SW
Assalamu alaykum warahmatullahi wabarakatuh
Namuomba Allah awalipe malipo mema katika kazi yenu kubwa mnayofana kutujibia maswali yetu. Mmetufunza
Kwa vile nafanya kazi na wanawake wengi nimetambua yafuatayo ambayo yamenitia shaka. Hivo nakuombeni mashekhe wetu mtujibu haya yanayotendeka katika jamii yetu nayo ni: Baadhi ya wanawake wanapokwenda kwa hair-dresser kusuka au kuchana nywele kwa staili ima kwa ajili ya harusi au kujipamba tu – huwa hawataki kuharibu nywele zao kuziosha hivyo wanakaa masiku hawaoshi – kwa sababu huona hasara kupoteza hela kwenda kwa hair dresser kila mara. Hali hii huwafanya:
1- Wakatae kulala na waume zao kufanya kitendo cha ndoa kwa hofu ya kuosha nywele, na waume hupiga huwa hawapati haki zao.
2- Au huwa hawaogi janaba wanabakia na nywele zao zisiharibike.
3- Wengine hawaogi josho la hedhi au janaba wanadai kwamba nywele hazitokauka asubuhi akiosha na atachelewa kwenda kazini.
Hali hiyo huwafanya hata wasiweze kusali kwa siku kadha.
Tunaomba majibu ya ufafanuzi ili tuwafahmishe dada zetu mtindo wao huo
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako muhimu kuhusu masuala yako mchanganyiko ya mambo ya kike. Mwanzo ni muhimu
Tufahamu kuwa ni madhambi makubwa kwa mwanamke kumkatalia mumewe anapomtaka bila udhuru wa kisheria
Ni ajabu kwa wanawake kujipamba tu wanapotaka kwenda harusini na kazini lakini hawawapambii waume zao. Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaah 'anhuma) alikuwa anajipambia kwa ajili ya mkewe
Wanawake wengi pia hukosea kwa kuongeza vipande vya nywele bandia au za kweli juu ya nywele zao na hiyo ni haramu kabisa. Zipo Hadiyth nyingi kuhusu
Kuweka Madawa Ya Nywele Na Kuvaa Nywele Za Bandia
Mwanamke Kupaka Dawa Ya Nywele
Kuvaa Nywele Za Bandia Kufunika Nywele Turkey Kwa Sababu Ya Kukatazwa Hijaab
Nini Hukumu Ya Nywele Za Bandia?
Kusuka Nywele Na Kuchanganya Na Nyuzi Inafaa?
Hukmu Ya Mtu Kuswali Na Kaweka Nywele Za Bandia
Ama kutokuoga kwa ajili ya janaba au hedhi pia ni makosa kwani hiyo inaonyesha utovu wa maadli na kuwa umezifanya nywele zako kuwa ni mungu wako. Allaah Aliyetukuka Anasema:
"Je, umemuona yule aliyefanya matamanio yake (kila anachokipenda) kuwa Mungu wake?" (25: 43).
Na ikiwa ni hivyo basi watu hao watakuwa mahali pabaya
Inafaa dada yetu uwashauri wanawake hao wasiwe ni wenye kufanya hivyo na Allaah Aliyetukuka Atakupa tawfiki katika juhudi hizo.
Na Allaah Anajua zaidi