024-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nuwr Aayah 06-09: وَالَّذِينَ يَرْمُونَ أَزْوَاجَهُمْ وَلَمْ يَكُن لَّهُمْ شُهَدَاءُ إِلَّا أَنفُسُهُمْ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

24-Suwrah An-Nuwr Aayah 6 - 9

Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى):

وَالَّذِينَ يَرْمُونَ أَزْوَاجَهُمْ وَلَمْ يَكُن لَّهُمْ شُهَدَاءُ إِلَّا أَنفُسُهُمْ فَشَهَادَةُ أَحَدِهِمْ أَرْبَعُ شَهَادَاتٍ بِاللَّـهِ ۙ إِنَّهُ لَمِنَ الصَّادِقِينَ ﴿٦﴾

Na wale wanaowasingizia wake zao na hawana mashahidi isipokuwa nafsi zao, basi ushahidi wa mmoja wao utakuwa ni kushuhudia mara nne kwa kiapo cha Allaah kwamba yeye ni miongoni mwa wakweli.

وَالْخَامِسَةُ أَنَّ لَعْنَتَ اللَّـهِ عَلَيْهِ إِن كَانَ مِنَ الْكَاذِبِينَ ﴿٧﴾

Na (kiapo) cha tano kwamba laana ya Allaah iwe juu yake, akiwa ni miongoni mwa waongo.

وَيَدْرَأُ عَنْهَا الْعَذَابَ أَن تَشْهَدَ أَرْبَعَ شَهَادَاتٍ بِاللَّـهِ ۙ إِنَّهُ لَمِنَ الْكَاذِبِينَ ﴿٨﴾

Na itamwondokea (mke) adhabu atakapotoa ushahidi mara nne kwa kiapo cha Allaah kwamba yeye (mumewe) ni miongoni mwa waongo.

وَالْخَامِسَةَ أَنَّ غَضَبَ اللَّـهِ عَلَيْهَا إِن كَانَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿٩﴾

Na (kiapo) cha tano kwamba ghadhabu ya Allaah iwe juu yake akiwa (mumewe) ni miongoni mwa wakweli. [An-Nuwr: 6 – 9]

Sababun-Nuzuwl:

حَدَّثَنِي مُحَمَّدُ بْنُ بَشَّارٍ، حَدَّثَنَا ابْنُ أَبِي عَدِيٍّ، عَنْ هِشَامِ بْنِ حَسَّانَ، حَدَّثَنَا عِكْرِمَةُ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، أَنَّ هِلاَلَ بْنَ أُمَيَّةَ، قَذَفَ امْرَأَتَهُ عِنْدَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم بِشَرِيكِ بْنِ سَحْمَاءَ، فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ الْبَيِّنَةَ أَوْ حَدٌّ فِي ظَهْرِكَ ‏"‏‏.‏ فَقَالَ يَا رَسُولَ اللَّهِ إِذَا رَأَى أَحَدُنَا عَلَى امْرَأَتِهِ رَجُلاً يَنْطَلِقُ يَلْتَمِسُ الْبَيِّنَةَ‏.‏ فَجَعَلَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ ‏"‏ الْبَيِّنَةَ وَإِلاَّ حَدٌّ فِي ظَهْرِكَ ‏"‏ فَقَالَ هِلاَلٌ وَالَّذِي بَعَثَكَ بِالْحَقِّ إِنِّي لَصَادِقٌ، فَلَيُنْزِلَنَّ اللَّهُ مَا يُبَرِّئُ ظَهْرِي مِنَ الْحَدِّ، فَنَزَلَ جِبْرِيلُ، وَأَنْزَلَ عَلَيْهِ ‏ وَالَّذِينَ يَرْمُونَ أَزْوَاجَهُمْ‏  فَقَرَأَ حَتَّى بَلَغَ ‏ ‏إِنْ كَانَ مِنَ الصَّادِقِينَ‏ فَانْصَرَفَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فَأَرْسَلَ إِلَيْهَا فَجَاءَ هِلاَلٌ، فَشَهِدَ، وَالنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ ‏"‏ إِنَّ اللَّهَ يَعْلَمُ أَنَّ أَحَدَكُمَا كَاذِبٌ فَهَلْ مِنْكُمَا تَائِبٌ ‏"‏‏.‏ ثُمَّ قَامَتْ فَشَهِدَتْ فَلَمَّا كَانَتْ عِنْدَ الْخَامِسَةِ وَقَّفُوهَا، وَقَالُوا إِنَّهَا مُوجِبَةٌ‏.‏ قَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ فَتَلَكَّأَتْ وَنَكَصَتْ حَتَّى ظَنَنَّا أَنَّهَا تَرْجِعُ ثُمَّ قَالَتْ لاَ أَفْضَحُ قَوْمِي سَائِرَ الْيَوْمِ، فَمَضَتْ‏.‏ فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ أَبْصِرُوهَا فَإِنْ جَاءَتْ بِهِ أَكْحَلَ الْعَيْنَيْنِ سَابِغَ الأَلْيَتَيْنِ خَدَلَّجَ السَّاقَيْنِ، فَهْوَ لِشَرِيكِ بْنِ سَحْمَاءَ ‏"‏‏.‏ فَجَاءَتْ بِهِ كَذَلِكَ، فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ لَوْلاَ مَا مَضَى مِنْ كِتَابِ اللَّهِ لَكَانَ لِي وَلَهَا شَأْنٌ ‏"‏‏

Amenihadithia Muhammad bin Bashshaar, ametuhadithia Ibn Abiy ‘Adiyy kutoka kwa Hishaam bin Hassaan, ametuhadithia ‘Ikrimah, kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  kuwa Hilaal bin Umayyah  alimshutumu mkewe (kuwa amezini) na Shariyk bin Sahmaa. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimwambia (Hilaal): “Lete ubainifu (mashahidi wanne) au hadd (adhabu iliyowekwa na Shariy’ah ya viboko) mgongoni mwako”. Hilaal akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Mmoja wetu anapomuona mwanamme juu ya mkewe atoke kwenda kutafuta mashahidi? Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaendelea kumwambia, “Ima ulete ubainifu (wa mashahidi wanne) au hadd mgongoni mwako”. Hapo, Hilaal  akasema: “Naapa kwa Yule Aliyekutuma kwa haki, hakika mimi ni mkweli na Allaah Atateremsha kitakacho usalimisha mgongo wangu na hadd”. Jibriyl akateremka na kumteremshia:

وَالَّذِينَ يَرْمُونَ أَزْوَاجَهُمْ وَلَمْ يَكُن لَّهُمْ شُهَدَاءُ إِلَّا أَنفُسُهُمْ فَشَهَادَةُ أَحَدِهِمْ أَرْبَعُ شَهَادَاتٍ بِاللَّـهِ ۙ إِنَّهُ لَمِنَ الصَّادِقِينَ ﴿٦﴾

Na wale wanaowasingizia wake zao na hawana mashahidi isipokuwa nafsi zao, basi ushahidi wa mmoja wao utakuwa ni kushuhudia mara nne kwa kiapo cha Allaah kwamba yeye ni miongoni mwa wakweli.

وَالْخَامِسَةُ أَنَّ لَعْنَتَ اللَّـهِ عَلَيْهِ إِن كَانَ مِنَ الْكَاذِبِينَ ﴿٧﴾

Na (kiapo) cha tano kwamba laana ya Allaah iwe juu yake, akiwa ni miongoni mwa waongo.

وَيَدْرَأُ عَنْهَا الْعَذَابَ أَن تَشْهَدَ أَرْبَعَ شَهَادَاتٍ بِاللَّـهِ ۙ إِنَّهُ لَمِنَ الْكَاذِبِينَ ﴿٨﴾

Na itamwondokea (mke) adhabu atakapotoa ushahidi mara nne kwa kiapo cha Allaah kwamba yeye (mumewe) ni miongoni mwa waongo.

وَالْخَامِسَةَ أَنَّ غَضَبَ اللَّـهِ عَلَيْهَا إِن كَانَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿٩﴾

Na (kiapo) cha tano kwamba ghadhabu ya Allaah iwe juu yake akiwa (mumewe) ni miongoni mwa wakweli. [An-Nuwr: 6 – 9]

Akaondoka Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  akatuma aletwe mke, naye Hilaal alikwenda na kumleta na kisha akala kiapo (kuthibitisha madai yake). Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  alikuwa anasema: “Allaah Anajua kuwa mmoja wenu ni muongo, kwa hiyo yupo kati yenu atakaye tubu?” Kisha mwanamke akasimama kuchukua viapo na alipokuwa anataka kuchukua cha tano, watu walimsimamisha, wakasema: “Hakika hicho (kiapo cha tano) ni wajibu (bila shaka kitaleta laana ya Allaah ikiwa una hatia)”. Ibn ‘Abbaas akasema: “Alisita na kurudi nyuma (kuchukua kiapo) mpaka tukadhania kuwa ataachilia mbali kukata kwake (kwa kukiri kosa). Kisha akasema, ‘Sitawafedhi (sitawatia aibu) kaumu yangu siku zote hizi’, na akaendelea (katika mfumo wa kula kiapo)”. Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  akasema: “Mtizameni; ikiwa atazaa mtoto wa macho meusi mwenye kiuno kipana na miundi minene, basi atakuwa ni mtoto wa Shariyk bin Sahma”. Baadaye alizaa mtoto kama alivyoelezea. Akasema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  “Lau si kwa hukumu katika Kitabu cha Allaah, ningemuadhibu adhabu kali.” [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Tafsiyr]

Pia,

 حَدَّثَنَا إِسْحَاقُ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا الأَوْزَاعِيُّ، قَالَ حَدَّثَنِي الزُّهْرِيُّ، عَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ، أَنَّ عُوَيْمِرًا، أَتَى عَاصِمَ بْنَ عَدِيٍّ وَكَانَ سَيِّدَ بَنِي عَجْلاَنَ فَقَالَ كَيْفَ تَقُولُونَ فِي رَجُلٍ وَجَدَ مَعَ امْرَأَتِهِ رَجُلاً، أَيَقْتُلُهُ فَتَقْتُلُونَهُ أَمْ كَيْفَ يَصْنَعُ سَلْ لِي رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم عَنْ ذَلِكَ فَأَتَى عَاصِمٌ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ يَا رَسُولَ اللَّهِ، فَكَرِهَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم الْمَسَائِلَ، فَسَأَلَهُ عُوَيْمِرٌ فَقَالَ إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَرِهَ الْمَسَائِلَ وَعَابَهَا، قَالَ عُوَيْمِرٌ وَاللَّهِ لاَ أَنْتَهِي حَتَّى أَسْأَلَ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم عَنْ ذَلِكَ فَجَاءَ عُوَيْمِرٌ فَقَالَ يَا رَسُولَ اللَّهِ رَجُلٌ وَجَدَ مَعَ امْرَأَتِهِ رَجُلاً، أَيَقْتُلُهُ فَتَقْتُلُونَهُ أَمْ كَيْفَ يَصْنَعُ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ قَدْ أَنْزَلَ اللَّهُ الْقُرْآنَ فِيكَ وَفِي صَاحِبَتِكَ ‏"‏‏.‏ فَأَمَرَهُمَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم بِالْمُلاَعَنَةِ بِمَا سَمَّى اللَّهُ فِي كِتَابِهِ، فَلاَعَنَهَا ثُمَّ قَالَ يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنْ حَبَسْتُهَا فَقَدْ ظَلَمْتُهَا، فَطَلَّقَهَا، فَكَانَتْ سُنَّةً لِمَنْ كَانَ بَعْدَهُمَا فِي الْمُتَلاَعِنَيْنِ، ثُمَّ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ انْظُرُوا فَإِنْ جَاءَتْ بِهِ أَسْحَمَ أَدْعَجَ الْعَيْنَيْنِ عَظِيمَ الأَلْيَتَيْنِ خَدَلَّجَ السَّاقَيْنِ فَلاَ أَحْسِبُ عُوَيْمِرًا إِلاَّ قَدْ صَدَقَ عَلَيْهَا، وَإِنْ جَاءَتْ بِهِ أُحَيْمِرَ كَأَنَّهُ وَحَرَةٌ فَلاَ أَحْسِبُ عُوَيْمِرًا، إِلاَّ قَدْ كَذَبَ عَلَيْهَا ‏"‏‏.‏ فَجَاءَتْ بِهِ عَلَى النَّعْتِ الَّذِي نَعَتَ بِهِ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم مِنْ تَصْدِيقِ عُوَيْمِرٍ، فَكَانَ بَعْدُ يُنْسَبُ إِلَى أُمِّهِ‏.‏

Ametuhadithia Is-Haaq, ametuhadithia Muhammad bin Yuwsuf, ametuhadithia Al-Awzaaiy amesema, amenihadithia Az-Zuhriy toka kwa Sahl  bin Sa’ad kuwa ‘Uwaymir alimwendea ‘Aaswim bin ‘Adiyy ambaye alikuwa ni Mtemi (Chifu) wa Baniy ‘Ajlaan na kumuuliza: Mnasema nini kuhusu mtu aliyemfumania mkewe na mwanamume mwingine, je amuue mgoni, kisha nyinyi mumuue (mume kwa kisasi), au afanye vipi? Niulizie hukmu ya hilo kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). ‘Aaswim akamwendea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  na kumwambia: Ee Rasuli wa Allaah! (akamuuliza swali lile). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)   hakupendezewa na swali. [‘Aaswim akarudi na] ‘Uwaymir akamuuliza nini kakujibu Rasuli], akamwambia: Hakika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakupendezwa na swali na ameliona ni la utovu wa hishma. ‘Uwaymir akasema: Wa-Allaahi, sitonyamaza mpaka nimuulize  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu hukmu ya hilo. ‘Uwaymir akaenda kwa Rasuli na kumwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Mtu kamkuta mkewe na mwanaume, je amuue mgoni, halafu nyinyi mje mumuue [mume kwa kisasi], au afanye vipi? Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  akamwambia: ((Hakika Allaah Ameteremsha Aayaat kukuzungumzia wewe pamoja na mkeo)). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akawaamuru waapizane kwa kulaaniana kwa picha Aliyoielezea Allaah katika Kitabu Chake, na yeye [‘Uwaymir] akamuapiza mkewe kwa laana [kuthibitisha kuwa ni mkweli katika madai yake]. Kisha akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Kama nitabaki naye, basi hakika nitamnyanyasa na kumfanyia ukatili, kisha akamtaliki. Na kumtaliki mke kukawa ndio hukmu ya kisharia baada yao kwa wenye kuapizana. Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)   akasema: ((Angalieni! Ikiwa [mke wa ‘Uwaymir] atazaa mtoto mweusi ti, mwenye macho makubwa meusi yaliyodumbukia, mwenye makalio makubwa, na miundi iliyojaza, basi dhana yangu ni kuwa ‘Uwaymir atakuwa amesema kweli katika madai yake dhidi ya mkewe. Na kama atazaa mtoto mwekundu wekundu uliokoza mithili ya mjusi [waharah]”, basi dhana yangu ni kuwa ‘Uwaymir atakuwa amemsingizia mkewe uongo. Akamzaa kwa sifa zile zile alizozitaja Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) za kuthibitisha ukweli wa madai ya ‘Uwaymir. Na baada ya hapo akawa ananasibishwa kwa mama yake)).  [Al-Bukhaariy katika Mujallad wa Kumi ukurasa wa 64]

[Hadiyth hii imekharijiwa vile vile na Al-Bukhaariy katika Kitabu cha Talaka Mjeledi wa 11 kurasa za 282, 369 na 376, Pia Muslim katika Mujallad wa 10 kurasa za 120 na 123].
 
وأخرج البزار عن حذيفة رضي الله عنه قال رسول الله صلى الله عليه وعلى آله وسلم لأبي بكر: "لو رأيت مع أم رومان رجلا ما كنت فاعلا به؟" قال: كنت والله فاعلا به شرا. قال: "فأنت يا عمر" قال: كنت والله قاتله، كنت أقول لعن الله الأعجز. فإنه خبيث، فنزلت {وَالَّذِينَ يَرْمُونَ أَزْوَاجَهُمْ وَلَمْ يَكُنْ لَهُمْ شُهَدَاءُ إِلَّا أَنْفُسُهُمْ ...}
 
Al-Bazzaaz amekhariji toka kwa Hudhayfah (رضي الله عنه)  kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  alimuuliza Abu Bakr: “Hivi kama ungelimfumania Ummu Ruwmaan na mwanaume, nini ungelimfanya mtu huyo?” Akasema: “Ningelimfanya, Wa-Allaahi, jambo baya kabisa”. Akasema: “Na wewe ‘Umar?”. Akasema: “Mimi, Wa-Allaahi, ningelimuua. Ningelisema Allaah Amlaani mtu ajizi, kwani ni khabithi.” Na hapo ikateremka:

وَالَّذِينَ يَرْمُونَ أَزْوَاجَهُمْ وَلَمْ يَكُن لَّهُمْ شُهَدَاءُ إِلَّا أَنفُسُهُمْ فَشَهَادَةُ أَحَدِهِمْ أَرْبَعُ شَهَادَاتٍ بِاللَّـهِ ۙ إِنَّهُ لَمِنَ الصَّادِقِينَ ﴿٦﴾

Na wale wanaowasingizia wake zao na hawana mashahidi isipokuwa nafsi zao, basi ushahidi wa mmoja wao utakuwa ni kushuhudia mara nne kwa kiapo cha Allaah kwamba yeye ni miongoni mwa wakweli.

وَالْخَامِسَةُ أَنَّ لَعْنَتَ اللَّـهِ عَلَيْهِ إِن كَانَ مِنَ الْكَاذِبِينَ ﴿٧﴾

Na (kiapo) cha tano kwamba laana ya Allaah iwe juu yake, akiwa ni miongoni mwa waongo.

وَيَدْرَأُ عَنْهَا الْعَذَابَ أَن تَشْهَدَ أَرْبَعَ شَهَادَاتٍ بِاللَّـهِ ۙ إِنَّهُ لَمِنَ الْكَاذِبِينَ ﴿٨﴾

Na itamwondokea (mke) adhabu atakapotoa ushahidi mara nne kwa kiapo cha Allaah kwamba yeye (mumewe) ni miongoni mwa waongo.

وَالْخَامِسَةَ أَنَّ غَضَبَ اللَّـهِ عَلَيْهَا إِن كَانَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿٩﴾

Na (kiapo) cha tano kwamba ghadhabu ya Allaah iwe juu yake akiwa (mumewe) ni miongoni mwa wakweli. [An-Nuwr: 6 – 9]

[Al-Haythamiy amesema katika Majma’u Az Zawaaid Mujallad wa Saba ukurasa wa 74 kuwa wapokezi wake ni watu wa kuaminika]

(Rejeja Aayah Namba 01 hadi 10 Suwrah hiyo ya An-Nuwr kupata Aayah zinazohusiana na maudhui).

Share