Skip to main content

017-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Israa 110-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Israa Aayah 110: قُلِ ادْعُوا اللَّـهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَـٰنَ ۖ أَيًّا مَّا تَدْعُوا فَلَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ وَلَا تَجْهَرْ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتْ بِهَا وَابْتَغِ بَيْنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

017-Asbaab Nuzuwl Suwrah al-Israa Aayah 110

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

قُلِ ادْعُوا اللَّـهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَـٰنَ ۖ أَيًّا مَّا تَدْعُوا فَلَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ وَلَا تَجْهَرْ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتْ بِهَا وَابْتَغِ بَيْنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا ﴿١١٠﴾

Sema; Muiteni Allaah au muiteni Ar-Rahmaan, vyovyote mtakavyomwita basi Yeye Ana Majina Mazuri kabisa. Na wala usisome kwa jahara Swalaah yako na wala usiifiche kimya kimya, bali shika njia ya wastani baina yake. [Al-Israa: 110]

Sababun-Nuzuwl: 

حَدَّثَنَا مُسَدَّدٌ، عَنْ هُشَيْمٍ، عَنْ أَبِي بِشْرٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ ـ رضى الله عنهما ((‏وَلاَ تَجْهَرْ بِصَلاَتِكَ وَلاَ تُخَافِتْ بِهَا‏))‏ قَالَ أُنْزِلَتْ وَرَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم مُتَوَارٍ بِمَكَّةَ، فَكَانَ إِذَا رَفَعَ صَوْتَهُ سَمِعَ الْمُشْرِكُونَ فَسَبُّوا الْقُرْآنَ وَمَنْ أَنْزَلَهُ وَمَنْ جَاءَ بِهِ‏.‏ وَقَالَ اللَّهُ تَعَالَى: ((‏وَلاَ تَجْهَرْ بِصَلاَتِكَ وَلاَ تُخَافِتْ بِهَا‏))‏ لاَ تَجْهَرْ بِصَلاَتِكَ حَتَّى يَسْمَعَ الْمُشْرِكُونَ، وَلاَ تُخَافِتْ بِهَا عَنْ أَصْحَابِكَ فَلاَ تُسْمِعُهُمْ: ((‏وَابْتَغِ بَيْنَ ذَلِكَ سَبِيلاً‏))‏ أَسْمِعْهُمْ وَلاَ تَجْهَرْ حَتَّى يَأْخُذُوا عَنْكَ الْقُرْآنَ‏.‏  البخاري

Ametuhadithia Musaddad kutoka kwa Hushaym kutoka kwa Abuu Bishr, kutoka kwa Sa’iyd bin Jubayr kutoka kwa Ibn ‘Abaas (رضي الله عنهما) kuhusu Kauli ya Allaah (عز وجل):

وَلَا تَجْهَرْ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتْ بِهَا

Na wala usisome kwa jahara Swalaah yako na wala usiifiche kimya kimya…

Amesema: “Aayah hii iliteremshwa ilhali Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amejificha Makkah. Alikuwa akiipandisha sauti yake katika kusoma Qur-aan, walipomsikia washirikina, wakaitukana Qur-aan na wakamtukana Aliyeiteremsha na aliyeileta. Basi Allaah (عز وجل) Akasema:

وَلَا تَجْهَرْ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتْ بِهَا

Na wala usisome kwa jahara Swalaah yako na wala usiifiche kimya kimya…

Yaani: Usiisome kwa sauti kubwa hadi kwamba washirikiana wakusikie (kisha waitukane). 

وَلَا تُخَافِتْ بِهَا  

na wala usiifiche kimya kimya

Yaani: Usiisome kimya kimya hadi kwamba Swahaba zako wasiisikie unapowasomea washindwe kujifunza kwayo,

وَابْتَغِ بَيْنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا  

bali shika njia ya wastani baina yake.

Yaani: Wasikilizishe (Swahaba) kiasi cha kuisikia kwao.

[Al-Bukhaariy Kitaab At-Tawhiyd]  

Pia,

عَنْ عَائِشَةَ ـ رضى الله عنها ـ قَالَتْ نَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ ‏‏وَلاَ تَجْهَرْ بِصَلاَتِكَ وَلاَ تُخَافِتْ بِهَا‏‏ فِي الدُّعَاءِ‏.‏ 

Kutoka kwa ‘Aaishah (رضي الله عنها) kwamba Iliteremka Aayah hii:

وَلَا تَجْهَرْ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتْ بِهَا  

Na wala usisome kwa jahara Swalaah yako na wala usiifiche kimya kimya...

Kasema: “Inahusiana na Du’aa.”

[Al-Bukhaariy - Kitaab At-Tawhiyd, Kitaab At-Tafsiyr, na Muslim – Kitaab Asw-Swalaah]

Pia:

Sifa hii ya Rahmah ni ya dhati Yake Allaah ambayo haiwezi kutoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى). Makafiri wa Makkah hawakupenda Sifa na Jina hili la Ar-Rahmaan. Basi wakakataa kuliandika katika mkataba wa Hudaybiyah, pale Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipomuamrisha mwandishi wa mkataba andike “BismiLLaah (Kwa Jina la Allaah) Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rehma) Ar-Rahiym (Mwenye kurehemu).” Wakasema: “Andika: Biismika-Allaahumma.”  Hapo Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha:

قُلِ ادْعُوا اللَّـهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَـٰنَ ۖ أَيًّا مَّا تَدْعُوا فَلَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ  

“Sema: Muiteni Allaah au muiteni Ar-Rahmaan, vyovyote mtakavyomwita basi Yeye Ana Majina Mazuri kabisa.”  [Al-Israa: 110]

[Tafsiyr Ibn Kathiyr]