Nini Tofauti Ya Mitihani Ya Mwana Aadam Kulinganisha Na Mitihani Ya Allaah?

 

Nini Tofauti Ya Mitihani Ya Mwana Aadam Kulinganisha Na Mitihani Ya Allaah?

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Mitihani Ya Mwana Aadam:

 

Inahitajika kusoma vitabu vingi na mwanafunzi inambidi afanye juhudi kubwa na kwa mashaka kusoma hadi apasi mitihani yake

 

 

 

Mitihani Ya Allaah:

 

Kitabu kimoja tu chepesi kukisoma nacho ni Qur-aan.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

إِنَّ هَـٰذَا الْقُرْآنَ يَهْدِي لِلَّتِي هِيَ أَقْوَمُ وَيُبَشِّرُ الْمُؤْمِنِينَ الَّذِينَ يَعْمَلُونَ الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ أَجْرًا كَبِيرًا ﴿٩﴾

Hakika hii Qur-aan inaongoza katika yaliyonyooka kabisa, na inawabashiria Waumini wanaotenda mema kwamba watapata ujira mkubwa.  [Al-Israa: 17:9]

 

كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ مُبَارَكٌ لِّيَدَّبَّرُوا آيَاتِهِ وَلِيَتَذَكَّرَ أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٢٩﴾

Kitabu Tumekiteremsha kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) chenye Baraka, ili wapate kuzingatia kwa makini Aayaat zake, na ili wapate kukumbuka wenye akili.  [Swaad 38: 29]

 

 

Mitihani Ya Mwana Aadam

 

Mitihani ya binaadamu haijulikani ni maswali yepi yatakayokuja kabla ya mitihani

 

 

Mitihani Ya Allaah

 

Maswali tayari yameshajulikana kama;

Nani Rabb Wako

Ipi Dini Yako

Nani Nabiy wako?

Umeutumiaje ujana wako?

Umeipata vipi mali yako na umeitumiaje?

Umri wako umeutumia vipi?

Elimu yako umeitumiaje?

 

Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

 يُثَبِّتُ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ . قال : نزلت في عذابِ القبرِ . يقالُ له : مَنْ ربُّك ؟ فيقولُ : ربِّيَ اللهُ ، وديني دينُ محمدٍ . فذلك قوله : يُثَبِّتُ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ

Allaah Huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti katika uhai wa dunia na Aakhirah. Amesema: Imeteremka kuhusu adhabu ya kaburi. Huulizwa: Nani Rabb Wako? Husema: Rabbi wangu ni Allaah, na Dini yangu ni Dini ya Muhammad” basi hiyo ndio kauli Yake: Allaah Huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti katika uhai wa dunia na Aakhirah [Imepokelewa kutoka kwa Al-Baraa bin ‘Aazib (Radhwiya Allaahu 'anhu) - Swahiyh An-Nasaai (2056), riwaayah nyenginezo kama hizo katika Al-Bukhaariy, Muslim]

 

عَنْ أَبِي بَرْزَةَ الأَسْلَمِيِّ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((لاَ تَزُولُ قَدَمَا عَبْدٍ يَوْمَ الْقِيَامَةِ حَتَّى يُسْأَلَ عَنْ عُمْرِهِ فِيمَا أَفْنَاهُ وَعَنْ عِلْمِهِ فِيمَا فَعَلَ وَعَنْ مَالِهِ مِنْ أَيْنَ اكْتَسَبَهُ وَفِيمَا أَنْفَقَهُ وَعَنْ جِسْمِهِ فِيمَا أَبْلاَهُ))‏ ‏.‏ قَالَ هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ ‏.‏

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Barazh Al-Aslamiyy kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mguu wa mja hautaondoka Siku ya Qiyaamah mpaka auliziwe (matano); umri wake kautumiaje, elimu yake kaifanyia nini, mali yake kaichumaje na kaitoaje, mwili wake kauchakaa vipi)) [At-Tirmidhiy amesema HAdiyth Hasan Swahiyh, Swahiyh At-Tirmidhiy (2417), na riwaayah nyengine Taz Swahiyh Al-Jaami’ (7300)]

 

 

 

 

Mitihani Ya Mwana Aadam

 

Hupewi majibu kabla ya mitihani.

 

 

Mitihani Ya Allaah

 

Majibu yako tayari katika Qur-aan na Sunnah unaweza kuyapata na kuyafanyia kazi.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

مَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُ حَيَاةً طَيِّبَةً ۖ وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٩٧﴾

Mwenye kutenda mema miongoni mwa wanamume au wanawake naye ni Muumin, Tutamhuisha uhai mzuri, na bila shaka Tutawalipa ujira wao kwa mazuri zaidi ya yale waliyokuwa wakitenda.  [An-Nahl: 16]

 

 

 

Mitihani Ya Mwana Aadam

 

Waalimu waliochaguliwa kufundisha masomo ya mitihani hiyo wanaweza kukosea

 

Mitihani Ya Allaah

 

Waalimu waliochaguliwa na Allaah kusimamia na kufundisha mitihani, ni Ma’aswumiyn (Wamelindwa na makosa) nao ni Manabii.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kuhusu Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٣﴾

Na wala hatamki kwa hawaa.

 

إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ ﴿٤﴾

Hayo si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa. [An-Najm 53: 3-4]

 

 

 

 

Mitihani Ya Mwana Aadam

 

Muda wa mitihani haizidi masaa.

 

Mitihani Ya Allaah

 

Muda wa mitihani unaweza kufika hadi miaka 70 au zaidi ambao ni umri wa mwana Aadam!

 

عَنْ أَبِى هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((أَعْمَارُ أُمَّتِي مَا بَيْنَ سِتِّينَ إِلَى سَبْعِينَ ، وَأَقَلُّهُمْ مَنْ يَجُوزُ ذَلِكَ))  رواه الترمذي وغيره ، وقَالَ : حَدِيثٌ حَسَنٌ غَرِيبٌ ، وحسنه الألباني رحمه الله في الصحيحة 2/385   .

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Umri wa ummah wangu ni baina ya (miaka) sitiini na sabiini, na wachache wao watakavuka hiyo)) [At-Tirmidhiy na wengineo na amesema: Hadiyth Hasan Ghariyb na ameipa daraja ya Hasan Al-Albaaniy katika Asw-Swahiyhah (2/385)]

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِن كُنتُمْ فِي رَيْبٍ مِّنَ الْبَعْثِ فَإِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ مِن نُّطْفَةٍ ثُمَّ مِنْ عَلَقَةٍ ثُمَّ مِن مُّضْغَةٍ مُّخَلَّقَةٍ وَغَيْرِ مُخَلَّقَةٍ لِّنُبَيِّنَ لَكُمْ ۚ وَنُقِرُّ فِي الْأَرْحَامِ مَا نَشَاءُ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ثُمَّ نُخْرِجُكُمْ طِفْلًا ثُمَّ لِتَبْلُغُوا أَشُدَّكُمْ ۖ وَمِنكُم مَّن يُتَوَفَّىٰ وَمِنكُم مَّن يُرَدُّ إِلَىٰ أَرْذَلِ الْعُمُرِ لِكَيْلَا يَعْلَمَ مِن بَعْدِ عِلْمٍ شَيْئًا ۚ وَتَرَى الْأَرْضَ هَامِدَةً فَإِذَا أَنزَلْنَا عَلَيْهَا الْمَاءَ اهْتَزَّتْ وَرَبَتْ وَأَنبَتَتْ مِن كُلِّ زَوْجٍ بَهِيجٍ ﴿٥﴾

Enyi watu!  Mkiwa mko katika shaka ya kufufuliwa; basi hakika Sisi Tumekuumbeni kutokana na mchanga, kisha kutokana na manii, kisha pande la damu linaloning’inia, kisha, kinofu cha nyama na kinachotiwa umbo, na kisichotiwa umbo, ili Tukubainishieni. Na Tunakikalisha katika fuko la uzazi Tukitakacho mpaka muda maalumu uliokadiriwa. Kisha Tunakutoeni hali ya mtoto, kisha ili mfikie umri kupevuka kwenu; na miongoni mwenu yule anayefishwa, na miongoni mwenu yule anayerudishwa kwenye umri mbaya na dhaifu zaidi hata awe hajui kitu chochote kile baada ya elimu (yake). Na utaona ardhi kame, lakini Tunapoiteremshia maji hutikisika na kuumuka, na inaotesha mimea ya kila namna; anisi mizuri. [Al-Hajj 22:5]

 

 

 

Mitihani Ya Mwana Aadam

 

Fursa ya kurudia mtihani baada ya kufeli ni mara chache tu, hata hivyo hakuna dhamana kuwa ndio kufuzu

 

Mitihani Ya Allaah

 

Fursa ya kurudia mtihani ipo wazi hadi kabla ya mauti ya mwana Aadam na dhamana ya kufuzu ipo madamu tu utajaribu!

 

قال النبي صلى الله عليه وآله وسلم: ((إنّ الله يقبلُ توبةَ العبد ما لم يُغرغِر))

Amesema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Hakika Allaah Anapokea tawbah ya mja Wake kabla ya roho kufika kwenye mkoromo wa mauti)) [Swahiyh At-Tirmidhiyy (3537) na wengineo]

 

Na pia:

 

عَنْ أَبِي مُوسَى عَبْدِ الله بنِ قَبَسٍ الأَشْعَرِيِّ  (رضي الله عنه) عن النَّبيّ (صلى الله عليه و آله وسلم) قال: ((إِنَّ اللَّهَ تَعَالَى يَبْسُطُ يَدَهُ بِاللَّيْلِ لِيَتُوبَ مُسِيءُ النَّهَارِ وَيَبْسُطُ يَدَهُ بِالنَّهَارِ لِيَتُوبَ مُسِيءُ اللَّيْلِ حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ مِنْ مَغْرِبِهَا)) رواه مسلم

Imepokelewa kutoka kwa Abu Muwsaa ‘Abdillaah bin Qays Al-Ash‘ariyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika Allaah Anakunjua Mkono Wake usiku ili Apokee tawbah ya mkoseaji mchana. Na Anakunjua Mkono Wake mchana ili Apokee tawbah ya mkoseaji usiku mpaka jua lichomoze Magharibi [mahali linapokuchwa])) [Muslim]

 

 

Mitihani Ya Mwana Aadam

 

Daraja unayopewa haizidi 100%

 

 

Mitihani Ya Allaah

 

Daraja yake kubwa ni 700 na Allaah Huzidisha zaidi Atakavyo.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

مَّثَلُ الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ كَمَثَلِ حَبَّةٍ أَنبَتَتْ سَبْعَ سَنَابِلَ فِي كُلِّ سُنبُلَةٍ مِّائَةُ حَبَّةٍ ۗ وَاللَّـهُ يُضَاعِفُ لِمَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٦١﴾ 

Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika njia ya Allaah ni kama mfano wa punje moja ya mbegu iliyotoa mashuke saba, katika kila shuke kuna punje mia. Na Allaah Humzidishia Amtakaye; na Allaah ni Mwenye wasaa, Mjuzi wa yote. [Al-Baqarah 2: 261]

 

Na

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَظْلِمُ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ ۖ وَإِن تَكُ حَسَنَةً يُضَاعِفْهَا وَيُؤْتِ مِن لَّدُنْهُ أَجْرًا عَظِيمًا﴿٤٠﴾

Hakika Allaah Hadhulumu hata uzito au chembe (au sisimizi). Na ikiwa ni ‘amali njema Huizidisha na Hutoa kutoka Kwake ujira adhimu. [An-Nisaa 4: 40]

 

 

 

Mitihani Ya Mwana Aadam

 

Matokeo yake yaani kufuzu kwake ni ya kidunia pekee

 

 

Mitihani Ya Allaah

 

Matokeo na kufuzu kwake ni duniani na Akhera pia.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)

 

مَّن كَانَ يُرِيدُ ثَوَابَ الدُّنْيَا فَعِندَ اللَّـهِ ثَوَابُ الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ سَمِيعًا بَصِيرًا﴿١٣٤﴾

Anayetaka thawabu za dunia basi kwa Allaah kuna thawabu za dunia na Aakhirah. Na Allaah daima ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.  [An-Nisaa 4: 134]

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَمَن يُرِدْ ثَوَابَ الدُّنْيَا نُؤْتِهِ مِنْهَا وَمَن يُرِدْ ثَوَابَ الْآخِرَةِ نُؤْتِهِ مِنْهَا ۚ وَسَنَجْزِي الشَّاكِرِينَ ﴿١٤٥﴾ 

Na yeyote anayetaka thawabu za dunia Tutampa katika hizo. Na yeyote anayetaka thawabu za Aakhirah Tutampa katika hizo; na Tutawalipa wanaoshukuru.  [Aal-‘Imraan 3: 145]

 

 

Mitihani Ya Mwana Aadam

 

Husahau mtihani baada ya muda

 

 

Mitihani Ya Allaah

 

Haisahauliki kwani imehifadhika katika Lawhum Mahfuwdhw (ubao uliohifadhiwa)

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

إِنَّا نَحْنُ نُحْيِي الْمَوْتَىٰ وَنَكْتُبُ مَا قَدَّمُوا وَآثَارَهُمْ ۚ وَكُلَّ شَيْءٍ أَحْصَيْنَاهُ فِي إِمَامٍ مُّبِينٍ ﴿١٢﴾

Hakika Sisi Tunahuisha wafu, na Tunaandika yale waliyoyakadimisha na athari zao na kila kitu Tumekirekodi barabara katika daftari bayana.  [Yaasiyn 36: 12]

 

 

 

Mitihani Ya Mwana Aadam

 

Zawadi yake ni karatasi na wino (shahada) ambayo itatoweka tu

 

 

Mitihani Ya Allaah

 

Zawadi yake ni Jannah ya kudumu daima bila ya kubadilika hali yake

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ كَانَتْ لَهُمْ جَنَّاتُ الْفِرْدَوْسِ نُزُلًا ﴿١٠٧﴾

Hakika wale walioamini na wakatenda mema, watapata Jannaat za Al-Firdaws kuwa ni mahali pao pa makaribisho.

خَالِدِينَ فِيهَا لَا يَبْغُونَ عَنْهَا حِوَلًا ﴿١٠٨﴾

Ni wenye kudumu humo hawatotaka kuihama. [Al-Kahf 18: 107-108]

 

Na Anasema pia:

 

وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّـهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَن يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّـهُ وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَىٰ مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ﴿١٣٥﴾

Na wale ambao wanapofanya machafu au wakajidhulumu nafsi zao (kwa maasi), humdhukuru Allaah wakaomba maghfirah kwa madhambi yao. Na nani anayeghufuria madhambi isipokuwa Allaah. Na hawaendelei katika waliyoyafanya na wao wanajua.

أُولَـٰئِكَ جَزَاؤُهُم مَّغْفِرَةٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَجَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ وَنِعْمَ أَجْرُ الْعَامِلِينَ ﴿١٣٦﴾

136. Hao jazaa yao ni maghfirah kutoka kwa Rabb wao na Jannaat zipitazo chini yake mito, ni wenye kudumu humo. Na uzuri ulioje ujira wa watendaji (wema). [Aal-‘Imraan 3: 135-136]

 

 

 

Mitihani Ya Mwana Aadam

 

Inabidi utoke uende masafa shuleni au chuoni

 

 

Mitihani Ya Allaah

 

Unaweza kufanya mtihani ukiwa nyumbani kwako kwa kufanya ‘ibaadah na kuomba ufuzu.

 

عَنْ زَيْدِ بْنِ ثَابِتٍ رضى الله عنه قَالَ: احْتَجَرَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم حُجَيْرَةً مُخَصَّفَةً أَوْ حَصِيرًا، فَخَرَجَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يُصَلِّي فِيهَا، فَتَتَبَّعَ إِلَيْهِ رِجَالٌ وَجَاءُوا يُصَلُّونَ بِصَلاَتِهِ، ثُمَّ جَاءُوا لَيْلَةً فَحَضَرُوا وَأَبْطَأَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم عَنْهُمْ، فَلَمْ يَخْرُجْ إِلَيْهِمْ فَرَفَعُوا أَصْوَاتَهُمْ وَحَصَبُوا الْبَابَ، فَخَرَجَ إِلَيْهِمْ مُغْضَبًا فَقَالَ لَهُمْ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((مَا زَالَ بِكُمْ صَنِيعُكُمْ حَتَّى ظَنَنْتُ أَنَّهُ سَيُكْتَبُ عَلَيْكُمْ، فَعَلَيْكُمْ بِالصَّلاَةِ فِي بُيُوتِكُمْ، فَإِنَّ خَيْرَ صَلاَةِ الْمَرْءِ فِي بَيْتِهِ، إِلاَّ الصَّلاَةَ الْمَكْتُوبَةَ)) ‏  

Imepokelewa kutoka kwa Zayd bin Thaabit (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitengeneza sehemu ya chumba katika Msikiti kwa kutumia majani ya mtende au ya ukili.  Akatoka Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwenda kuswali hapo. Watu wakamfuata wakaja kuswali naye. Kisha wakaja tena usiku wakimsubiri lakini Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakutokea. Wakapandisha sauti zao wakarusha vijiwe mlangoni. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akawaghadhibikia na kuwaambia: ((Kwa hayo mliyokuwa mkiyafanya, nilielemea kudhania kwamba mtaandikiwa kuwajibika nayo.  Basi swalini majumbani mwenu kwani Swalaah bora kabisa ya mtu ni nyumbani kwake isipokuwa Swalaah za fardhi)) [Al-Bukhariy, Muslim na wengineo]

 

 

 

Mitihani Ya Mwana Aadam

 

Wakati au tarehe yake ni fulani tu

 

 

Mitihani Ya Allaah

 

Wakati wowote, siku yoyote katika uhai wako.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَهُوَ الَّذِي جَعَلَ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ خِلْفَةً لِّمَنْ أَرَادَ أَن يَذَّكَّرَ أَوْ أَرَادَ شُكُورًا ﴿٦٢﴾

62. Naye Ndiye Aliyejaalia usiku na mchana ufuatane kwa atakaye kukumbuka au atakaye kushukuru. [Al-Furqaan 25: 62]

 

Na pia:

  عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ بُسْرٍ، أَنَّ أَعْرَابِيًّا، قَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ! مَنْ خَيْرُ النَّاسِ؟  قَالَ: ((مَنْ طَالَ عُمُرُهُ وَحَسُنَ عَمَلُهُ ))‏

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaahi bin Busr kwamba Bedui mmoja alisema: Ee Rasuli wa Allaah! Nani mtu bora kabisa? Akasema: ((Ambaye umri wake umerefuka na ‘amali zake zikawa nzuri)) [Jaami’ At-Tirmidhiy Kitaab Az-Zuhd, Swahiyh At-Targhiby (3364)

 

 

Mitihani Ya Mwana Aadam

 

Masikini anaweza asijimudu kulipia mtihani

 

 

Mitihani Ya Allaah

 

Masikini au fakiri wote wanaweza kutekeleza mtihani wa Allaah.

 

Allaah Amewafadhilisha Waumini masaakiyn kuliko makafiri wenye mali Alipomwambia Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

وَاصْبِرْ نَفْسَكَ مَعَ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ ۖ وَلَا تَعْدُ عَيْنَاكَ عَنْهُمْ تُرِيدُ زِينَةَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَلَا تُطِعْ مَنْ أَغْفَلْنَا قَلْبَهُ عَن ذِكْرِنَا وَاتَّبَعَ هَوَاهُ وَكَانَ أَمْرُهُ فُرُطًا ﴿٢٨﴾

28. Na isubirishe nafsi yako pamoja na wale wanaomuomba Rabb wao asubuhi kabla jua kucha na jioni, wanataka Wajihi Wake. Na wala macho yako yasiwavuke kwa kutaka pambo la uhai wa dunia. Na wala usimtii Tuliyemghafilisha moyo wake na Ukumbusho Wetu akakafuata hawaa zake, na jambo lake limekuwa la kuzidi kuvuka mipaka. [Al-Kahf 18: 28]

 

 

Na pia:

يدخلُ فقراءُ المسلمين الجنَّةَ قبل الأغنياءِ بنصفِ يومٍ ، وهو خمسُمائةِ عامٍ

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Masikini wa Kiislamu wataingia Jannah kabla ya matajiri kwa nusu siku  nayo ni miaka mia tano)) [Ibn Maajah, At-Tirmidhiy, taz Swahiyh At-Tirmidhiy (2354), Swahiyh Al-Jaami’ (8076)

 

 

 

Mitihani Ya Mwana Aadam

 

Kunaweza kutokea upendeleo akadhulumiwa mwana Aadam asipewe natija anayostahiki

 

 

Mitihani Ya Allaah

 

Hadhulumiwi mtu hata chembe ya khardal, atalipwa mwana Aadam kila kitu!

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَوُضِعَ الْكِتَابُ فَتَرَى الْمُجْرِمِينَ مُشْفِقِينَ مِمَّا فِيهِ وَيَقُولُونَ يَا وَيْلَتَنَا مَالِ هَـٰذَا الْكِتَابِ لَا يُغَادِرُ صَغِيرَةً وَلَا كَبِيرَةً إِلَّا أَحْصَاهَا ۚ وَوَجَدُوا مَا عَمِلُوا حَاضِرًا ۗ وَلَا يَظْلِمُ رَبُّكَ أَحَدًا ﴿٤٩﴾

Na kitawekwa Kitabu, basi utaona wahalifu ni wenye khofu kwa yale yaliyokuwemo ndani yake; na watasema: “Ole wetu! Kitabu hiki kina nini, hakiachi dogo wala kikubwa isipokuwa kimerekodi hesabuni.” Na watakuta yale waliyoyatenda yamehudhuria. Na Rabb wako Hamdhulumu yeyote. [Al-Kahf 18: 49]

 

Na pia Anasema:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَظْلِمُ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ ۖ وَإِن تَكُ حَسَنَةً يُضَاعِفْهَا وَيُؤْتِ مِن لَّدُنْهُ أَجْرًا عَظِيمًا﴿٤٠﴾

Hakika Allaah Hadhulumu hata uzito au chembe (au sisimizi). Na ikiwa ni ‘amali njema Huizidisha na Hutoa kutoka Kwake ujira adhimu.  [An-Nisaa 4: 40]

 

 

Kwa hiyo ni maajabu makubwa kwa mtu kufuzu mitihani ya mwana Aadam na kufeli mitihani ya Rabb Muumbaji!

 

 

 

 

Share