36-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Allaah Hakuwaadhibu Au Kuwaangamiza Makafari Kwa Sababu Ya Uwepo Wakee

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

36-Allaah Hakuwaadhibu Au Kuwaangamiza Makafari Kwa Sababu Ya Kuweko Kwake

 

www.alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

  وَإِذْ قَالُوا اللَّـهُمَّ إِن كَانَ هَـٰذَا هُوَ الْحَقَّ مِنْ عِندِكَ فَأَمْطِرْ عَلَيْنَا حِجَارَةً مِّنَ السَّمَاءِ أَوِ ائْتِنَا بِعَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٣٢﴾

Na pindi waliposema: “Ee Allaah! Kama haya ni haki kutoka Kwako; basi Tunyeshee mvua ya mawe kutoka mbinguni, au Tuletee adhabu iumizayo.”

 

وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُعَذِّبَهُمْ وَأَنتَ فِيهِمْ ۚ وَمَا كَانَ اللَّـهُ مُعَذِّبَهُمْ وَهُمْ يَسْتَغْفِرُونَ﴿٣٣﴾

Na Allaah Hakuwa wa kuwaadhibu na hali wewe (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uko nao. Na Allaah Hakuwa wa kuwaadhibu hali wao wanaomba maghfirah. [Al-Anfaal: 32- 33]

 

Imaam As-Sa’diy  (رحمه الله)  amesema:  “Kutokana na kauli yao hiyo (ya Aayah 32 ya kuomba adhabu) ni dhahiri kuwa wao ni wajinga wapumbavu, madhalimu. Lau kama Allaah Angewaharakazia adhabu basi wasingebakia kuishi. Lakini Allaah Amewakinga na adhabu kwa sababu ya uwepo wa Rasuli miongoni mwao. Basi uwepo wa Rasuli ni amani kwao kutokana na adhabu.”

 

Share