Vikeki Vya Vikombe Vya Vanilla Kwa Icing Ya Cocoa Na Kahawa

Vikeki Vya Vikombe Vya Vanilla Kwa Icing Ya Cocoa Na Kahawa

 

 

 

Vipimo

 

Kutengenezea keki 24 takriban

 

Unga wa keki – vikombe 2 vilojaa

Mayai – manne – tenganisha ute na kiini.

Baking powder – 4 vijiko cha chai

Vanilla – 1 kijiko cha chai

Sukari – 1 ½ kikombe

Maziwa – 1 kikombe

Mafuta ½ kikombe

Siagi – 1 ½ kijiko cha kulia

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

 

  1. Changanya unga pamoja na baking powder.
  2. Piga katika machine ute wa mayai pamoja na kijiko 1 (kimoja) cha baking powder. Piga mpaka iwe yabisi (stiff).
  3. Tia sukari polepole huku unaendelea kupiga na kuchanganya.
  4. Tia viini vya yai na vanilla na endelea kupiga.
  5. Changanya maziwa, mafuta na siagi kisha uchemshe na ipoe.
  6. Wacha machine katika speed ndogo kabisa huku unachanganya mchanganyiko wa unga pole pole na hukku unatia mchanganyiko wa maziwa na kuchanganyika vizuri.
  7. Teka mchanganyiko na ugawe katika vikombe vya karatasi za keki au vibakuli ya kupikia keki (muffin bowls).
  8. Choma (bake) kwa dakika 15 – 20 takriban mpaka iwe unapotia kijiti kuhakikisha kinatoka kikiwa hakinati.

 

 

Mwagio Wa Chokoleti (Chocolate Topping)

 

Vipimo:

 

Cream – kibati kimoja kidogo

Icing sugar – kiasi upendavyo

Unga wa cocoa – vijiko 2 vya kulia

Unga wa kahawa – kijiko ½ cha chai

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

 

 

  1. Changanya vitu vyote kisha tia katika kibomba cha icing sugar uzungurushie juu ya vikeki.
  2. Ukipenda pambia mrashio wa sukari ya rangi rangi au vipipi vya rangi rangi.

 

Ikiwa mchanganyiko umetokea mzito ongezea 1 kijiko cha maziwa.

 

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

 

 

 

Share