Hajj

Hajj

Makosa Yanayofanywa Baada Ya Kumaliza Hajj na Kurudi Nyumbani - Kutoka Kitabu Cha Alhidaayah Katika Manaasik Za Hajj Na ‘Umrah

Muislamu anapomaliza Hajj anapaswa kuthibitika katika ‘Ibaadah zake. Kubakia katika istiqaamah (kuthibitika) ni dalili ya kutakabaliwa Hajj yako. Aayah na Hadiyth kadhaa zimetaja kuhusu jambo hili; baadhi ni hizi zifuatazo:

Share

Mdhukuru Allaah Kwa Wingi Na Omba Maghfirah Baada Ya Kutenda Mema Katika Siku Kumi Bora Kabisa Za Allaah

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) 

وَاذْكُرُوا اللَّـهَ فِي أَيَّامٍ مَّعْدُودَاتٍ ۚ  

Na mdhukuruni Allaah katika siku za kuhesabika.  [[Al-Baqarah:203]

 

Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kasema: "Siku zinazohisabiwa ni siku za Tashriyq" (11, 12, 13 Dhul-Hijjah) [Al-Qurtwubiy: 3.3] Kwa maana ni siku ya pili, ya tatu na ya nne baada ya siku ya 'Iyd. Hivyo ndivyo Anavyotuamrisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  kuwa tumdhukuru baada ya kusherehekea siku kuu yetu ya 'Iydul-Adhwhaa ('Iyd ya kuchinja). Na hivi ndivyo ilivyo desturi ya ‘ibaadah zetu kuwa zinamalizika kwa kuambatana na mema na si kwa maasi.

 

Mahujaji wanapotekeleza Hajj ipasavyo na wanapomaliza kisimamo cha 'Arafah, huwa wameghufuriwa madhambi yao yote kama ilivyotajwa katika Hadiyth ifuatayo:

 

Share

Pages

Subscribe to RSS - Hajj