08-Uswuul Al-Fiqhi: Maswahaba Ambao Walitoa Fatwa Kipindi Cha Maisha Ya Mtume

 

Maswahaba ambao walitoa Fatwa kipindi cha maisha ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni: Abu Bakr, ‘Uthmaan, ‘Aliyy, ‘Abdur- Rahmaan bin ‘Awf, ‘Abdullaah bin Mas’uud, ‘Ubayd bin Ka’ab, Mu’aadh bin Jabal, ‘Ammaar bin Yaasir, Hudhayfah bin al-Yamaaniy, Zayd bin Thaabit, Abu ad-Dardaa, Abu Muusa al-‘Ash’ariy na Salmaan al-Faarisiy, Allaah Awe Radhi nao wote.

 

Maswahaba wengine walitoa Fatwa nyingi kuliko wengine. Wale ambao walitoa Fatwa nyingi ni: ‘Aaishah Ummul Mu’miniyn, ‘Umar bin al-Khattwaab, na mwanawe ‘Abdullaah, ‘Aliyy bin Abi Twaalib, ‘Abdullaah bin ‘Abbaas na Zayd bin Thaabit. Fatwa ambazo zilitolewa na yeyote kati ya hawa sita zinaweza kujaza kitabu kikubwa. Kwa mfano, Abu Bakr Muhammad bin Muussa bin Ya’quub bin al-Khalyfah Ma’muun alikusanya Fatwa za Ibn ‘Abbaas kwa vitabu ishirini.

 

Wale ambao wana idadi ya chini za Fatwa wamepokewa kuwa ni: Ummu Salamah Ummul Mu’uminiyn, Anas ibn Maalik, Abu Sa’iyd al-Khudriyy, Abu Hurayrah, ‘Uthman bin ‘Affaan, ‘Abdullaah bin Amr bin al-‘Aasw, ‘Abdullaah bin Zubayr, Abu Muusa al-Ash’ariy, Sa’iyd bin Abi Waqqaas, Salmaan al- Faarisiy, Jaabir bin ‘Abdullaah, Mu’aadh bin Jabal na Abu Bakr asw-Swiddiyq. Fatwa za mmoja kati ya hawa kumi na tatu zinajaza sehemu ndogo tu ya kitabu.

 

Orodha hii inaweza kuongezwa kwa Twalhah, az-Zubayr, ‘Abdur-Rahmaan bin Awf, ‘Imraan bin Huswayn, Abu Bakr, ‘Ubaydah bin asw-Swaamit na Mu’awiyah bin Abi Sufyaan. Waliobaki wametoa idadi chache za Fatwa, na mmoja au wawili tu kwenye matukio mengine zimesimuliwa kutoka kwa yeyote kati yao. Fatwa zao zinaweza kukusanywa kwenye kitabu kidogo, lakini baada tu ya kufanya uchunguzi na kuunganisha vipande vipande kwa hali ya juu[1].

 

Katika kutayarisha Fatwa zao, Maswahaba walikuwa wakipambanisha tukio moja moja lililowahi kuwatokea na suala linalofanana ambalo hukumu imetolewa katika maandiko ya Qur-aan na Sunnah. Hivyo, kulirudisha kuangalia maana na uhalisia wa kisheria kwa kujaribu na maandiko kwenye maana halisi ya neno, makusudio yake, na maelezo mengine yoyote yenye kunasibiana.

Baada ya kufikia maamuzi, watawaeleza wengine namna walivochambua mijadala yaliyowapelekea kwenye maamuzi, aidha kama ikiwa zimefikiwa kutoka kwenye herufi za maandiko au kutoka kwenye chanzo chake na watu watawafuata wao. Hakika, wanachuoni hawa wa Kiislamu wa mwanzo hawakusita kuchunguza suala mpaka kufikia katika uamuzi utakaojitesheleza nao, na mpaka wawe hakika wametosheka kwamba wamefanya jitihada zao za juu na hawawezi tena kuendelea.

  

[1] Angalia Ibn Hazm, Al-Ihkaam, Mj. uk. 92-93.

 

 

 

 

Share