Anadhani Kapoteza Bikra Kwa Kujichua, Hajui La Kumwambia Atakayemuoa

 

Anadhani Kapoteza Bikra Kwa Kujichua, Hajui La Kumwambia Atakayemuoa

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Mimi ni mzima kwa uwezo wa ALLAH (SWT) natumai wewe pia.  Swali langu ni hivi mie ni msichana wa kiislam ila nimekua nafanya mambo kinyume na maadili ya kiislam. Imefikia wakati sasa ninajionea huruma na sijui hata nifanyaje nina maika 24 sijaolewa bado na sijawahi kuwa na rafiki wa kiume kwasababu nilikua najichunga sana na wanaume ila ilifikia wakati hamu ya kufanya tendo zikaanza kunijia basi nikaanza kujichua kwa vidole kuna siku moja nikatokwa na damu kidogo nilikua sijui kitu chochote kuhusu tendo la ndoa nilipatwa na hofu sana mpaka sasa sijui nitafanyaje. Naomba nijibu hiyo damu inamaanisha bikra yangu imetoka  na nitamwambiaje mume wangu wa baadae kuwa sina bikra na sijawahi kufanya tendo la ndoa inaniuma sana kwasbabu nimejitunza sana halafu nimepoteza bikra yangu bila kujua kwasababu ya kutojua ni nini maana ya tendo la ndoa asant natumai utanijibu vizuri.

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Hakika kufanya ulivyokuwa ukifanya ni kosa Kiislamu na huko ni kama kuuoa au kuolewa na mkono wako ambako Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza.

 

 

Unapaswa uombe msamaha kwa Allaah Aliyetukuka kikweli kweli, utie Niyah ya kutorudia, ujute kwa uliyoyafanya na ufanye mazuri ili hilo baya lifutwe.

 

 

Baada ya kufanya hivyo nenda kwa daktari wa kike ili akupime kama ubikra umeondoka ama bado upo. Ikiwa upo mshukuru Allaah Aliyetukuka, rudi Kwake kwa kuomba toba na kufanya mazuri. Ukiwa ubikira umetoka vumilia kwani huo ni mtihani ambao umekukumba na umuombe Allaah Aliyetukuka Akusitiri usiwe ni mwenye kuingia aibu.

 

 

Ikiwa ubikra wako umeondoka na mume amekuja kukuoa na tunaomba awe wa kheri kwako katika Dini yako na maisha yako na hatima yako,  na endapo baada ya kukuoa akataka kujua sababu za kupoteza ubikra wako, itabidi umweleze yaliyotendeka bila ya kumficha kwani ukweli huo ndio utakaomfanya kujua ukweli na kuridhika kwa hilo na kuishi kwa kuaminiana bila kujengeka wasiwasi wowote ule na wewe na maisha yako ya nyuma.

 

 

Na bila shaka Allaah Atakusitiri kwa kujuta kwa kitendo chako hicho.

 

 

Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo na manufaa zaidi:

 

Wanawake Wanaojichua, Bikira Huweza Kuondoka?

 

Kurudisha Ubikra Haifai Na Ni Udanganyifu

 

Dawa Gani Za Kurudisha Ubikra

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share