Zakaatul-Fitwr: Kiwango Cha Zakaatul-Fitwr Ni Chakula Cha Masikini Mmoja Si Siku 30

Kiwango Cha Zakaatul-Fitwr Ni Chakula Cha Masikini Mmoja Si Siku 30

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

assalam aleikum

 

nilikuwa nataka kujua kiasi gani nitoe kwenye zakkatul fitr, na hizo kilo ni za siku 30? naomba nifafanulia

ahsante

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himdi Anastahiki Allaah Rabb wa walimwengu Swalaah na salamu zimshukie kipenzi chetu Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Kiwango cha Zakaatul-Fitwr ni saa' moja ambayo takriban ni kilo mbili na nusu ya chakula kinachotumika sana katika mji unaotoa Zakaah. Kwa hiyo ikiwa uko pekee yako basi ni saa' moja. Ikiwa una familia basi kila mmoja umtolee Zakaatul-Fitwr ya kiwango hicho hicho na sio kulipia siku 30.

 

Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate faida zaid kuhusu Zakaatul-Fitwr

Fataawaa: Za Zakaatul-Fitwr

Fataawaa: Mukhtasari Wa Fataawaa Za Zakaatul-Fitwr

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share