U-Majina Ya Swahaba: Maana, Wasifu Wao Kwa Mukhtasari: 'Uwaymir Bin Zayd (Abu Dardaa)

A-Majina Ya Swahaba: Maana, Wasifu Wao Kwa Mukhtasari

 

 

‘Uwaymir Bin Zayd (Abu Dardaa)  (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)  

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Jina Lake: ‘Uwaymir Bin Zayd (Abu Dardaa)

 

Al-Answaariy

   عويمر بن زيد

 

 

Maana Yake:

 

‘Uwaymir -  (Kifupisho Cha ‘Aamir) Maana yake ni kuthibitika katika Iymaan, harufu nzuri, mwenye utulivu, mwenye kuamirisha, mjenzi, mwenye kupitisha umri mrefu  

 

Wengine wasema jina lake ni ‘Uwaymiyr bin ‘Aamir, au ‘Uwaymir bin ‘Abdullaah, au ‘Uwaymir bin Tha’labah.

 

 

Dardaa Maana yake ni Lulu ya hikmah

 

 

Wasifu Wake:

 

Abu Dardaa (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alikuwa tajiri na maarufu huko Madiyna na kila mtu alimpenda na kumheshimu.

 

Ni Swahaba mwenye hekima na busara. Abu Dardaa (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) hakuzaliwa kwenye Uislaam, bali  alisilimu baada ya vita vya Badr.

 

Iymaan yake katika Uislaam ilikuwa kutokutilia umuhimu wa kuwa na utajiri wa kidunia. Alisema “Nilikuwa mfanyabiashara kabla ya Unabiy wa Nabiy Muhammad (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم). Wakati     Uislamu ulipokuja, nilitafuta kuchanganya biashara na ‘ibaadah lakini hivi viwili havikuungana hivyo niliachana na biashara na nikachagua ‘ibaadah.

 

 

Kufariki Kwake:

 

Abu Dardaa (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alifariki akiwa na umri wa miaka 72. Kaburi lake lipo ndani ya Msikiti wa jina lake; Abu Dardaa huko Damascus mjini Syria.

 

 

 

 

 

 

Share