042-Asbaabun-Nuzuwl: Ash-Shuwraa Aayah 27: وَلَوْ بَسَطَ اللَّـهُ الرِّزْقَ لِعِبَادِهِ لَبَغَوْا فِي الْأَرْضِ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 042-Asbaabun-Nuzuwl Ash-Shuwraa Aayah 27

 

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَلَوْ بَسَطَ اللَّـهُ الرِّزْقَ لِعِبَادِهِ لَبَغَوْا فِي الْأَرْضِ وَلَـٰكِن يُنَزِّلُ بِقَدَرٍ مَّا يَشَاءُ ۚ إِنَّهُ بِعِبَادِهِ خَبِيرٌ بَصِيرٌ﴿٢٧﴾

Na lau kama Allaah Angelikunjua riziki kwa waja Wake, bila shaka wangefanya ufedhuli katika ardhi; lakini Anateremsha kwa kiasi Akitakacho. Hakika Yeye kwa waja Wake ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika, Mwenye kuona yote. [Ash-Shuwraa (42:27)]

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

أَخْبَرَنَا ابْن وَهْب   قَالَ : قَالَ أَبُو هَانِئ : سَمِعْت عَمْرو بْن حُرَيْث وَغَيْره يَقُولُونَ : إِنَّمَا أُنْزِلَتْ هَذِهِ الْآيَة فِي أَصْحَاب الصُّفَّة ((وَلَوْ بَسَطَ اللَّه الرِّزْق لِعِبَادِهِ لَبَغَوْا فِي الْأَرْض وَلَكِنْ يُنَزِّل بِقَدَرٍ مَا يَشَاء)) ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا : لَوْ أَنَّ لَنَا   فَتَمَنَّوْا

Ametueleza Ibn Wahab amesema: Amesema Abu Haaniy (naye ni Humayd bin Haaniy Al-Khawalaaniy): Nimemsikia ‘Amri bin Hurayth na wengineo wakisema: Hakika Aayah hii iliteremshwa kuwazungumzia Aswhaab As-Swuffah:

وَلَوْ بَسَطَ اللَّـهُ الرِّزْقَ لِعِبَادِهِ لَبَغَوْا فِي الْأَرْضِ

Na lau kama Allaah Angelikunjua riziki kwa waja Wake, bila shaka wangefanya ufedhuli katika ardhi. [Ash-Shuwraa (42:27)] Hiyo ni kwa vile wao walisema: Lau na sisi tungelikuwa navyo (walivyonavyo wengine), hivyo wakatamani.”

[Ibn Jariyr katika Mujallad wa 25 Uk. wa 30] 

 

 

Aswhaab Asw-Swuffah Ni: Swahaba masikini hohehahe wasio na makazi ambao walihamia Madiynah na kuhifadhiwa kwenye Msikiti wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). 

 

حَدَّثَنَا مُحَمَّد بْن سِنَان الْقَزَّاز  قَالَ : حدثنا أَبُو عَبْد الرَّحْمَن الْمُقْرِي  قَالَ : حدثنا حَيْوَة  قَالَ : أَخْبَرَنِي أَبُو هَانِئ  أَنَّهُ سَمِعَ عَمْرو بْن حُرَيْث يَقُول : إِنَّمَا نَزَلَتْ هَذِهِ الْآيَة

 

Ametuhadithia Muhammad bin Sinaan Al-Qazzaaz amesema: Ametuhadithia Abu ‘Abdur Rahmaan Al-Muqriy amesema: Ametuhadithia Haywah amesema: Amenieleza Abu Haaniy kuwa amemsikia ‘Amri bin Hurayth akisema: Hakika Aayah hii iliteremshwa, na akataja mnasaba wake.”

 

 

Al-Haythamiy amesema katika “Majma’ Az-Zawaaid” katika Mujallad wa 7 Uk. wa 104 kuwa imesimuliwa na At-Twabaraaniy, na Wapokezi wake ni Wapokezi wa As-Swahiyh. Hapo kuna tamshi: “Kwa kuwa wao waliitamani dunia.” Al-Waahidiy ameikhariji katika “Asbaab An-Nuzuwl”, na Abu Nu’aym ameikhariji katika “Al-Hilyat” Mujallad wa 1 Uk. wa 338.

 

Pia Al-Haakim ameikhariji na amesema ni Swahiyh. Adh-Dhahabiy ameashiria kuwa iko juu ya sharti ya Mashekhe Wawili katika Mujallad wa 2 Uk wa 445 toka kwa ‘Aliy bin Abiy Twaalib mfanowe.

 

 

Tanbihi:

‘Amri bin Hurayth amezozaniwa kuhusiana na Uswahaba wake kama ilivyoelezwa katika “Al-Iswaabah.”.

 

 

 

 

Share