076 - Al-Insaan
الإِنْسَان
Al-Insaan: 076
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
هَلْ أَتَىٰ عَلَى الْإِنسَانِ حِينٌ مِّنَ الدَّهْرِ لَمْ يَكُن شَيْئًا مَّذْكُورًا﴿١﴾
1. Kwa hakika kilimpitia binaadamu kipindi fulani katika dahari, hakuwa kitu kinachotajwa.
إِنَّا خَلَقْنَا الْإِنسَانَ مِن نُّطْفَةٍ أَمْشَاجٍ نَّبْتَلِيهِ فَجَعَلْنَاهُ سَمِيعًا بَصِيرًا﴿٢﴾
2. Hakika Sisi Tumemuumba binaadamu kutokana na tone la manii iliyochanganyika ili Tumjaribu, Tukamfanya mwenye kusikia na mwenye kuona.
إِنَّا هَدَيْنَاهُ السَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرًا وَإِمَّا كَفُورًا﴿٣﴾
3. Hakika Sisi Tumemuongoza njia; ima (awe) ni mwenye kushukuru au mwingi wa kukufuru.
إِنَّا أَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ سَلَاسِلَ وَأَغْلَالًا وَسَعِيرًا﴿٤﴾
4. Hakika Sisi Tumewaandalia makafiri minyororo, na pingu na moto uliowashwa vikali mno.
إِنَّ الْأَبْرَارَ يَشْرَبُونَ مِن كَأْسٍ كَانَ مِزَاجُهَا كَافُورًا﴿٥﴾
5. Hakika Waumini watendao wema kwa wingi watakunywa katika vikombe vya mvinyo, mchanganyiko wake ni kaafuwr.
عَيْنًا يَشْرَبُ بِهَا عِبَادُ اللَّـهِ يُفَجِّرُونَهَا تَفْجِيرًا﴿٦﴾
6. Nayo ni chemchemu watakayokunywa toka humo Waja wa Allaah, wataibubujua kwa wingi.
يُوفُونَ بِالنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْمًا كَانَ شَرُّهُ مُسْتَطِيرًا﴿٧﴾
7. Wanatimiza nadhiri na wanaiogopa siku ambayo shari yake ni yenye kuenea kwa upana.
وَيُطْعِمُونَ الطَّعَامَ عَلَىٰ حُبِّهِ مِسْكِينًا وَيَتِيمًا وَأَسِيرًا﴿٨﴾
8. Na wanalisha chakula, juu ya kuwa wao wanakipenda, masikini na mayatima na mateka.
إِنَّمَا نُطْعِمُكُمْ لِوَجْهِ اللَّـهِ لَا نُرِيدُ مِنكُمْ جَزَاءً وَلَا شُكُورًا﴿٩﴾
9. Hakika sisi tunakulisheni kwa ajili ya Wajihi wa Allaah, hatukusudii kutoka kwenu jazaa wala shukurani.
إِنَّا نَخَافُ مِن رَّبِّنَا يَوْمًا عَبُوسًا قَمْطَرِيرًا﴿١٠﴾
10. Hakika sisi tunaikhofu kutoka kwa Rabb wetu siku ya masononeko, ngumu na ndefu mno.
فَوَقَاهُمُ اللَّـهُ شَرَّ ذَٰلِكَ الْيَوْمِ وَلَقَّاهُمْ نَضْرَةً وَسُرُورًا﴿١١﴾
11. Basi Allaah Atawakinga na shari ya siku hiyo, na Atawapa nuru ya ujamali na furaha.
وَجَزَاهُم بِمَا صَبَرُوا جَنَّةً وَحَرِيرًا﴿١٢﴾
12. Na Atawalipa kwa sababu ya kusubiri kwao, Jannah na nguo za hariri.
مُّتَّكِئِينَ فِيهَا عَلَى الْأَرَائِكِ ۖ لَا يَرَوْنَ فِيهَا شَمْسًا وَلَا زَمْهَرِيرًا﴿١٣﴾
13. Wataegemea humo juu ya makochi ya fakhari, hawatoona humo joto la jua wala baridi kali.
وَدَانِيَةً عَلَيْهِمْ ظِلَالُهَا وَذُلِّلَتْ قُطُوفُهَا تَذْلِيلًا﴿١٤﴾
14. Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao na yatainamishwa matunda yake ya kuchumwa, yawakurubie.
وَيُطَافُ عَلَيْهِم بِآنِيَةٍ مِّن فِضَّةٍ وَأَكْوَابٍ كَانَتْ قَوَارِيرَا﴿١٥﴾
15. Na watazungushiwa vyombo vya fedha, na bilauri za vigae.
قَوَارِيرَ مِن فِضَّةٍ قَدَّرُوهَا تَقْدِيرًا﴿١٦﴾
16. Vigae safi kutokana na fedha wamezipima kwa kipimo.
وَيُسْقَوْنَ فِيهَا كَأْسًا كَانَ مِزَاجُهَا زَنجَبِيلًا﴿١٧﴾
17. Na watanyweshwa humo kikombe cha mvinyo ambao mchanganyiko wake ni tangawizi.
عَيْنًا فِيهَا تُسَمَّىٰ سَلْسَبِيلًا﴿١٨﴾
18. (Mvinyo utokao) chemchemu iliyomo humo inayoitwa Salsabiyl.
وَيَطُوفُ عَلَيْهِمْ وِلْدَانٌ مُّخَلَّدُونَ إِذَا رَأَيْتَهُمْ حَسِبْتَهُمْ لُؤْلُؤًا مَّنثُورًا﴿١٩﴾
19. Na watawazungukia wavulana wa kudumishwa, utakapowaona, utawadhania ni lulu zilizotawanywa.
وَإِذَا رَأَيْتَ ثَمَّ رَأَيْتَ نَعِيمًا وَمُلْكًا كَبِيرًا﴿٢٠﴾
20. Na utakapoona huko, utaona neema na ufalme adhimu.
عَالِيَهُمْ ثِيَابُ سُندُسٍ خُضْرٌ وَإِسْتَبْرَقٌ ۖ وَحُلُّوا أَسَاوِرَ مِن فِضَّةٍ وَسَقَاهُمْ رَبُّهُمْ شَرَابًا طَهُورًا﴿٢١﴾
21. Juu yao watavaa nguo za hariri nyororo za kijani na za hariri nyororo za makhmel, na watapambwa vikuku vya fedha, na Rabb wao Atawanywesha kinywaji kitwaharifu.
إِنَّ هَـٰذَا كَانَ لَكُمْ جَزَاءً وَكَانَ سَعْيُكُم مَّشْكُورًا﴿٢٢﴾
22. (Wataambiwa): Hakika haya ni jazaa yenu, kwani juhudi zenu zimethaminiwa.
إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْقُرْآنَ تَنزِيلًا﴿٢٣﴾
23. Hakika Sisi Tumekuteremshia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Qur-aan uteremsho wa hatua kwa hatua.
فَاصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ وَلَا تُطِعْ مِنْهُمْ آثِمًا أَوْ كَفُورًا﴿٢٤﴾
24. Basi fanya subira kwa Hukumu ya Rabb wako, na wala usimtii miongoni mwao atendaye dhambi au mwingi wa kukufuru.
وَاذْكُرِ اسْمَ رَبِّكَ بُكْرَةً وَأَصِيلًا﴿٢٥﴾
25. Na lidhukuru Jina la Rabb wako asubuhi na jioni.
وَمِنَ اللَّيْلِ فَاسْجُدْ لَهُ وَسَبِّحْهُ لَيْلًا طَوِيلًا﴿٢٦﴾
26. Na katika sehemu ya usiku msujudie, na uswali kwa ajili Yake usiku mrefu.
إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ يُحِبُّونَ الْعَاجِلَةَ وَيَذَرُونَ وَرَاءَهُمْ يَوْمًا ثَقِيلًا﴿٢٧﴾
27. Hakika hawa wanapenda uhai wa dunia na wanaacha nyuma yao siku nzito (ya Qiyamaah).
نَّحْنُ خَلَقْنَاهُمْ وَشَدَدْنَا أَسْرَهُمْ ۖ وَإِذَا شِئْنَا بَدَّلْنَا أَمْثَالَهُمْ تَبْدِيلًا﴿٢٨﴾
28. Sisi Tumewaumba, na Tumetia nguvu viungo vyao. Na kama Tukitaka, Tutawabadilisha mfano wao badala yao.
إِنَّ هَـٰذِهِ تَذْكِرَةٌ ۖ فَمَن شَاءَ اتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِ سَبِيلًا﴿٢٩﴾
29. Hakika haya ni mawaidha. Basi anayetaka achukue njia ya kuelekea kwa Rabb wake.
وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا﴿٣٠﴾
30. Na hamtoweza kutaka isipokuwa Atake Allaah. Hakika Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.
يُدْخِلُ مَن يَشَاءُ فِي رَحْمَتِهِ ۚ وَالظَّالِمِينَ أَعَدَّ لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا﴿٣١﴾
31. Anamuingiza Amtakaye katika Rahmah Yake, na madhalimu Amewaandalia adhabu iumizayo.
