Fadhila Za Siku Ya 'Arafah Na Yawmun-Nahr (Siku Ya Kuchinja)

Fadhila Za Siku Ya 'Arafah Na Yawmun-Nahr (Siku Ya Kuchinja)

 

Alhidaaya.com

 

 

‘Arafah ni jabali ambalo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisimama katikati ya bonde lake kuhutubia Maswahaba katika Hajjatul-widaa’i. (hajj ya kuaga), na hapo ndipo wanaposimama Mahujaji kutimiza fardhi ya Hajj. Kusimama hapo ndio nguzo mojawapo kuu ya Hajj. Bila ya kusimama ‘Arafah hijjah ya mtu itakuwa haikutimia kwa dalili ifuatayo:

 

عن عبد الرحمن بن يعمر قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((الْحَجُّ عَرَفَة، مَنْ جَاءَ قَبْلَ طُلُوعِ الْفَجْرِ مِنْ لَيْلَةِ جَمْعٍ فَقَدْ أَدْرَكَ الْحَجّ)) صحيح الجامع   

‘Abdur-Rahmaan bin Ya’mur (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Al-Hajj ni ‘Arafah, atakayekuja kabla kutoka Alfajiri usiku wa kujumuika atakuwa ameipata Hajj)) [Swahiyh Al-Jaami’].

 

 

 

A-Fadhila Za Siku ya ‘Arafah:

 

1-Ni Siku Iliyokamilika Dini Yetu  

 

عَنْ طَارِقِ بْنِ شِهَابٍ قَالَ: جَاءَ رَجُلٌ مِنَ الْيَهُودِ إِلَى عُمَرَ، فَقَالَ: يَا أَمِيرَ الْمُؤْمِنِينَ، آيَةٌ فِي كِتَابِكُمْ تَقْرَؤُونَهَا، لَوْ عَلَيْنَا نَزَلَتْ مَعْشَرَ الْيَهُودِ، لَاتَّخَذْنَا ذَلِكَ الْيَوْمَ عِيدًا. قَالَ: وَأَيُّ آيَةٍ؟ قَالَ: ((الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمْ الْإِسْلَامَ دِينًا)) فَقَالَ عُمَرُ: إِنِّي لَأَعْلَمُ الْيَوْمَ الَّذِي نَزَلَتْ فِيهِ، وَالْمَكَانَ الَّذِي نَزَلَتْ فِيهِ، نَزَلَتْ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ،  بِعَرَفَاتٍ، فِي يَوْمِ جُمُعَةٍ.

Twaariq bin Shihaab (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba alikuja Myahudi mmoja kwa ‘Umar akasema: Ee Amiri wa Waumini! Aayah katika Kitabu chenu mnaisoma, kama ingeteremkwa kwetu hadhara ya Mayahudi, basi bila shaka tungeifanya siku hiyo kuwa ni siku ya kusherehekea. Akasema (‘Umar): Aayah ipi? Akasema: ((Leo Nimekukamilishieni Dini yenu na Nimekutimzieni Neema Zangu kwenu na Nimekuridhieni Uislamu kuwa ni Diyn yenu)) [Al-Maaidah (5: 3] ‘Umar akasema: Hakika naijua siku gani imeteremka Aayah hii, na sehemuu iliyoteremkia, imeteremka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa ‘Arafah, siku ya Ijumaa.  [Muslim]

 

Ilikuwa ni mara ya kwanza Waislamu kutekeleza Hajj, kwa hiyo imemaanishwa kukamilika dini yao baada ya kukamilisha kutumiza nguzo za Kiislamu zote. 

 

 

2-Kufunga Swawm ni kufutiwa madhambi ya miaka miwili:

 

Ni fadhila kubwa kwa Waislamu kufutiwa madhambi yao.

 

عَنْ أَبِي قَتَادَةَ رضي الله عنه أن النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ :  ((صِيَامُ يَوْمِ عَرَفَةَ أَحْتَسِبُ عَلَى اللَّهِ أَنْ يُكَفِّرَ السَّنَةَ الَّتِي قَبْلَهُ وَالسَّنَةَ الَّتِي بَعْدَهُ )) أخرجه مسلم

Abuu Qataadah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Swawm ya 'Arafah nataraji (kwa Allaah) kufuta madhambi ya mwaka uliopita na wa baada yake)) [Muslim]

 

Kufunga Swawm siku ya ‘Arafah ni makhsusi kwa wasiokuweko huko ‘Arafah siku hiyo. Ama mahujaji hawatakiwi kufunga Swawm siku hiyo kwa dalili:

 

عنْ مَيْمُونَةَ زَوْجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، أَنَّهَا قَالَتْ: إِنَّ النَّاسَ شَكُّوا فِي صِيَامِ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَوْمَ عَرَفَةَ، فَأَرْسَلَتْ إِلَيْهِ مَيْمُونَةُ بِحِلَابِ اللَّبَنِ، وَهُوَ وَاقِفٌ فِي الْمَوْقِفِ، فَشَرِبَ مِنْهُ وَالنَّاسُ يَنْظُرُونَ إِلَيْهِ

Mama wa Waumini Maymuwnah bint Al-Haarith (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) amehadithia kwamba watu walitia shaka kuhusu Swawm ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa  aalihi wa sallam) [kama alifunga] Siku ya ‘Arafah, nikampelekea maziwa, naye akiwa amesimama akayanywa na huku watu wanamtazama.  [Al-Bukhaariy]

 

 

3-Siku Ambayo Wataokolewa Waja Kutokana Na Moto; Wataghufuriwa Madhambi Yao

 

عن  جابر  رضي الله عنه  عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((مَا مِنْ يَوْمٍ أَفْضَلُ عِنْدَ اللَّهِ مِنْ يَوْمِ عَرَفَةَ، يَنْزِلُ اللَّهُ تَعَالَى إلَى سَمَاءِ الدُّنْيَا فَيُبَاهِي بِأَهْلِ الْأَرْضِ أَهْلَ السَّمَاءِ)) وروى ابن حبان

وفي رواية: ((إنَّ اللَّهَ يُبَاهِي بِأَهْلِ عَرَفَةَ مَلَائِكَتَهُ، فَيَقُولُ: يَا مَلَائِكَتِي، اُنْظُرُوا إلَى عِبَادِي، قَدْ أَتَوْنِي شُعْثا غُبْرا ضَاحِينَ))

Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa  aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna siku iliyo bora kabisa mbele ya Allaah kama siku ya ‘Arafah. Anateremka Allaah Ta’ala mbingu ya dunia (ya kwanza) kisha Anawafakhiri watu  ardhi  kwa watu wa mbingu))

 

Na pia:

 

عن عبدالله بن عمرو إنَّ اللهَ عزَ وجلَّ يباهي ملائكتَهُ عشيةَ عرفةَ بأهلِ عرفةَ فيقولُ : انظروا إلى عبادي أتوني شُعثا غُبرا

((Hakika Allaah (‘Azza wa Jalla) Huwafakharisha watu ‘Arafah kwa Malaika Wake jioni ya ‘Arafah na Husema: “Watazameni waja Wangu wamenijia wakiwa timtimu wamejaa vumbi.”)) [Musnad Ahmad (12/42) na ameisahihisha Imaam Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Targhiyb (1153), Swahiyh Al-Jaami’ (1868), Taz pia As-Silsilah Asw-Swahiyhah (1503)

 

Pia,

 قَالَتْ عَائِشَةُ إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ مَا مِنْ يَوْمٍ أَكْثَرَ مِنْ أَنْ يُعْتِقَ اللَّهُ فِيهِ عَبْدًا مِنْ النَّارِ مِنْ يَوْمِ عَرَفَةَ وَإِنَّهُ لَيَدْنُو ثُمَّ يُبَاهِي بِهِمْ الْمَلَائِكَةَ فَيَقُولُ مَا أَرَادَ هَؤُلَاءِ. اشْهَدُوا مَلاَئِكَتِي أَنِّي قَدْ غَفَرْتُ لَهُمْ. صحيح الترغيب

‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakuna siku Anayoacha Allaah kwa wingi huru waja kutokana na moto kama siku ya ‘Arafah. Na huwa karibu kisha Anajigamba kwao kwa Malaika na Husema: Wametaka nini hawa? Shuhudieni Malaika wangu kwamba hakika Mimi Nimewaghufuria)) [Swahiyh At-Targhiyb]

 

Pia:

عن جابر  قال: قال رَسُوْلُ الله صلى الله عليه وسلم : (( ما مِنْ أيامٍ عِنْدَ الله أَفْضَل مِنْ عَشْرِ ذِي الحِجَة)) قَال: فَقَالَ رَجُلٌ: يا رَسُولُ الله هُنُّ أَفْضَلُ أمْ عَدَدَهُنَّ جِهَادًا في سَبِيلِ الله؟ قال: ((هُنَّ أَفْضَل مِنْ عَدَدُهْنَّ جِهادًا في سَبِيلِ الله، ومَاَ مِنْ يَوْم أفْضَلُ عِنْد الله مِنْ يَوم عَرَفةَ: يَنْزِلُ الله تَبَارْكَ وتَعَالى إلى السْمَاءِ الدُّنيا فَيُباهي بِأهْلِ الأرض أهَلْ السْمَاءِ، فيقول: انْظُروا إلى عِبَادِي جَاءوا شُعْثًا غُبْرًا حَاجِين جَاءْوا مِنْ كُلِ فجٍّ عَمِيقْ يَرجُونَ رَحْمَتي ولم يَروا عَذَابي، فَلَم يُرَ يومٌ أكثر عتيقًا مِنْ النَّار مِنْ يَوم عَرَفْة))

Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna Siku iliyo bora kabisa kama siku kumi za Dhul-Hijjah, akasema mtu: “Ee Rasuli wa Allaah, hizo ni bora au jihaadi katika njia ya Allaah? Akasema: ((Hizo ni bora kuliko jihaad katika njia ya Allaah, na hakuna siku bora kabisa mbele ya Allaah, kama siku ya ‘Arafah, Anateremka Allaah Tabaaraka wa Ta’aalaa katika mbingu ya dunia kisha Anawafakhiri watu wa ardhini kwa watu wa mbinguni kisha Anasema: Tazameni waja Wangu wamenijia timtimu wamejaa vumbi wamekuja kutoka kila pembe ya mbali wanataraji rahmah Yangu na wala hawajaona adhabu Yangu. Na wala hakuona siku inayoachwa huru shingo kutokana na moto kama siku ya ‘Arafah)) [At-Targhiyb wat-Tarhiyb – Isnaad yake Swahiyh au Hasan]

  

4-Siku Ya Kutakabaliwa Du’aa

 

Amesema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa  aalihi wa sallam):

 

 ((خَيْرُ الدُّعَاءِ دُعَاءُ يَوْمِ عَرَفَةَ، وخَيْرُ مَا قُلْتُ أنَا وَالنَّبيُّونَ مِنْ قَبْـلِي: لَا إِلَهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لا شَرِيْكَ لَهُ، لَهُ الـمُلْكُ، ولَهُ الـحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيءٍ قَدِير)) روى الترمذي

((Du’aa bora kabisa ni du’aa katika siku ya 'Arafah, na yaliyo bora kabisa niliyosema mimi na Manabii kabla yangu ni:

 

لَا إِلَهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لا شَرِيْكَ لَهُ، لَهُ الـمُلْكُ، ولَهُ الـحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيءٍ قَدِير

 

'Laa Ilaaha illa Allaah Wah-dahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku wa-Lahul-hamdu wa Huwa 'alaa kulli shay-in Qadiyr

 

Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, Hana mshirika, ufalme wote ni Wake, na Himdi zote ni Zake, Naye ni Mweza wa kila kitu daima)) [Swahiyh At-Tirmidhiy (3/184), Silsilatu Al-Ahaadiyth Asw-Swahiyhah (4/6)]

 

 

5-Siku Ambayo Allaah Ameiapia

 

Allaah Ameiapia siku hii ya ‘Arafah ambayo inajulikana kwa ‘Siku ya Kushuhudiwa’. Hii kutokana na kauli Yake Subhaanahu wa Ta’ala:

وَالسَّمَاءِ ذَاتِ الْبُرُوجِ ﴿١﴾

Naapa kwa mbingu zenye sayari kubwa zilizodhahiri.

وَالْيَوْمِ الْمَوْعُودِ ﴿٢﴾

Na (Naapa kwa) Siku iliyoahidiwa (ya Qiyaamah). 

 

وَشَاهِدٍ وَمَشْهُودٍ ﴿٣﴾

Na (Naapa kwa) shahidi na kinachoshuhudiwa.  [Al-Buruwj 85: 1-3]

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللّهِ صَلّى اللّه عَلَيْهِ وَسَلّمَ: ((الْيَوْمُ الْمَوْعُودُ يَوْمُ الْقِيَامَةِ وَالْيَوْمُ الْمَشْهُودُ هُوَ يَوْمُ عَرَفَةَ وَالشّاهِدُ يَوْمُ الْجُمُعَةِ))

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa alihi wa sallam) amesema: ((Siku ya kuahidiwa ni siku ya kufufuliwa. Siku ya kushuhudiwa ni siku ya ‘Arafah, na Siku ya kinachoshuhudiwa ni Siku ya Ijumaa)) [At-Tirmidhiy, Swahiyh Al-Jaami’ (8201)]

 

 

6-Siku Ambayo Allaah Amechukua Fungamano (ahadi) Kutoka Kizazi Cha Aadam

 

 عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ( أَخَذَ اللهُ الْمِيثَاقَ مِنْ ظَهْرِ آدَمَ، فَأَخْرَجَ مِنْ صُلْبِهِ كُلَّ ذُرِّيَّةٍ ذَرَأَهَا، فَنَثَرَهُمْ بَيْنَ يَدَيْهِ كَالذَّرِّ ، ثُمَّ كَلَّمَهُمْ قِبَلًا، قَالَ:(( أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ ؟ قَالُوا بَلَى شَهِدْنَا أَنْ تَقُولُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّا كُنَّا عَنْ هَذَا غَافِلِينَ، أَوْ تَقُولُوا إِنَّمَا أَشْرَكَ آبَاؤُنَا مِنْ قَبْلُ وَكُنَّا ذُرِّيَّةً مِنْ بَعْدِهِمْ أَفَتُهْلِكُنَا بِمَا فَعَلَ الْمُبْطِلُونَ))

Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah Amechukua fungamano kutoka mgongo wa Aadam katika Na’maan yaani ‘Arafah. Akalete mbele mgongo wake kizazi chake chote na akawatandaza mbele Yake, kisha Akawakabali kuwauliza: “Je, Mimi siye Rabb wenu?” Wakasema: “Ndiye, tunashuhudia!” (Allaah Akawaambia): “Msije kusema Siku ya Qiyaamah: hakika sisi tulikuwa tumeghafilika nayo haya. Au mkasema: “Hakika baba zetu ndio walioshirikisha kabla, nasi tulikuwa kizazi baada yao. Basi Utatuangamiza kwa yale waliyoyafanya wabatilifu?” (Al-A’raaf 7: 172-173) [Ameipokea Ahmad na imepewa daraja ya Swahiyh na Shaykh Al-Albaaniy]

 

B-Fadhila Za Yawmun-Nahr – Siku ya Kuchinja:

 

Siku kuu ya ‘Iydul-Adhw-haa na ndio inajulikana pia kwa Yawmun-Nahr. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: 

 

 ((إنَّ أَعْظَمَ اْلأيَّامِ عِنْدَ الله تبارك وتعالى يَوْمُ النَّحْرِ ثُمَّ يَوْمُ الْقَرِّ)) رواه أبو داود والنسائي وصححه الألباني

((Siku iliyo tukufu kabisa kwa Allaah ni siku ya kuchinja, kisha siku ya kutulia (siku ya Minaa)) [Abuu Daawuwd]

 

Sababu ya kuchinja ni kufuata Sunnah ya baba yetu Nabiy ‘Ibraahiym (‘Alayhis-Salaam) alipotaka kumchinja mwanawe Ismaa’iyl na Allaah Akamteremshia badala yake kafara ya mnyama.

 

Bonyeza kiungo kifuatacho upate faida ziyada:

 

Kuchinja - Fadhila, Hikmah Na Hukmu Zake

 

 

 

Share