024-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nuwr Aayah 34: وَلاَ تُكْرِهُوا فَتَيَاتِكُمْ عَلَى الْبِغَاءِ إِنْ أَرَدْنَ تَحَصُّنًا

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

024-Suwrah An-Nuwr Aayah 34

 

 

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَلْيَسْتَعْفِفِ الَّذِينَ لَا يَجِدُونَ نِكَاحًا حَتَّىٰ يُغْنِيَهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ ۗ وَالَّذِينَ يَبْتَغُونَ الْكِتَابَ مِمَّا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ فَكَاتِبُوهُمْ إِنْ عَلِمْتُمْ فِيهِمْ خَيْرًا ۖوَآتُوهُم مِّن مَّالِ اللَّـهِ الَّذِي آتَاكُمْ ۚ وَلَا تُكْرِهُوا فَتَيَاتِكُمْ عَلَى الْبِغَاءِ إِنْ أَرَدْنَ تَحَصُّنًا لِّتَبْتَغُوا عَرَضَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۚ وَمَن يُكْرِههُّنَّ فَإِنَّ اللَّـهَ مِن بَعْدِ إِكْرَاهِهِنَّ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣٣﴾

Na wajisitiri (yaliyoharamishwa) wale ambao hawapati uwezo wa ndoa mpaka Allaah Awatajirishe katika fadhila Zake. Na wale wanaotaka kuandikiwa kuachiwa huru katika wale ambao imemiliki mikono yenu ya kuume, basi waandikieni kama mkijua wema kwao. Na wapeni katika mali ya Allaah Aliyokupeni. Na wala msiwalazimishe vijakazi wenu kufanya ukahaba kama wakitaka kujisitiri, ili mtafute mafao ya uhai wa dunia. Na yeyote yule atakayewalazimisha, basi hakika Allaah, baada ya kulazimishwa kwao huko, ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.     [An Nuwr (24:31)]

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

 

حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرِ بْنُ أَبِي شَيْبَةَ، وَأَبُو كُرَيْبٍ جَمِيعًا عَنْ أَبِي مُعَاوِيَةَ، - وَاللَّفْظُ لأَبِي كُرَيْبٍ - حَدَّثَنَا أَبُو مُعَاوِيَةَ، حَدَّثَنَا الأَعْمَشُ، عَنْ أَبِي سُفْيَانَ، عَنْ جَابِرٍ، قَالَ كَانَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ أُبَىٍّ ابْنُ سَلُولَ يَقُولُ لِجَارِيَةٍ لَهُ اذْهَبِي فَابْغِينَا شَيْئًا فَأَنْزَلَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ:  ‏((‏وَلاَ تُكْرِهُوا فَتَيَاتِكُمْ عَلَى الْبِغَاءِ إِنْ أَرَدْنَ تَحَصُّنًا لِتَبْتَغُوا عَرَضَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَمَنْ يُكْرِهْهُنَّ فَإِنَّ اللَّـهَ مِن بَعْدِ إِكْرَاهِهِنَّ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣٣﴾

 

Ametuhadithia Abu Bakr bin Abiy Shaybah na Abu Kurayb, na wote wawili toka kwa Mu’aawiyah – na tamshi ni la Abu Kurayb – ametuhadithia Abu Mu’aawiyah, ametuhadithia Al-A’amash toka kwa Abu Sufyaan toka kwa Jaabir amesema: ‘Abdullaah bin Ubayya bin Saluwl alikuwa akimwambia kijakazi wake: Toka nenda ukajitembeze utuletee chochote. Na hapo Allaah (عز وجل) Akateremsha:

 

وَلاَ تُكْرِهُوا فَتَيَاتِكُمْ عَلَى الْبِغَاءِ إِنْ أَرَدْنَ تَحَصُّنًا لِتَبْتَغُوا عَرَضَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَمَنْ يُكْرِهْهُنَّ  فَإِنَّ اللَّـهَ مِن بَعْدِ إِكْرَاهِهِنَّ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣٣﴾

Na wala msiwalazimishe vijakazi wenu kufanya ukahaba kama wakitaka kujisitiri, ili mtafute mafao ya uhai wa dunia. Na yeyote yule atakayewalazimisha, basi hakika Allaah, baada ya kulazimishwa kwao huko [hao vijakazi], ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

[Muslim katika Mujallad wa 18 ukurasa wa 162]

 

Pia,

 

حَدَّثَنِي أَبُو كَامِلٍ الْجَحْدَرِيُّ، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنِ الأَعْمَشِ، عَنْ أَبِي سُفْيَانَ، عَنْ جَابِرٍ، أَنَّ جَارِيَةً، لِعَبْدِ اللَّهِ بْنِ أُبَىٍّ ابْنِ سَلُولَ يُقَالُ لَهَا مُسَيْكَةُ وَأُخْرَى يُقَالُ لَهَا أُمَيْمَةُ فَكَانَ يُكْرِهُهُمَا عَلَى الزِّنَى فَشَكَتَا ذَلِكَ إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَأَنْزَلَ اللَّهُ:  وَلاَ تُكْرِهُوا فَتَيَاتِكُمْ عَلَى الْبِغَاءِ إِنْ أَرَدْنَ تَحَصُّنًا لِتَبْتَغُوا عَرَضَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَمَنْ يُكْرِهْهُنَّ  فَإِنَّ اللَّـهَ مِن بَعْدِ إِكْرَاهِهِنَّ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣٣﴾

Ametuhadithia Abu Kaamil Al-Jahdariyy, ametuhadithia Abu ‘Awaanah kutoka kwa Al-A’amash toka kwa Abu Sufyaan, kutoka kwa Jaabir kwamba vijakazi wa  ‘Abdullaah bin Ubayya bin Saluwl mmojawapo aliyekuwa akiitwa Musaykah na mwenginewe akiitwa Umaymah, alikuwa akiwalazimisha wajiuze (kuzini), wakamshtakia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hapo Allaah Akateremsha:   

 

وَلَا تُكْرِهُوا فَتَيَاتِكُمْ عَلَى الْبِغَاءِ إِنْ أَرَدْنَ تَحَصُّنًا لِّتَبْتَغُوا عَرَضَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۚ وَمَن يُكْرِههُّنَّ فَإِنَّ اللَّـهَ مِن بَعْدِ إِكْرَاهِهِنَّ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣٣﴾

Na wala msiwalazimishe vijakazi wenu kufanya ukahaba kama wakitaka kujisitiri, ili mtafute mafao ya uhai wa dunia. Na yeyote yule atakayewalazimisha, basi hakika Allaah, baada ya kulazimishwa kwao huko, ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Muslim]

 

 

Na pia,

 

حَدَّثَنَا أَحْمَدُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ حَجَّاجٍ، عَنِ ابْنِ جُرَيْجٍ، قَالَ أَخْبَرَنِي أَبُو الزُّبَيْرِ، أَنَّهُ سَمِعَ جَابِرَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ، يَقُولُ جَاءَتْ مُسَيْكَةُ لِبَعْضِ الأَنْصَارِ فَقَالَتْ إِنَّ سَيِّدِي يُكْرِهُنِي عَلَى الْبِغَاءِ فَنَزَلَ فِي ذَلِكَ  (( وَلاَ تُكْرِهُوا فَتَيَاتِكُمْ عَلَى الْبِغَاءِ ))

Ametuhadithia Ahmad bin Ibraahiy, kutoka kwa Hajjaaj, kutoka kwa Ibn Jurayj amesema: Amenijulisha Abu Az-Zubayr kwamba kamsikia Jaabir bin ‘Abdillaah akisema: “Alikuja Musaykah (kijakazi cha ‘Abdullaah bin Ubayy bin Saluwl) kwa baadhi ya Answaari akasema: Bwana wangu ananilazimisha kuzini.” Ikateremshwa:

 

وَلَا تُكْرِهُوا فَتَيَاتِكُمْ عَلَى الْبِغَاءِ إِنْ أَرَدْنَ تَحَصُّنًا لِّتَبْتَغُوا عَرَضَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۚ وَمَن يُكْرِههُّنَّ فَإِنَّ اللَّـهَ مِن بَعْدِ إِكْرَاهِهِنَّ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣٣﴾

Na wala msiwalazimishe vijakazi wenu kufanya ukahaba kama wakitaka kujisitiri, ili mtafute mafao ya uhai wa dunia. Na yeyote yule atakayewalazimisha, basi hakika Allaah, baada ya kulazimishwa kwao huko, ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Abu Daawuwd katika Mujallad wa Pili ukurasa wa 264]

 

 

Na pia,

 

Ibn ‘Abbaas (Radhwiya-Allaahu ‘anhumaa) amesimulia akisema: “’Abdullaah bin Ubayya alikuwa na kijakazi anayemfanyia ukahaba wakati wa Ujahilia. Zinaa ilipoharamishwa alimkatalia kufanya hivyo na kumwambia: Wa-Allaahi, sitozini kamwe! Na hapo ikateremka Aayah:

 

وَلاَ تُكْرِهُوا فَتَيَاتِكُمْ عَلَى الْبِغَاءِ إِنْ أَرَدْنَ تَحَصُّنًا لِتَبْتَغُوا عَرَضَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَمَنْ يُكْرِهْهُنَّ  فَإِنَّ اللَّـهَ مِن بَعْدِ إِكْرَاهِهِنَّ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣٣﴾

 Na wala msiwalazimishe vijakazi wenu kufanya ukahaba kama wakitaka kujisitiri, ili mtafute mafao ya uhai wa dunia. Na yeyote yule atakayewalazimisha, basi hakika Allaah, baada ya kulazimishwa kwao huko [hao vijakazi], ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

[Majma’u Az Zawaaid Mujallad wa Saba ukurasa wa 82]

 

Imesimuliwa mfano wake na At-Twabaraaniy na Al-Bazzaar, na wapokezi wa At-Twabaraaniy ni wapokezi wa As-Swahiyh [Isnaad yao imekharijiwa na Al-Bukhaariy au Muslim]

  

 

 

Share