14-Uswuul Al-Fiqhi: Wakati Wa ‘Aliy Ibn Abi Twaalib (Radhiya Allaahu ‘Anhu)

 

Wakati Wa ‘Aliy Ibn Abi Twaalib (Radhiya Allaahu ‘anhu)

 

 

‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alikuwa kama ‘Umar ibn al Khattwaab (Radhiya Allaahu ‘Anhu), kwa maana ya kwamba alielewa na kutumia maandiko ya Qur-aan na akijali sana kuunganisha masuala fulani kwa misingi ya jumla. Kabla ya kushikilia ofisi ya Khaliyfah, alitambulika kuwa jaji bora Madiynah.

 

Pale (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomteua ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) kuwa ni jaji nchini Yemen. Yeye (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimuombea dua, akisema: “Ewe Mola, Uongoze moyo wake na mfanye atamke ukweli.” Hakika, ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alithibitisha kuwa ni jaji bora, na alitatua kesi ngumu kwa wingi.

 

‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alielezea elimu yake kwa kusema: “Kwa Allaah, hakuna aya ya Qur-aan iliyowahi kuteremshwa isipokuwa nilijua nini ilishushwa, wapi na kwanini ilishushwa. Mola wangu Ameniwekea juu yangu moyo ambao unafahamu na ulimi wenye kutamka vyema.”

 

Wakati wowote linapopelekwa jambo kwa ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) kwa maamuzi atalikubali bila ya kusita. Na kama ataulizwa kutoa Fatwa, atafanya hivyo kwa kuisoma kutoka Kitabu cha Allaah, na baadae Sunnah ya (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hakika, undani wa elimu ya Qur-aan na Sunnah ulijulikana vizuri sana.

 

‘Aishah (Radhiya Allaahu ‘Anha) alisema: “Kwa mnasaba wa Sunnah ya (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), alikuwa ni mbora na maarufu kuliko watu wote.”

 

‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alikuwa akitengeneza maana yake mwenyewe kwa njia ya Ijtihaad ikiegemezwa katika al Qiyaas, al Istis-haab[1], al Istihsaan[2], na al Istislaah[3], mara zote akiegemeza mawazo yake kwenye madhumuni mapana ya Shari’ah pindi anaposhauriwa kuhusu uwezekano wa kuengezeka Hadd-adhabu inayopatikana kwa yule aliyepatikana na hatia ya kunywa ulevi, alipambanisha ulewaji wa msingi usiokuwa sahihi kwamba ulewaji unaweza kumpelekea mtu kufanya tuhuma kama hizo.

 

Wakati wa Khilaafah yake, ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alimtaka ushauri ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) kuhusiana na adhabu ya kundi la watu walioafikiana kwa pamoja kukusudia kufanya mauaji. ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alisema, “Ewe Kiongozi wa Wakweli! Kama kundi la watu watakusanyika pamoja katika kuiba, je, hutokata mkono mmoja wa kila mmoja?” Pale ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alipojibu kwa kukubali, ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alisema, “Ndivyo, hivyo inavokuwa kwa kesi hii.” Kwa sababu hiyo, ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alitamka msemo wake maarufu: Kama raia wote wa Swan’aa watakubalina kwa pamoja kumuua mtu mmoja, nitawaadhibu kifo wengi kati yao.”

 

Mfanano baina ya mauaji na wizi ulifanywa kwa sababu katika kila kesi kuna msukumo wa kijinai uliogaiwa baina yao wote waliotenda matendo hayo, na ni hili linalofanya adhabu kuwa yenye kutisha.

 

Juu ya hivyo, ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alipendelea kuwachoma moto wakiwa hai wale walioritadi kwa nguvu na wazushi waliomzulia, ijapokuwa alikuwa anaelewa vyema kwamba maamuzi ya Sunnah yapo laini kumuweka asiyeamini kama huyo na walioritadi kwenye adhabu ya kifo. Katika maamuzi haya, ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alionesha yeye mwenyewe kuwa na bidii kuanzisha adhabu kali na yenye kuzuia kuliko adhabu nyengine yoyote ya murtaddi, kwa sababu alitambua kuwa suala hili ni nyeti sana. Hivyo, alianzisha adhabu kali mno kwa tendo kama hilo, ili kuwaogopesha watu kulitenda. Juu ya hivyo, ili kusisistiza hili, hapo hapo alinukuu ubeti ufuatao wa shairi:

 

“Nilipotambua namna jambo lilivyo zito,

Nikawasha moto mkubwa na kusimama kwa ajili ya Qanbar.”

 

Pale ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alipomsikia mwanamke ambaye mumewe alikuwa nje kwa safari za kijeshi na ambaye nyumbani kwake watu asiowajua walikuwa wakimjia. Hivyo, ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) akampelekea ujumbe kwamba asipokee wageni pale mumewe anapokuwa hayupo. Pale huyo mwanamke aliposikia kwamba Khaliyfah anataka kuzungumza naye, alifikwa na woga, na kwa vile alikuwa mjamzito, aliharibu mimba akiwa njiani kumuona ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu).

 

‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alikereka sana kwa lile lililotokea, aliwataka ushauri Swahaabah kuhusiana na jambo hilo. Miongoni mwao, alikuwa ‘Uthmaan ibn ‘Affaan, na ‘Abdur-Rahmaan ibn ‘Awf, walimuhakikishia: “Hukufanya jambo isipokuwa ukijaribu kumuelimisha, hukufanya jambo baya.”

 

Baadaye ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alimgeukia ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu), akimtaka mawazo yake. ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alijibu, “Watu hawa wamezungumza, na kama hili ni wazo bora walilokuja nalo juu, basi ni la uadilifu tosha. Lakini, kama wamezungumza tu kukuridhisha wewe, basi wamekulaghai. Nategemea kwamba Allaah Atakusamehe kwa kosa hilo, kwani Yeye Anatambua nia yako ilikuwa njema. Lakini, kwa Allaah, ulipe fidia kwa mtoto.”

 

‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alisema, “Kwa Allaah, umezungumza nami kwa utiifu. Naapa kwamba usikae chini hadi ugawe pesa hii miongoni mwa watu wako.”

 

 [1] Al-Istishaab: Kutambua mazingira katika utaratibu wa kutoa hoja ya kisheria.

[2] Al Istihsaan: Kuikubali Qiyaas-kufananisha ambayo inaonekana kuwa juu kisheria kwa kulinganisha na mfananisho ulio dhahiri. Ni katika maelezo hayo ambapo al Istihsaan inakuja kwa mara kadhaa kutafsiriwa kama ni “Hiari ya Mwanachuoni”.

[3] Al-Isislaah: Kutambua kisheria ustawi na hali njema za wote, mmoja mmoja na jamii kwa pamoja.

Share