿١٧﴾

17. Hakika ni juu Yetu kuikusanya na kukuwezesha kuisoma kwake.

 

Amesema: Hukusanywa kwenye kifua chake na kusoma. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa baada ya hapo anapojiwa na Jibriyl akimsikiliza na anapoondoka Jibriyl Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akisoma kama alivyosomeshwa na Jibriyl.

 

[Muslim (4/165-166), At-Tirmidhiy (4/209), na akasema Hadiyth hii ni Hasan Swahiyh, An-Nasaaiy (2/115), Ahmad (1/343), Atw-Twayaalisiy (2/25), Ibn Sa’d (1/132), Ibn Jariyr (29/187), Al-Humadiyy (1/242), Ibn Abiy Haatim kama ilivyo kwenye Tafsiyr Ibn Kathiyr (4/449)]

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

أَوْلَىٰ لَكَ فَأَوْلَىٰ﴿٣٤﴾

34. Ole kwako! Tena ole kwako (ewe kafiri)!

 

ثُمَّ أَوْلَىٰ لَكَ فَأَوْلَىٰ﴿٣٥﴾

35. Kisha ole kwako! Tena ole kwako!

 

An-Nasaaiy (227) kama ilivyo katika Tafsiyr Ibn Kathiyr (4/452), Ya’quwb bin Ibraahiym ametuhadithia na Abuu Nu’maan Abuu ‘Awaanah hali kadhalika. Tumempata Abuu Daawuwd na Muhammad bin Sulayman ametuhadithia Abuu 'Awaanah kutoka kwa Muwsaa bin Abiy ‘Aaishah kutoka kwa Sa’iyd bin Jubayr kuwa amesema Nilimwambia Ibn ‘Abbaas:

 

 أَوْلَىٰ لَكَ فَأَوْلَىٰ﴿٣٤﴾

34. Ole kwako! Tena ole kwako (ewe kafiri)!

 

Amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ameisema hiyo kwa Abuu Jahal kisha Allaah Akateremsha.

 

[Hadiyth ina wapokezi (rijaal) wote Swahiyh kwani Ya’quwb bin Ibraahiym kuwa yeye ni Ad-Duwrqiy amepokea kutoka kwake kundi, na Abuu Nu’maan naye ni Muhammad bin Al-Fadhwl ambaye amepewa laqab ya ‘Aarim miongoni mwa watu wa kundi. Abu ‘Awaanah  ni Wadhwaah bin 'Abdillaah Al-Yashkiry miongoni mwa watu wa kundi na katika njia nyingine ni Al-Imaam Abuu Daawuwd Sulayman bin Al-Ash’ath mwenye As-Sunan na Muhammad bin Sulayman ambaye amepewa laqab ya Balwayn miongoni mwa watu wa Abuu Daawuwd, na An-Nasaaiy ni thiqqah, na watu wa Sanad waliobakia wanafahamika (Imepokewa na Ibn Jariyr (29/200) kutoka kwa Shaykh wake Muhammad bin Humayd Ar-Raaziy na ndani yake kuna maneno). 

 

 

Share