Vitumbua Vya Kuku 2

 

Vitumbua Vya Kuku 2

(Kupata vitumbua 37 takriban)

 

 

Vipimo

Kuku kidari (Steak) 1 kilo

Mayai 10

Unga  wa dengu 3 vya supu

Baking powder kijiko 1 cha chai

Kotmiri fungu 1 kubwa au 2 madogo (bunch) – katakata (chop)

Vitunguu maji 2 – menya na katakata

Pilipili mboga 1 - katakata

Kidonge cha supu 1

Pilipili mbichi 1 

Pilipili manga 2 vijiko vya chai

Chumvi ½ kijiko cha chai

Mafuta – kiasi ya kuchomea

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Katakata kuku vipande kisha kausha kwa ndimu kidogo chumvi pilipili manga. Epua.
  2. Changanya na upige katika blender mayai, unga, baking powder, pilipili mbichi, chumvi, pilipili manga, kidonge cha supu na kuku.
  3. Mimina katika bakuli kisha tia vitunguu, pilipili mboga, kotmiri changanya pamoja.
  4. Choma katika kama unavyopika vitumbua. Jaribu kimoja ikiwa chepesi ongeza unga wa dengu. Ikiwa nzito ongeza maziwa kidogo utokee kama uzito wa vitumbua.
  5. Epua uchuje mafuta vikiwa tayari.

 

 Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)  

 

 

Share