031-Asbaabun-Nuzuwl: Luqmaan Aayah 13: وَإِذْ قَالَ لُقْمَانُ لِابْنِهِ وَهُوَ يَعِظُهُ يَا بُنَيَّ لَا تُشْرِكْ بِاللَّـهِ ۖ إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

031-Asbaabun-Nuzuwl: Luqmaan Aayah 13

 

 

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَإِذْ قَالَ لُقْمَانُ لِابْنِهِ وَهُوَ يَعِظُهُ يَا بُنَيَّ لَا تُشْرِكْ بِاللَّـهِ ۖ إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ ﴿١٣﴾

Na Luqmaan alipomwambia mwanawe huku akimuwaidhi: Ee mwanangu! Usimshirikishe Allaah, hakika shirki ni dhulma kubwa mno! [Luqmaan (31:13)]

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

 حَدَّثَنَا أَبُو الْوَلِيدِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنِ الأَعْمَشِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عَلْقَمَةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ لَمَّا نَزَلَتِ: ((‏الَّذِينَ آمَنُوا وَلَمْ يَلْبِسُوا إِيمَانَهُمْ بِظُلْمٍ‏))‏ قَالَ أَصْحَابُ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم أَيُّنَا لَمْ يَلْبِسْ إِيمَانَهُ بِظُلْمٍ فَنَزَلَتْ: ((‏لاَ تُشْرِكْ بِاللَّهِ إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ ‏))

Ametuhadithia Abul Waliyd amesema, ametuhadithia Shu‘bah amesema, na amenihadithia Bishr amesema, ametuhadithia Muhammad toka kwa Shu’bah toka kwa Sulaymaan toka kwa Ibraahiym toka kwa ‘Al-Qamah toka kwa ‘Abdullaah amesema: Ilipoteremka:

 

الَّذِينَ آمَنُوا وَلَمْ يَلْبِسُوا إِيمَانَهُم بِظُلْمٍ أُولَـٰئِكَ لَهُمُ الْأَمْنُ وَهُم مُّهْتَدُونَ ﴿٨٢﴾

Wale walioamini na hawakuchanganya iymaan zao na dhulma; hao ndio watakaopata amani nao ndio waliohidika. [Al-An‘Aam (6:82)]..

 

Swahaba wa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) walimuuliza: Nani kati yetu ambaye hakuidhulumu nafsi yake? Hapo Allaah (‘Azza wa Jalla) Akateremsha:

 

  لَا تُشْرِكْ بِاللَّـهِ ۖ إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ ﴿١٣﴾

Usimshirikishe Allaah, hakika shirki ni dhulma kubwa mno! [Luqmaan (31:13)]

 

[Al-Bukhaariy katika Mujallad wa Kwanza ukurasa wa 95]

 

Ameikhariji vile vile kwenye Kitaabu At-Tafsiyr Mujallad wa Tisa ukurasa wa 363.

 

 

Angalizo:

 

Al-Haafidh katika Al Fat-h Mujallad wa Kwanza ukurasa wa 95 amesema: “Kwa muktadha wa Riwaayah hii ya Shu‘bah ni kuwa swali hili ndilo sababu ya kuteremka Aayah nyingine iliyoko katika Suwrat Luqmaan. Lakini Al-Bukhaariy na Muslim wameisimulia kwa Isnaad nyingine toka kwa Al-A‘amash ambaye ni Sulaymaan aliyetajwa katika Hadiyth hii. Katika Riwaayah ya Jariyr toka kwake, Swahaba wakauliza: “Ni nani kati yetu ambaye hakuchanganya iymaan yake na dhulma?” [Rasuli] akasema: “Si kwa hilo, je hamuisikii kauli ya Luqmaan?” Na katika riwaayah ya Wakiy’u toka kwake, akasema [Rasuli]: “Si kama mnavyodhania”. Na katika riwaayah ya ‘Iysaa bin Yuwnus: “Hakika hiyo ni shirki. Je hamkusikia aliyoyasema Luqmaan?” Na hii inaonyesha kuwa Aayah iliyoko kwenye Suwrah Luqmaan ilikuwa ikijulikana, na kwa ajili hiyo aliwazindushia. Pia inawezekana kuwa iliteremka hapo hapo akawasomea, kisha akawatanabahisha, na kwa hivyo Riwaayah mbili zinaoana.

 

 

 

Share