A-Majina Ya Swahaba: Maana, Wasifu Wao Kwa Mukhtasari: ‘Abdullaah Bin ‘Amr Ibn Al-‘Aasw

 

A-Majina Ya Swahaba: Maana, Wasifu Wao Kwa Mukhtasari

 

‘Abdullaah Bin ‘Amr Ibn Al-‘Aasw (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Jina Lake:  ‘Abdullaah bin ‘Amr Ibn Al-‘Aasw

 

(Al-Qurayshiyy)

عبد الله بن عمر بن العاص

 

Maana Yake:   Mja wa Allaah.

 

 

Wasifu Wake:

 

 

‘Abdullah ibn ‘Amr ibn Al-‘Aasw (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)  alikuwa ni mtoto wa Swahaba mashuhuriAmr ibn Al-‘Aasw  (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ). Alikusanya Hadiyth nyingi za Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم).

 

 

‘Abdullaah   alijitolea kwa bidii kuhudumia Dini ya Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى) kupita kiasi mpaka alilazimishwa na baba yake kuoa.   Usiku wa Nikaah yake alimuomba   mke wake (biharusi) ruhusa ili aswali rakaa mbili. Kutokana na khushuu ya Swalaah yake, akajisahau aliendelea na Swalaah mpaka Adhaan ya Alfajiri. Siku   ya pili alikaa na mke wake ilipofika usiku alimwomba tena ruhusa mke wake aende akaswali rakaa mbili. Akapitiza tena mpaka Adhaan ya Alfajiri. Alirudia tena hivo hivo siku ya tatu. ‘Amr ibn Al-‘Aasw alienda kumtembelea mke wa mwanae na kumuulizia mwanae ‘Abdullaah. Yule mke alimweleza kuhusu ‘Abdullaah na ‘ibaadah zake. Yule baba alimchukua mwanae na kumpeleka kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) ili amkumbushe haki za wengine na haki za miili yetu. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم)   alimweleza ‘Abdullaah  kwamba aswali usiku na pia awe analala, afunge (Swiyaam) siku chache na aache siku zingine, aupe mwili wake mwili haki, ampe  mke wake haki, na hata wageni wake awape haki zao.

 

    

Kufariki Kwake:

 

‘Abdullaah bin ‘Amr ibn Al-‘Aasw (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)  alifariki Misr na alizikwa kwenye nyumba yake ndogo mwaka 65AH. Hakuzikwa kwenye makaburi alizikwa nyumbani kwasababu   ya mfarakano wa jeshi dhidi ya Marwaan.

 

  

Share