43-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Iymaan Hazitimii Bila Ya Kufuata Na Kutekeleza Hukmu Yake (صلى الله عليه وآله وسلم)

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

43-Iymaan Hazitimii Bila Ya Kufuata Na Kutekeleza

Hukmu Yake (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

 فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ﴿٦٥﴾

Basi Naapa kwa Rabb wako, hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni mwamuzi katika yale wanayozozana baina yao, kisha wasipate katika nyoyo zao karaha katika yale uliyohukumu na wajisalimishe, kwa kujisalimisha kikamilifu. [An-Nisaa: 65]

 

 

Kisa cha Maswahaba kilichosababisha kuteremshwa Aayah hiyo tukufu:

 

عَنْ عُرْوَةَ بْنِ الزُّبَيْرِ، أَنَّ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ الزُّبَيْرِ، حَدَّثَهُ أَنَّ رَجُلاً مِنَ الأَنْصَارِ خَاصَمَ الزُّبَيْرَ عِنْدَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِي شِرَاجِ الْحَرَّةِ الَّتِي يَسْقُونَ بِهَا النَّخْلَ، فَقَالَ الأَنْصَارِيُّ: سَرِّحِ الْمَاءَ‏ يَمُرُّ، فَأَبَى عَلَيْهِمْ، فَاخْتَصَمُوا عِنْدَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم لِلزُّبَيْرِ: ‏"‏ اسْقِ يَا زُبَيْرُ ثُمَّ أَرْسِلِ الْمَاءَ إِلَى جَارِكَ ‏"‏ ‏.‏ فَغَضِبَ الأَنْصَارِيُّ فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَنْ كَانَ ابْنَ عَمَّتِكَ، فَتَلَوَّنَ وَجْهُ نَبِيِّ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ثُمَّ قَالَ: ‏"‏ يَا زُبَيْرُ اسْقِ ثُمَّ احْبِسِ الْمَاءَ حَتَّى يَرْجِعَ إِلَى الْجَدْرِ ‏"‏ ‏.‏ فَقَالَ الزُّبَيْرُ: وَاللَّهِ إِنِّي لأَحْسِبُ هَذِهِ الآيَةَ نَزَلَتْ فِي ذَلِكَ:‏ فَلاَ وَرَبِّكَ لاَ يُؤْمِنُونَ حَتَّى يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لاَ يَجِدُوا فِي أَنْفُسِهِمْ حَرَجًا

‘Urwa bin Zubayr (رضي الله عنه)  amehadithia kwamba ‘Abdullaah bin Zubayr alimhadithia kwamba, bwana mmoja katika Answaar, alikhitilafiana naye mbele ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu maeneo ya kumwagia maji ya Harra ambayo wanamwagilia maji mitende yao. Answaari akasema: “Acha maji yatiririke.” Lakini (Zubayr) alikataa kufanya hivyo na gomvi likaletwa kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) naye akamwambia Zubayr: “Ee Zubayr, mwagilia maji (mitende yako) na acha maji yatiririke kwa jirani yako.”  Answaari akaghadhibika na kusema: “Ee Rasuli wa Allaah! (umetoha hukmu hiyo) kwa kuwa ni bin wa ammat (Shangazi) yako?”  Hapo uso wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ukabadilika rangi (kwa ghadhabu). Basi hapo akasema: “Ee Zubayr mwagilia maji (mitende yako) kisha izuie hadi ipande juu katika kuta.” Zubayr akasema: “Wa-Allaahi, nadhani kuwa Aayah hii imeteremka kwa ajili hiyo.”

 

 فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ﴿٦٥﴾

Basi Naapa kwa Rabb wako, hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni mwamuzi katika yale wanayozozana baina yao, kisha wasipate katika nyoyo zao karaha katika yale uliyohukumu na wajisalimishe, kwa kujisalimisha kikamilifu. [An-Nisaa: 65 - Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Share