033-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Ahzaab Aayah 25: وَرَدَّ اللَّـهُ الَّذِينَ كَفَرُوا بِغَيْظِهِمْ لَمْ يَنَالُوا خَيْرًا ۚ وَكَفَى اللَّـهُ الْمُؤْمِنِينَ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

033-Asbaabun-Nuzuwl Al-Ahzaab Aayah 25

 

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَرَدَّ اللَّـهُ الَّذِينَ كَفَرُوا بِغَيْظِهِمْ لَمْ يَنَالُوا خَيْرًا ۚ وَكَفَى اللَّـهُ الْمُؤْمِنِينَ الْقِتَالَ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ قَوِيًّا عَزِيزًا ﴿٢٥﴾

Na Allaah Akawarudisha nyuma wale waliokufuru kwa ghaidhi zao hawakupata kheri yoyote. Na Allaah Amewatosheleza Waumini vitani. Na Allaah daima ni Mwenye nguvu zote, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika. [Al-Ahzaab (33:26)]

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَلِيٍّ، قَالَ حَدَّثَنَا يَحْيَى، قَالَ حَدَّثَنَا ابْنُ أَبِي ذِئْبٍ، قَالَ حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ أَبِي سَعِيدٍ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي سَعِيدٍ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ شَغَلَنَا الْمُشْرِكُونَ يَوْمَ الْخَنْدَقِ عَنْ صَلاَةِ الظُّهْرِ، حَتَّى غَرَبَتِ الشَّمْسُ وَذَلِكَ قَبْلَ أَنْ يَنْزِلَ فِي الْقِتَالِ مَا نَزَلَ فَأَنْزَلَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ ‏((‏وَكَفَى اللَّهُ الْمُؤْمِنِينَ الْقِتَالَ))‏ فَأَمَرَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم بِلاَلاً فَأَقَامَ لِصَلاَةِ الظُّهْرِ فَصَلاَّهَا كَمَا كَانَ يُصَلِّيهَا لِوَقْتِهَا ثُمَّ أَقَامَ لِلْعَصْرِ فَصَلاَّهَا كَمَا كَانَ يُصَلِّيهَا فِي وَقْتِهَا ثُمَّ أَذَّنَ لِلْمَغْرِبِ فَصَلاَّهَا كَمَا كَانَ يُصَلِّيهَا فِي وَقْتِهَا ‏.‏

 

Ametueleza ‘Amri bin ‘Aliy amesema, ametuhadithia Yahyaa amesema, ametuhadithia Ibn Ubayya Dhi-ib amesema, ametuhadithia Sa’iyd bin Abiy Sa’iyd toka kwa ‘Abdur-Rahmaan bin Abiy Sa’iyd toka kwa baba yake akisema: Washirikina walitushughulisha Siku ya Khandak tusiweze kuswali Swalaah ya Adhuhuri mpaka jua likachwa, na hiyo ilikuwa kabla ya Allaah (عز وجل)   kuteremsha (Aayah hii) kuhusiana na vita:

وَكَفَى اللَّـهُ الْمُؤْمِنِينَ الْقِتَالَ 

Na Allaah Amewatosheleza Waumini vitani.

 

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwamuru Bilaal (aqimu), akaqimu kwa Swalaah ya Adhuhuri, (Rasuli wa Allaah صلى الله عليه وآله وسلم)  akaiswali kama alivyokuwa anaiswali katika wakati wake. Kisha (Bilaal) akaqimu kwa Swalaah ya Al-‘Aswr, na (Rasuli wa Allaah صلى الله عليه وآله وسلم) akaiswali kama alivyokuwa anaiswali katika wakati wake. Halafu akaadhini kwa Swalaah ya Maghrib, na (Rasuli wa Allaah صلى الله عليه وآله وسلم) akaiswali kama alivyokuwa anaiswali katika wakati wake.”

 

[An-Nasaaiy katika Mujallad wa 2 Uk wa 15, Wapokezi wa Hadiyth hii ni wapokezi wa As-Swahiyh, na Ibn Jariyr ameikhariji katika Mujallad wa 21 ukurasa wa 149]

 

Share