Lu-ulu-un-Manthuwrun
(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)
Hadiyth Ya 72
Enezeni Salaam, Lisheni Chakula, Ungeni Undugu, Swalini Tahajjud,
Mtaingia Jannah Kwa Amani
Alhidaaya.com
عَنْ أبِي يُوسُفَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَلاَمٍ (رضي الله عنه) قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ الله صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُول: ((يَا أَيُّهَا النَّاسُ، أَفْشُوا السَّلاَمَ، وَأَطْعِمُوا الطَّعَامَ، وَصِلُوا الأَرْحَامَ، وَصَلُّوا وَالنَّاسُ نِيَامٌ، تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ بِسلاَمٍ)) رواه الترمذي وقال: حديث حسن صحيح
Imepokelewa kutoka kwa Abu Yuwsuf ‘Abdullah bin Salaam (رضي الله عنه) amesema: “Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Enyi watu! Enezeni [amkianeni kwa] Salaam! Na lisheni chakula, na ungeni undugu [na jamaa wa uhusiano wa damu], na swalini wakati watu wamelala, mtaingia Jannah kwa amani)). [At-Tirmidhiy na amesema: Hadiyth Hasan Swahiyh]
Mafunzo Na Mwongozo:
1. Maamkizi ya Kiislamu, kulisha watu, kuunga undugu na kuamka usiku kuswali, ni sababu mojawapo ya kumuingiza Muislamu Jannah, nayo ni mambo mepesi kabisa kuyatenda.
2. Amri, umuhimu na fadhila za kuamkiana kwa maamkizi ya Kiislamu.
Rejea: An-Nisaa (4: 86), An-Nuwr (24: 27-28).
Na rejea pia Hadiyth namba (42).
Bonyeza Kiungo kifuatacho kwa faida ziyada:
Maamkizi Ya Kiislaam: Maamrisho Na Fadhila Zake
3. Sisitizo na himizo la kulisha maskini. Fadhila zake ni adhimu kama kuingizwa katika neema tele za Allaah (سبحانه وتعالى) huko Jannah. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):