00-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Jinai: Mlango Wa Makosa Ya Jinai

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

كِتَابُ اَلْجِنَايَاتِ

Kitabu Cha  Jinai

 

 

بَابُ اَلْجِنَايَاتِ

00-Mlango Wa Makosa Ya Jinai[1]

 

 

 

 

 

992.

عَنْ اِبْنِ مَسْعُودٍ  رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ  صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {لَا يَحِلُّ دَمُ اِمْرِئٍ مُسْلِمٍ، يَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ، وَأَنِّي رَسُولُ اَللَّهِ، إِلَّا بِإِحْدَى ثَلَاثٍ: اَلثَّيِّبُ اَلزَّانِي، وَالنَّفْسُ بِالنَّفْسِ، وَالتَّارِكُ لِدِينِهِ، اَلْمُفَارِقُ لِلْجَمَاعَةِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Ibn Mas-‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Si halaal damu ya mtu Muislam anayeshuhudia kuwa hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah na kuwa mimi ni Rasuli wa Allaah ila kwa mojawapo ya mambo matatu:[2] Mzinifu aliyeoa, nafsi kwa nafsi na aliyeacha Dini yake (aliyeritadi) aliyefarikiana na jamaa (umoja wa Waislam).” [Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

993.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا، عَنْ رَسُولِ اَللَّهِ  صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَ: {لَا يَحِلُّ قَتْلُ مُسْلِمٍ إِلَّا فِي إِحْدَى ثَلَاثِ خِصَالٍ: زَانٍ مُحْصَنٌ فَيُرْجَمُ، وَرَجُلٌ يَقْتُلُ مُسْلِمًا مُتَعَمِّدًا فَيُقْتَلُ، وَرَجُلٌ يَخْرُجُ مِنْ اَلْإِسْلَامِ فَيُحَارِبُ اَللَّهَ وَرَسُولَهُ، فَيُقْتَلُ، أَوْ يُصْلَبُ، أَوْ يُنْفَى مِنْ اَلْأَرْضِ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Si halaal kumuua Muislam ila kwa mojawapo ya mambo matatu: mzinifu aliyehifadhika atapigwa mawe, mtu anayemuua Muislam kwa makusudi naye atauawa, na mtu anayetoka katika Uislam, akawa anampiga vita Allaah na Rasuli wake atauawa, au atasulubiwa na atatolewa katika nchi.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy na akaisahihisha Al-Haakim]

 

 

 

994.

وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ  رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ  صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {أَوَّلُ مَا يُقْضَى بَيْنَ اَلنَّاسِ يَوْمَ اَلْقِيَامَةِ فِي اَلدِّمَاءِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa ‘Abdillaah bin Mas-‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Jambo la kwanza watakalohukumiwa watu siku ya Qiyaamah ni katika damu.”[3] [Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

995.

وَعَنْ سَمُرَةَ  رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ  صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {مَنْ قَتَلَ عَبْدَهُ قَتَلْنَاهُ، وَمَنْ جَدَعَ عَبْدَهُ جَدَعْنَاهُ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَالْأَرْبَعَةُ، وَحَسَّنَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَهُوَ مِنْ رِوَايَةِ اَلْحَسَنِ اَلْبَصْرِيِّ عَنْ سَمُرَةَ، وَقَدْ اُخْتُلِفَ فِي سَمَاعِهِ مِنْهُ

وَفِي رِوَايَةٍ لِأَبِي دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيِّ: {وَمَنْ خَصَى عَبْدُهُ خَصَيْنَاهُ}‏ وَصَحَّحَ اَلْحَاكِمُ هَذِهِ اَلزِّيَادَةَ

Kutoka kwa Samurah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kumuua mtumwa wake, nasi tutamuua, na mwenye kumkata pua mtumwa wake na si tutamkata.”[4] [Imetolewa na Ahmad na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah), na At-Tirmidhiy amesema ni Hasan nayo ni katika Riwaayah ya Al-Hasan Al-Baswriy kutoka kwa Samurah, wametofautiana katika kusikia kwake kwa Samurah au sivyo]

Katika Riwaayah ya Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy kuna ziada hii: “…na mwenye kumhasi mtumwa wake na sisi tutamhasi.”  Al-Haakim ameipa daraja ya sahihi ziada hii.

 

 

 

996.

وَعَنْ عُمَرَ بْنِ اَلْخَطَّابِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اَللَّهِ  صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ يَقُولُ:{لَا يُقَادُ اَلْوَالِدُ بِالْوَلَدِ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ، وَابْنُ مَاجَهْ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ اَلْجَارُودِ وَالْبَيْهَقِيُّ، وَقَالَ اَلتِّرْمِذِيُّ: إِنَّهُ مُضْطَرِبٌ

Kutoka kwa ‘Umar bin Al Khatwaab (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema nilimsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Baba halipizwi kisasi kwa mwanawe.”[5] [Imetolewa na Ahmad, At-Tirmidhiy na Ibn Maajah, na akaisahihisha Ibn Al-Jaaruwd na Al-Bayhaqiyy. Na akasema At-Tirmidhiy ni ‘Mudhwtwarib’][6]

 

 

 

997.

وَعَنْ أَبِي جُحَيْفَةَ قَالَ: {قُلْتُ لَعَلِيٍّ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا: هَلْ عِنْدَكُمْ شَيْءٌ مِنْ اَلْوَحْيِ غَيْرَ اَلْقُرْآنِ ؟ قَالَ: لَا وَاَلَّذِي فَلَقَ اَلْحَبَّةَ وَبَرَأَ اَلنِّسْمَةَ، إِلَّا فَهْمٌ يُعْطِيهِ اَللَّهُ رَجُلًا فِي اَلْقُرْآنِ، وَمَا فِي هَذِهِ اَلصَّحِيفَةِ.‏ قُلْتُ: وَمَا فِي هَذِهِ اَلصَّحِيفَةِ ؟ قَالَ: "اَلْعَقْلُ، وَفِكَاكُ اَلْأَسِيرِ، وَلَا يُقْتَلُ مُسْـلِمٌ بِكَافِرٍ}‏ رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

وَأَخْرَجَهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ: مِنْ وَجْهٍ آخَرَ عَنْ عَلِيٍّ وَقَالَ فِيهِ: {اَلْمُؤْمِنُونَ تَتَكَافَأُ دِمَاؤُهُمْ، وَيَسْعَى بِذِمَّتِهِمْ أَدْنَاهُمْ، وَهُمْ يَدٌ عَلَى مَنْ سِوَاهُمْ، وَلَا يُقْتَلُ مُؤْمِنٌ بِكَافِرٍ، وَلَا ذُو عَهْدٍ فِي عَهْدِهِ}‏ وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ

Kutoka kwa Abuu Juhayfah amesema: Nilisema kumuambia ‘Aliy: Nyinyi mna chochote katika Wahyi isiyokuwa Qur-aan?[7] Akasema: Hapana naapa kwa Aliyepasua mbegu na Akaumba nafsi, isipokuwa fahamu Allaah Humpa mtu katika Qur-aan (kuielewa), na yaliyomo katika sahifa (karatasi) hii. Nikasema katika sahifa hii kuna nini? Akasema: ‘Al ‘aqlu (kanuni za malipo ya damu), diya, kumfungua mateka na Muislam hauwawi kwa kumuua kafiri.[8] [Imetolewa na Al Bukhaariy]

Na wameipokea Ahmad, Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy kwa njia nyingine kutoka kwa ‘Aliy amesema: “Waumini damu zao zinalingana, na anaenda kwa dhima yao aliye karibu nao, nao wako juu ya wengine wala Muumini hauwawi kwa (kumuua) kafiri, wala mwenye mkataba katika mkataba wake.” [Ameisahihisha Al-Haakim]

 

 

 

998.

وَعَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ  رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  {أَنَّ جَارِيَةً وُجَدَ رَأْسُهَا قَدْ رُضَّ بَيْنَ حَجَرَيْنِ، فَسَأَلُوهَا: مَنْ صَنَعَ بِكِ هَذَا ؟ فُلَانٌ.‏ فُلَانٌ.‏ حَتَّى ذَكَرُوا يَهُودِيًّا.‏ فَأَوْمَأَتْ بِرَأْسِهَا، فَأُخِذَ اَلْيَهُودِيُّ، فَأَقَرَّ، فَأَمَرَ رَسُولُ اَللَّهِ  صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ أَنْ يُرَضَّ رَأْسُهُ بَيْنَ حَجَرَيْنِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِمُسْلِمٍ

Kutoka kwa Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: Mjakazi mmoja alipatikana hali ya kuwa kichwa chake kimepondwa katikati ya mawe mawili. Akaulizwa ni nani aliyekufanyia hivi? Ni fulani? Ni fulani? Hadi wakamtaja Myahudi, akaashiria kwa kichwa. “Ndiye” yule Myahudi akashikwa na akaungama. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akaamuru kichwa chake kipondwe baina ya mawe mawili.[9] [Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Muslim]

 

 

 

999.

وَعَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَيْنٍ  رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  {أَنَّ غُلَامًا لِأُنَاسٍ فُقَرَاءَ قَطَعَ أُذُنَ غُلَامٍ لِأُنَاسٍ أَغْنِيَاءَ، فَأَتَوا اَلنَّبِيَّ  صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ فَلَمْ يَجْعَلْ لَهُمْ شَيْئًا} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَالثَّلَاثَةُ، بِإِسْنَادٍ صَحِيحٍ

Kutoka kwa ‘Imraan bin Huswayn (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: Kijana wa watu mafukara[10] alikata sikio la watu matajiri, wakamuendea Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) basi hawakuwapa chochote. [Imetolewa na Ahmad na Ath-Thalaathah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd) kwa isnaad Swahiyh]

 

 

 

1000.

وَعَنْ عَمْرِوِ بْنِ شُعَيْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ،  رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  {أَنَّ رَجُلًا طَعَنَ رَجُلًا بِقَرْنٍ فِي رُكْبَتِهِ، فَجَاءَ إِلَى اَلنَّبِيِّ  صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ فَقَالَ: أَقِدْنِي.‏ فَقَالَ: "حَتَّى تَبْرَأَ".‏ ثُمَّ جَاءَ إِلَيْهِ.‏ فَقَالَ: أَقِدْنِي، فَأَقَادَهُ، ثُمَّ جَاءَ إِلَيْهِ.‏ فَقَالَ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! عَرِجْتُ، فَقَالَ: "قَدْ نَهَيْتُكَ فَعَصَيْتَنِي، فَأَبْعَدَكَ اَللَّهُ، وَبَطَلَ عَرَجُكَ".‏ ثُمَّ نَهَى رَسُولُ اَللَّهِ  صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ "أَنْ يُقْتَصَّ مِنْ جُرْحٍ حَتَّى يَبْرَأَ صَاحِبُهُ"} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَاَلدَّارَقُطْنِيُّ، وَأُعِلَّ بِالْإِرْسَالِ

Kutoka kwa ‘Amr bin Shu’ayb kutoka kwa baba yake naye kutoka kwa babu yake (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: Mtu mmoja alimchoma mtu kwa pembe katika goti lake, (yule aliyedungwa) akamuendea Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Nilipizie kisasi.?” Akamuambia: “Subiri mpaka upone.” Yule mtu akasisitiza: “Nilipizie kisasi.?” Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamlipizia kisasi, kisha akamjia tena akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Nimekuwa kiwete.” Akamuambia: “Nilikukataza ukaniasi, Allaah Akakuweke mbali (na Rahma Zake), na ulemavu wako umebatilika.”[11] Kisha Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikataza mtu kulipiziwa kisasi cha jeraha mpaka aliyejeruhiwa apone. [Imetolewa na Ahmad na Ad-Daaraqutwniy na imetiwa ila kuwa ni Mursal]

 

 

 

1001.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ  رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: {اِقْتَتَلَتِ اِمْرَأَتَانِ مِنْ هُذَيْلٍ، فَرَمَتْ إِحْدَاهُمَا اَلْأُخْرَى بِحَجَرٍ، فَقَتَلَتْهَا وَمَا فِي بَطْنِهَا، فَاخْتَصَمُوا إِلَى رَسُولِ اَللَّهِ  صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ فَقَضَى رَسُولُ اَللَّهِ  صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ أَنَّ دِيَةَ جَنِينِهَا: غُرَّةٌ، عَبْدٌ أَوْ وَلِيدَةٌ، وَقَضَى بِدِيَةِ اَلْمَرْأَةِ عَلَى عَاقِلَتِهَا.‏ وَوَرَّثَهَا وَلَدَهَا وَمَنْ مَعَهُمْ.‏ فَقَالَ حَمَلُ بْنُ اَلنَّابِغَةِ اَلْهُذَلِيُّ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! كَيْفَ يَغْرَمُ مَنْ لَا شَرِبَ، وَلَا أَكَلَ، وَلَا نَطَقَ، وَلَا اِسْتَهَلَّ، فَمِثْلُ ذَلِكَ يُطَلُّ، فَقَالَ رَسُولُ اَللَّهِ  صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  "إِنَّمَا هَذَا مِنْ إِخْوَانِ اَلْكُهَّانِ"، مِنْ أَجْلِ سَجْعِهِ اَلَّذِي سَجَعَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

وَأَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ: مِنْ حَدِيثِ اِبْنِ عَبَّاسٍ، أَنَّ عُمَرَ  رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  سَأَلَ مَنْ شَهِدَ قَضَاءَ رَسُولِ اَللَّهِ  صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ فِي اَلْجَنِينِ ؟ قَالَ: فَقَامَ حَمَلُ بْنُ اَلنَّابِغَةِ، فَقَالَ: كُنْتُ بَيْنَ اِمْرَأَتَيْنِ، فَضَرَبَتْ إِحْدَاهُمَا اَلْأُخْرَى.‏.‏.‏ فَذَكَرَهُ مُخْتَصَرًا.‏ وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ، وَالْحَاكِمُ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Wanawake wawili wa Hudhayl walipigana, mmoja akamrushia jiwe mwenzie akamuuwa pamoja na kilicho tumboni mwake. Wakashtakiana kwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akahukumu: Diya ya mtoto wake (aliyekuwa tumboni)[12] ni mtumwa au mjakazi. Na akahukumu Diya ya mwanamke iwe juu ya jamaa zake (kwa baba). Akamrithisha mwanaye (yule mwanamke) na jamaa zao. Hamal bin An-Naabighat Al Hudhaliy[13] akasema Ee Rasuli wa Allaah! Vipi nimlipe ambaye hajanywa wala hajala, wala hakutamka wala hakulia? Na mfano wao hawalipwi. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema kuhusu mtu huyu: “Huyu ni ndugu wa makuhani.”[14] Kwa sababu ya mizani ya maneno yake anayotoa. [Bukhaariy, Muslim]

Na imetolewa na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy kutoka katika Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas kuwa: ’Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) aliuliza: Ni nani aliyeshuhudia hukumu ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) katika mtoto aliye tumboni? Hamal bin-An Naabighat akasimama akasema: Nilikuwa ni baina ya wanawake na mmoja kati yao akampiga mwenzie. Akaitaja Hadiyth hii kwa mukhtasari. Na akaisahihisha Ibn Hibbaan na Al-Haakim

 

 

 

1002.

وَعَنْ أَنَسٍ  رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  {أَنَّ اَلرُّبَيِّعَ بِنْتَ اَلنَّضْرِ عَمَّتَهُ كَسَرَتْ ثَنِيَّةَ جَارِيَةٍ، فَطَلَبُوا إِلَيْهَا اَلْعَفْوَ، فَأَبَوْا، فَعَرَضُوا اَلْأَرْشَ، فَأَبَوْا، فَأَتَوْا رَسُولَ اَللَّهِ  صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ وَأَبَوْا إِلَّا اَلْقِصَاصَ، فَأَمَرَ رَسُولُ اَللَّهِ  صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ بِالْقِصَاصِ، فَقَالَ أَنَسُ بْنُ اَلنَّضْرِ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! أَتُكْسَرُ ثَنِيَّةُ اَلرُّبَيِّعِ ؟ لَا، وَاَلَّذِي بَعَثَكَ بِالْحَقِّ، لَا تُكْسَرُ ثَنِيَّتُهَا، فَقَالَ رَسُولُ اَللَّهِ  صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ "يَا أَنَسُ! كِتَابُ اَللَّهِ: اَلْقِصَاصُ".‏ فَرَضِيَ اَلْقَوْمُ، فَعَفَوْا، فَقَالَ رَسُولُ اَللَّهِ  صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ : "إِنَّ مِنْ عِبَادِ اَللَّهِ مَنْ لَوْ أَقْسَمَ عَلَى اَللَّهِ لَأَبَرَّهُ"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيِّ

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: Ar-Rubayyi’ bint An-Nadhwr[15] shangazi yake alivunja meno ya msichana mmoja, wakamuombea msamaha, wakakataa, wakawapa fidia ya jeraha, wakakataa, wakaenda kwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) wakakataa ila kisasi. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akaamuru walipiziwe kisasi. Anas bin An-Nadhwr[16] akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Meno ya mbele ya Ar-Rubayyi’ yavunjwe, haiwezekani! Naapa kwa Alyekutuma kwa haki meno yake hayatavunjwa. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Ee Anas Kitabu cha Allaah ni kulipa kisasi.” Watu wakaridhia wakamsamehe. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Hakika miongoni mwa waja wa Allaah kuna ambao lau atamuapia Allaah (kwa jambo) Anamfanyia.”[17] [Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Al-Bukhaariy]

 

 

 

1003.

وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ  صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {مَنْ قُتِلَ فِي عِمِّيَّا أَوْ رِمِّيَّا بِحَجَرٍ، أَوْ سَوْطٍ، أَوْ عَصًا، فَعَلَيْهِ عَقْلُ اَلْخَطَإِ، وَمِنْ قُتِلَ عَمْدًا فَهُوَ قَوَدٌ، وَمَنْ حَالَ دُونَهُ فَعَلَيْهِ لَعْنَةُ اَللَّهِ} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ، وَابْنُ مَاجَهْ، بِإِسْنَادٍ قَوِيٍّ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kuuwawa kwa (‘Immiyyan)[18] au kwa kurushiwa jiwe, mjeledi au fimbo, basi diya yake ni diya ya kuuwawa kimakosa. Na mwenye kuuwawa kwa makusudi atalipiziwa kisasi. Atakayeweka pingamizi baina ya hayo yaliyotajwa na baina ya msimamizi wa aliyeuwawa basi laana ya Allaah Iwe juu yake.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy na Ibn Maajah kwa isnaad ya nguvu]

 

 

 

1004.

وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، عَنْ اَلنَّبِيِّ  صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَ: {إِذَا أَمْسَكَ اَلرَّجُلُ اَلرَّجُلَ، وَقَتَلَهُ اَلْآخَرُ، يُقْتَلُ اَلَّذِي قَتَلَ، وَيُحْبَسُ اَلَّذِي أَمْسَكَ} رَوَاهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ مَوْصُولًا وَمُرْسَلًا، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ اَلْقَطَّانِ، وَرِجَالُهُ ثِقَاتٌ، إِلَّا أَنَّ اَلْبَيْهَقِيَّ رَجَّحَ اَلْمُرْسَلَ

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mtu atakapomzuia mtu, na mtu mwingine akamuuwa, aliyeuwa atauwawa na yule aliyemzuia[19] atafungwa.” [Imetolewa na Ad-Daaraqutwniy ikiwa ni Mursal na akaisahihisha Ibn Al-Qatwaan, wapokezi wake ni madhubuti lakini Al-Bayhaqiyy ametilia nguvu kuwa ni Mursal]

 

 

 

1005.

وَعَنْ عَبْدِ اَلرَّحْمَنِ بْنِ الْبَيْلَمَانِيِّ، {أَنَّ اَلنَّبِيَّ  صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَتَلَ مُسْلِمًا بِمَعَاهِدٍ.‏ وَقَالَ: "أَنَا أَوْلَى مَنْ وَفَى بِذِمَّتِهِ}‏ أَخْرَجَهُ عَبْدُ اَلرَّزَّاقِ هَكَذَا مُرْسَلًا.‏ وَوَصَلَهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ، بِذِكْرِ اِبْنِ عُمَرَ فِيهِ، وَإِسْنَادُ اَلْمَوْصُولِ وَاهٍ

Kutoka kwa ‘Abdi Rahmaan bin Al-Baylamaaniy[20] amesema kuwa: Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuuwa Muislam kwa kumlipizia kafiri mwenye mkataba[21] na akasema: “Mimi ni aula wa kutekeleza dhima yake.” [Imetolewa na ‘Abdu Razzaaq ameipokea ikiwa ni Mursal. Ad-Daaraqutwniy amesema ni Mawsuwl kwa kutajwa Ibn ‘Umar ndani yake. Isnaad yake Mawsuwl ni dhaifu sana]

 

 

 

1006.

وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {قُتِلَ غُلَامٌ غِيلَةً، فَقَالَ عُمَرُ: لَوْ اِشْتَرَكَ فِيهِ أَهْلُ صَنْعَاءَ لَقَتَلْتُهُمْ بِهِ} أَخْرَجَهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: Kijana mmoja aliuwawa kwa kuviziwa,[22] ‘Umar akasema lau watu wa Swan’aa wangalishirikiana katika mauaji yake ningaliwauwa kwa sababu yake. [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

1007.

وَعَنْ أَبِي‏ شُرَيْحٍ اَلْخُزَاعِيِّ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ  صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {فَمَنْ قُتِلَ لَهُ قَتِيلٌ بَعْدَ مَقَالَتِي هَذِهِ، فَأَهْلُهُ بَيْنَ خِيَرَتَيْنِ: إِمَّا أَنْ يَأْخُذُوا اَلْعَقْلِ.‏ أَوْ يَقْتُلُوا} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ وَأَصْلُهُ فِي "اَلصَّحِيحَيْنِ" مِنْ حَدِيثِ أَبِي هُرَيْرَةَ بِمَعْنَاهُ

Kutoka kwa Abuu Shurayh Al-Khuzaa’iy[23] amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kuuawa mtu wake baada ya maneno yangu haya basi watu wake wako baina ya khiyari mbili: ima wachukue diya au nao waue.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy. Asili ya hadiyth hii iko katika sahihi mbili kutoka katika hadiyth ya Abuu Hurayrah kwa maana kama hiyo]

 

[1] Jinayaat ni wingi wa Jinaya yenye maana ya “Kumdhuru mtu kwa kumpa adhabu ya kiwiliwili.” Vyovyote iwavyo kama ni kwa bahati mbaya au kwa makusudi.

 

[2] Hairuhusiwi kumuua aliyetoa Shahaadah. Mzinifu aliyeoa, muuwaji, na aliyeritadi wanauliwa. Katika Hadiyth moja tunajifunza kuwa ni ruhusa kuuwa kwa kujilinda ikitokezea mtu kuja kwa niyyah ya kuuwa. Hili ni jambo la nne katika yanayoruhusiwa kwa aliyetoa Shahaadah. Neno nafsi kwa nafsi iliyotajwa kwa Hadiyth hii ni kuuwa kwa kulipiza kisasi.

 

[3] Hii inaonyesha kuwa kuuwa ni moja katika madhambi makubwa sana. Ni kanuni ya msingi kuwa jambo kubwa zaidi huwa linatangulizwa zaidi, na madamu ya kuwa mauwaji ni dhambi kubwa zaidi basi  na hukumu yake ndiyo itakayokuwa ya mwanzo siku ya Qiyaamah. Vivyo hivyo kwa kuwa majukumu ya watu kuswali hutangulizwa kuliko kingine chochote nacho ndicho kitakachoulizwa mwanzo hali kadhalika.

 

[4] ‘Ulamaa wamekubaliana kuwa mtumwa atakatwa kichwa chake kwa mauaji ya muungwana. Hata hivyo kuna rai tofauti ya ‘Ulamaa ikiwa naye muungwana atakatwa kichwa kwa kumuuwa mtumwa.

 

[5] ‘Ulamaa wengi wa mwanzo wamefuata rai ya kuwa ikiwa baba kamuuwa mwanawe, hawezi kuuliwa kwa kulipizwa kisasi cha mwanawe. Hata hivyo hawezi kukwepa adhabu inayomsubiri siku ya Qiyammaah. Sababu kubwa ya ubaguzi huu ni kuwa baba ndiye msingi na chanzo cha kuwepo kwa mtoto na sio kinyume chake na hivyo hawezi kuwa na haki ya kusitisha maisha ya baba yake.

 

[6] Al-Khatwaab amesema: “Makusudio ni kuwa zawadi haistahiki ila katika mashindno ya farasi, ngamia na mfano wa wanyama hao na kurusha mishale kwa sababu mambo haya ni maandalizi ya kupambana na adui na kutoa zawadi katika mashindano haya ni kuhimiza watu katika Jihaad.”

 

[7] Abuu Juhayfah aliuliza swali hili kwa sababu moja katika madhehebu ya Kishia linaamini kuwa pamoja na kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa ni Rasuli wa Allaah aliyekuwa akishushiwa Wahyi na familia yake vile vile walikuwa na sehemu ya wahyi uliokuwa ukiteremka kwao. Abuu Juhayfah alikua anataka muono huu ufutwe kutoka kwao.

 

[8] Hadiyth hii inajulisha kuwa Muislam hauliwi kwa kulipiza kisasi kwa kumuuwa kafiri. Ikiwa imethibitika kuwa kafiri yule anahusika na  nchi iliyo na vita na dola ya Kiislam basi hatouwawa kwa kuuwa kwake. Hii ni kwa mujibu wa kongamano la ‘Ulamaa. Ama ikithibitika kuwa aliyeuwawa ni dhimmi (kafiri anayeishi katika dola ya Kiislam na anayelipa kodi na ambaye yupo chini ya dola ya Kiislam), Maimaam watatu wana rai kuwa Muislam hatouwawa kwa mauaji haya ambapo Imaam wa nne Abuu Hanifa ana rai kuwa ni lazima auwawe.

[9] Hadiyth hii inathibitisha kuwa mtu huuliwa kwa kumuuwa mwanamke. Vivyo hivyo hakuna ubaguzi kwa misingi ya utajiri na umaskini wa mtu baina ya kijana na mtu mzima.

 

[10] Mtumwa alikata sikio la mtumwa. Sasa watu wakawa wana chaguo: Ni kisasi au kulipa diya. Bwana wa yule mtumwa hakutaka kisasi bali diya. Bwana wa yule mtumwa aliyetenda kosa hakuwa na uwezo wa kulipa na mtumwa mwenyewe hakuwa na uwezo wowote. Aliyeshtakia akawa hajapata chochote. Hii inamaanisha kuwa mwenye kuomba (maskini) hana jukumu la kulipa diya kwa yeyote na familia yake haishurutishwi kwa hilo vile vile. Kulipa fidia inakuwa ni wajibu kwa familia inayotarajia kurithi kutoka kwa mtu huyo. Madamu mtu mwenyewe hana cha kurithiwa, suala la kulipa fidia linakuwa halipo.

[11] Hadiyth hii inatujuvya kuwa mtu asipokee fidia yoyote na asubiri hadi atakapopona kabisa. Hikmah ya jambo hili ni kuthibitika kwa jeraha lenyewe kwa kupona au kutokupona. Suala la fidia litategemea hali atakayokuwa nayo aliyejuruhiwa.

[12] Ikiwa mtoto aliye tumboni alikufa kabla ya kuzaliwa fidiya yake itakuwa ni bei ya kijakazi au mtumwa. Ikiwa mtoto alikufa baada ya kuzaliwa, fidia itakayolipwa itakuwa ni sawa na ngamia mia moja. Mauaji ya kukusudia au mauaji ya bahati mbaya hayahitaji kisasi, bali fidiya tu. Jina la kiarabu ‘Aaqila inafasiriwa kama ni ‘Asaba (jamaa wa karibu) ina maana kuwa fidiya haiwajibiki kwa muuaji peke yake bali kwa jamaa zake wa karibu.

 

[13] Hamal bin Maalik bin An-Naabighat Al-Hudhaliy Abuu Nadla Al-Basri alikuwa ni Swahaba.

 

[14] Ni wingi wa kuhani, mpiga ramli.

[15] Ar-Rubayyi’ ni mtoto wa Nadhr bin Damdam bin Zaid bin Haram, alikuwa ni shangazi wa Anas bin Maalik, Swahaba mkubwa aliyekuwa mtumishi wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na alikuwa ni mama wa Haarith bin Suraaqa aliyekufa katika vita vya Badr.

 

[16] Alikuwa ni kaka yake Ar-Rubayyi’ na alikuwa ni ami yake Anas bin Maalik. Hakushiriki katika vita vya Badr na alikua akijutia hilo kila mara. Hivyo basi, katika siku ya vita vya Uhud, baadhi ya Waislam walipokimbia, alikuenda mstari wa mbele wa maadui mushirikina na kujutia hali ya Waislam na kusema kwa sauti: ”Nasikia harufu ya Jannah katika mlima wa Uhud” alipigana hadi akauwawa.

 

[17] Maneno haya aliyoyatoa Anas hayakuwa kupinga Shariy’ah ya Allaah. Alifanya kila jitihada lakini alikuwa na Iymaan kubwa na huruma ya Allaah. Kama ingalikuwa vinginevyo basi Rasuli wa Allaah asingemsifu bali angesema kinyume chake. Hadiyth hii inaeleza kuwa kisasi kinachukuliwa hata kwa kutolewa jino la mtu.

[18] ‘Immiyyan ni mtu kuuawa kwa kuchinjwa bila kujulikana muuaji wake au sababu zilizopelekea hilo kutofahamika. Vivyo hivyo, ikiwa mtu atauwawa katika vurugu, kisasi hakitahusika, kwa kuwa hukumu ihusikayo hapa ni Diya (fidiya ya fedha kwa mauaji). Ikiwa mtu amekufa kwa kupigwa na rungu, kupigwa mijeledi, au jiwe, aina hiyo ya mauaji inazingatiwa kuwa ni mauaji ya kukusudia ambayo inahitaji fidiya.

 

[19] Hadiyth hii inathibitisha kuwa mtu atakayemzuia mtu ili auwawe hauwawi bali atafungwa. Aina ya kifungo itatolewa na Qaadhw, inaweza kuwa ndefu au fupi kulingana na mazingira ya mauaji yenyewe.

[20] Huyu ni ‘Abdur-Rahmaan bin Abuu Zayd, muachwa huru wa ‘Umar bin Al-Khatwaab. Alikuwa ni mkazi wa Madiynah ambaye aliishi Haran. Alikuwa Taabi’i wa kizazi cha sita. Abuu Haatim anamuelezea: “Alikuwa ni dhaifu (katika mapokezi ya hadiyth)” Ibn Hibbaan anamtaja kuwa alikuwa madhubuti. Al Haafidh Abdul-‘Azim anasema kuhusiana naye: “Hakuwa katika watu wenye mamlaka kuhusu Hadiyth.”

 

[21] Neno la kiarabu lililotumika ni Mu’aahid ambalo lina maana ya kafiri ambaye hana makazi ya kudumu katika dola ya Kiislam na amekwenda katika dola hiyo kwa sababu maalumu baada ya kupata ruhusa kutoka katika dola hiyo. Mauaji ya mtu kama huyo kwa makubaliano ya kongomano la ‘Ulamaa ni haraam. Hata hivyo muuaji Muislam hatolipiziwa kisasi kulingana na ‘Ulamaa wote isipokuwa Abuu Haniyfah.

[22] Tukio lilikua ni watu watatu waliomuuwa kijana mmoja kwa pamoja na kwa kumvizia. ‘Umar alitoa hukmu ya kuuwawa kwa wote. Kuna rai tofauti kama inafaa kwa watu wengi waliomuua mtu mmoja kwa kuuwawa wote. Kauli yenye nguvu ni ile hukumu ya ‘Umar.

 

[23] Huyu ni ‘Amr bin Khuwaylid bin ‘Amr Al-Kabi Al-‘Adawi Al-Khuzaa’iy alisilimu baada ya Fat-h ya Makkah na alifariki Madiynah katika mwaka wa 68 Hijriyyah.

Share