083-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukataza Kumpatia Uongozi na Ukadhi na Nyadhifa Nyinginezo za Uongozi kwa Mwenye Kuomba Ama Kupupia

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب النهي عن تولية الإمارة والقضاء وغيرهما من الولايات لمن سألها أَوْ حرص عليها فعرَّض بها

083-Mlango Wa Kukataza Kumpatia Uongozi na Ukadhi na Nyadhifa Nyinginezo za Uongozi kwa Mwenye Kuomba Ama Kupupia

 

Alhidaaya.com

 

 

عن أَبي موسى الأشعريِّ رضي الله عنه ، قَالَ : دَخَلْتُ عَلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم أنَا وَرَجُلانِ مِنْ بَنِي عَمِّي ، فَقَالَ أحَدُهُمَا : يَا رسول الله ، أمِّرْنَا عَلَى بَعْض مَا ولاَّكَ اللهُ (عزّ وجلّ) ، وقال الآخَرُ مِثلَ ذَلِكَ ، فَقَالَ : ((  إنَّا وَاللهِ لاَ نُوَلِّي هَذَا العَمَلَ أحَداً سَألَهُ ، أَوْ أحَداً حَرَصَ عَلَيْهِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Muwsaa Al-Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nilienda kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nikiwa na watu wawili katika watoto wa ami zangu. Akasema mmoja wao: "Ee Rasuli wa Allaah! Tupe uongozi kwa baadhi ya aliyokutawalisha Allaah ('Azza wa Jalla)." Mwingine akasema mfano wake, Akasema: "Wa-Allaahi, sisi hatumpi kazi yeyote anayeomba au yeyote mwenye kuonyesha dalili ya kupupia." [Al-Bukhaariy, Muslim na An-Nasai].

 

 

 

Share