012-Asbaabun-Nuzuwl: Yuwsuf Aayah 1-3: نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ أَحْسَنَ الْقَصَص

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

012-Suwrah Yuwsuf Aayah 1-3

Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى):

الر ۚ تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْمُبِينِ ﴿١﴾

Alif Laam Raa. Hizo ni Aayaat za Kitabu kinachobainisha.

إِنَّا أَنزَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لَّعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿٢﴾

Hakika Sisi Tumeiteremsha Qur-aan kwa (lugha ya) Kiarabu ili muifahamu.

نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ أَحْسَنَ الْقَصَصِ بِمَا أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ هَـٰذَا الْقُرْآنَ وَإِن كُنتَ مِن قَبْلِهِ لَمِنَ الْغَافِلِينَ ﴿٣﴾

Sisi Tunakusimulia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) simulizi nzuri kabisa katika Tuliyokufunulia Wahy hii Qur-aan. Na japokuwa kabla yake ulikuwa miongoni mwa wasiojua. [Yuwsuf: 1-3]

Sababun-Nuzuwl: 

 عن مصعب بن سعد عن أبيه سعد بن أبي وقاص في قول الله عز وجل: ((نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ أَحْسَنَ الْقَصَصِ)) الآية. قال: أنزل الله القرآن على رسول الله صلى الله عليه وعلى آله وسلم فتلاه عليهم زمانا، فقالوا: يا رسول الله لو قصصت علينا فأنزل الله ((الر تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْمُبِينِ)) إلى قوله ((نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ أَحْسَنَ الْقَصَصِ)) الآية. فتلاها رسول الله صلى الله عليه وعلى آله وسلم زمانا، فقالوا: يا رسول الله لو حدثتنا فأنزل الله تعالى ((اللَّهُ نَزَّلَ أَحْسَنَ الْحَدِيثِ كِتَابًا مُتَشَابِهًا))  أخرجه ابن حبان في صحيحه  والحاكم  وقال صحيح الإسناد  

Kutoka kwa Musw-‘ab  kutoka kwa baba yake Sa’ad bin Abiy Waqqaasw kuhusu kauli ya Allaah (عز وجل):

نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ أَحْسَنَ الْقَصَصِ بِمَا أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ هَـٰذَا الْقُرْآنَ وَإِن كُنتَ مِن قَبْلِهِ لَمِنَ الْغَافِلِينَ ﴿٣﴾

Sisi Tunakusimulia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) simulizi nzuri kabisa katika Tuliyokufunulia Wahy hii Qur-aan. Na japokuwa kabla yake ulikuwa miongoni mwa wasiojua

Kwamba Qur-aan imeteremshwa kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akawasomea kwa kipindi kirefu. Kisha watu (wakatamani ziyada) wakasema: Ee Rasuli wa Allaah, ungelitusimulia: Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha:

الر ۚ تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْمُبِينِ ﴿١﴾

Alif Laam Raa. Hizo ni Aayaat za Kitabu kinachobainisha.

mpaka Kauli Yake:

نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ أَحْسَنَ الْقَصَصِ بِمَا أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ هَـٰذَا الْقُرْآنَ وَإِن كُنتَ مِن قَبْلِهِ لَمِنَ الْغَافِلِينَ ﴿٣﴾

Sisi Tunakusimulia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) simulizi nzuri kabisa katika Tuliyokufunulia Wahy hii Qur-aan. Na japokuwa kabla yake ulikuwa miongoni mwa wasiojua

Akawasomea kwa muda mrefu lakini (Swahaba wakatamani ziyada) wakasema: Ee Rasuli wa Allaah laiti ungelituhadithia (tena mengineyo): Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha:

اللَّـهُ نَزَّلَ أَحْسَنَ الْحَدِيثِ كِتَابًا مُّتَشَابِهًا مَّثَانِيَ تَقْشَعِرُّ مِنْهُ جُلُودُ الَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُمْ ثُمَّ تَلِينُ جُلُودُهُمْ وَقُلُوبُهُمْ إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكَ هُدَى اللَّـهِ يَهْدِي بِهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَمَا لَهُ مِنْ هَادٍ ﴿٢٣﴾

Allaah Ameteremsha kauli nzuri kabisa, Kitabu; zinazoshabihiana ibara zake, zenye kukaririwa kila mara, zinasisimua kwazo ngozi za wale wanaomkhofu Rabb wao, kisha zinalainisha ngozi zao na nyoyo zao katika kumdhukuru Allaah. Huo ndio mwongozo wa Allaah Humwongoza kwao Amtakaye. Na ambaye Allaah Amempotoa basi hana wa kumuongoa. [Az-Zumar: 23]

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “(Wametakabaliwa kama walivyotaka)Yote haya kwa ajili kuwafanya waamini Quraan.” [Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake, Al-Haakim akasema Isnaad yake Swahiyh]

Share