Ndizi Mbivu

Ndizi Mbivu

 

Vipimo

Ndizi Mbivu - 6

Nazi - Kikopo 1

Sukari -Vijiko 3 vya chakula

Hiliki - Kijiko 1

Namna ya kutayarisha na kupika

  1. Menya ndizi kisha zipasue kati utoe ule moyo wa kati.
  2. Zikate size unayopenda mwenyewe, kisha uzipange ndani ya sufuria.
  3. Weka maji kiasi na uzichemshe ndizi kidogo, karibu ya kuiva mimina tui.
  4. Mimina sukari na hiliki ndani ya ndizi  na ziwache zichemke mpaka tui libaki kidogo.
  5. Ziondoe jikoni na uziweke kwenye sahani tayari kwa kuliwa.

Kidokezo:

Ni nzuri sana kuliwa na kitu cha chumvi kama nyama ya kukausha au kuku wa kuchoma.

 

Share