Ukumbusho Wa Kuzuia Kukata Kucha Na Nywele Kwa Anayenuia Kuchinja

Ukumbusho Wa Kuzuia Kukata Kucha Na Nywele Kwa Anayetaka Kuchinja

 

 

Alhidaaya.com

 

 

Tunapenda kuwakumbusha ndugu zetu wengi jambo ambalo wanaghafilika nalo, kuwa, wenye kunuia kuchinja au kuchinjiwa (anayewakilisha mtu kumchinjia), kuanzia unapoingia tu mwezi wa Dhul-Hijjah wanatakiwa wajizuie kukata nywele za mwili na kucha mpaka watakapomaliza kuchinja. Haya ni maamrisho yanayopatikana katika Hadiyth ifuatayo:  

 

عن أم سلمة رضي الله عنها أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((إِذَا رَأَيْتُمْ هِلَالَ ذِي الْحِجَّةِ وَأَرَادَ أَحَدُكُمْ أَنْ يُضَحِّيَ ، فَلْيُمْسِكْ عَنْ شَعْرِهِ وَأَظْفَارِهِ )) وفي رواية: ((فَلا يَمَسَّ مِنْ شَعَرِهِ وَبَشَرِهِ شَيْئًا))

Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ukiandama mwezi wa Dhul-Hijjah na ikiwa yuko anayetaka kuchinja basi azuie (asikate) nywele zake na kucha zake)) na katika riwaaya nyengine ya Muslim (1977); ((basi asitoe kitu katika nywele zake wala ngozi yake)) [Muslim]

 

Share